Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Kimsingi wewe ni mbishi. Yaani mfano tungekuwa tunaongelea pombe, wenzako tunaongelea madhara ya pombe kwenye afya ya mtu m'moja m'moja na jamii kwa ujumla wewe unakuja na hoja za pombe kama pombe inazo faida kama kupeana dili bar, mapato kwa serikali, kutoa ajira kwa wahudumu wa bar, na kiwanda cha pombe plus wadangaji wanaovuna pesa za walevi.Yawezekana mama yako mdogo aliamua tu kugive up na kukubaliana na upumbavu wa wanaume ili mradi maisha yaende, yani wanaume mnachotaka ni wanawake wakubaliane tu na upumbavu wenu kwa sababu mmeshawajengea ile mentality ya kwamba wanaume hawawezi kubadilika, kwahiyo kinachotokea baada ya wanawake kufika umri fulani ni ile hali ya kuamua tu kufunika kombe mwanaharamu apite lakini si kwamba eti wanaume ndio mnakuwa mko sahihi sasa si kila mwanamke atakubali hilo
Sasa kama wapo mbona migogoro kwenye ndoa haiishi, hapo ndipo mnaponishangaza yani mnadai kwamba mnaoa wanawake wenye mienendo mizuri tu, ila cha ajabu migogoro kwenye ndoa haiishi na walalamikaji ni wanaume mara nyingi
Si unaona hivi kati ya mimi na wewe nani anayeandika uhalisia na nani anayeandika mawazo yake tu yani unadai kwamba wanawake wanaweza kuanza mahusiano wakiwa na miaka 18 na baada ya miaka 3 wanaweza kuolewa hebu niambie ni wanawake wangapi leo hii wanakubali kuolewa wakiwa kwenye early 20s na ndoa zao zikadumu, hivi siyo wewe kuna mjadala fulani tulikuwa tunabishana ukasema kwamba wanawake wengi wakitangaziwa ndoa katika umri mdogo huwa wanakataa wanasema hawako tayari wanasubiri hadi umri ukishaenda wakishaharibiwa na wakishazalishwa ndio wanaanza kutafuta ndoa halafu leo unasema eti wanawake wanaweza kuolewa katika umri mdogo, isitoshe wanaume wengi huwa wanakiri wenyewe kwamba wanawake wa siku hizi ukiwaoa mapema wanakuwa bado wana akili za kitoto hivyo huanza kusumbua kwenye ndoa na kupelekea ndoa nyingi kuwa na migogoro na kuishia kwenye talaka halafu wewe unakuja kusema nini hapa
Bado swali langu ni lile lile kama hamchukui wanawake wa sampuli hizo kwanini sasa ndoa nyingi leo hii ni migogoro kila kukicha au chanzo cha hiyo migogoro ni ninyi wanaume, mimi nilitegemea kwamba kwa sababu huwa mnaoa wake wema kama mnavyojisifia humu mitandaoni basi ndoa zote zitakuwa na furaha but unfortunately that is not the case sasa hiyo tafsiri yake ni nini, na ndio maana nasema wanaume wengi mnachoandika humu mitandaoni ni tofauti na mnachofanya kwenye maisha halisi halafu mimi nikisema mnadai eti napingana na uhalisia sasa kati ya mimi na ninyi nani anapingana na uhalisia hapa
Sasa kama wameshatendwa na wanawake na wanazijua rangi zote na na maovu yote ya wanawake kwanini wanaendelea kuoa yani hapo mimi ndipo swali langu lilipo, mind you tumekubaliana ndoa ina umuhimu kwa mwanamke tu na siyo kwa mwanaume sasa kwanini wanaume wanaendelea kuoa kwenye hii dunia ya leo ambayo wanawake wengi ni pasua vichwa, usitudanganye hapa kwamba eti wanaume wana upendo na huruma sijui blah blah kama mnavyodai kwa sababu haiwezekani mtu akawa na upendo na huruma kwa mtu ambaye anamfanyia vitendo vya kumuumiza na kama hao wake wema wangekuwepo basi migogoro na talaka vingeshaisha kwenye hizo ndoa
Yaani hoja zako unazotoa bado upo nje ya context ya madhara ya jambo husika.
Sasa tazama unasema upumbavu wa wanaume nikikwambia unambie ni upi still utaongelea tabia mbaya ambazo hata wanaume tunazikemea kila siku hapa na hatuziungi mkono. Yet wanaume hawaji kuongea kwa nia ya kuponda wanawake wanaongea kwa nia ya kukemea na kuelimishana.
Wewe unakuja kutetea kwa lengo la "mkiharibu na sisi tuna haribu" sasa yupi anatetea upumbavu hapa?
Wewe umeshawahi kutana na mwanaume anaekosa mwanamke wa kuishi nae katika jamii hii ya watanzania hata huko duniani eti kwa kukosa? Labda atake mwenyewe kuishi kisela.
Ila wanawake ni wangapi wanazalishwa na wanatafuta ndoa kwa nguvu wanakosa na wengine wanaishi wenyewe bila wanaume sio kwa kutaka bali ni imewalazimu kukosa.
Kwa style hiyo bado unatumia akili za darasani kudhania uhalisia ni wanaume ndio wana mwisho mbaya kwasababu wao ndio wanaolalamika hapa mitandaoni?
You have a long way to learn. Labda kama unabishana for fun ila nina jua unajua chuya na mchele vipo wapi. Unapoteza tu muda na hizi hoja zako hakuna uhalisia.