Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MWANAUME BORA LAZIMA UMTOE OUT MKEO NA KUMNUNULIA ZAWADI. HAIWEZEKANI MWAKA MZIMA HUJAFANYA HIVYO. HUO NI USHENZI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Siku 365 na masaa kadhaa Mkeo na watoto wapo nyumbani kama gereza la Kinguruila. Kila siku kupika chakula hapo nyumbani huyo Mkeo hachoki tuu. Huyo Mkeo hakinaiwi tuu kila siku Kula chakula anachopika yeye
Hivi unaakili sawasawa?
Miezi kumi na mbili mwanamke hata kumnunulia zawadi, hata nguo ya elfu kumi tuu. Wapi! Hata kumnunulia kiatu cha elfu saba wapi!
Mkeo ananuka jasho kwa kukosa matunzo. Hata kumnunulia Sababu ya elfu mbili na perfume za elfu tanotano wapi!
Alafu unataka huyo mwanamke akuheshimu, akupende, akuchekee chekee. Mtu kafubaa kama nguo za gereji atapataje Hilo tabasamu?
Alafu wanaume wa aina hii ndio haohao utawakuta wakishupalia hawataki Mke afanye Kazi ili wamchitishe, wamfubaze kisha waseme wanawake wanawahi kuzeeka wakati wao ndio wamewazeesha. USHENZI mtupu!
MKE Hana furaha kwa sababu umeshindwa mambo madogo ataachaje kuzeeka.
Unakuta mdada wa Miaka 28 tuu kazeeka utadhani Anamiaka 50 huko.
Alafu unajiita Mwanaume. Hakuna mwanaume hapo.
Mwanaume ni majukumu. Kujua kuhudumia Mkeo na watoto
Kujua kutumia rasilimali za familia kuinufaisha familia na kuifanya iwe na furaha.
Unataka Mke awe kama Msukule wako hapo. Yaani yupoyupo. Ananuka mijasho. Kapauka na kufubaa. Anavaa nguo Moja kama Sanda ya maiti. Dadeki! Acha USHENZI dogo.
Wanawake wafanye Kazi. Nawe kama Mume lazima ufanye Kazi zaidi kuliko mkeo.
Mtoe Out Mkeo.
Amua siku Moja muende hata Hoteli ya Nyota tano mkalale huko. Mkafurahie maisha. Usitake kuniambia mwaka mzima mkijipanga utakosa pesa ya kujivinjari na Kula bata na familia.
Wanasome ndoa ndoani ni Makafiri, wapagani na Waabudu mashetani.
Haiwezekani mkutane watu mnaopendana kwa hiyari yenu alafu ati mje mseme Ndoa ndoani.
Kama kuna Mmoja alileta Utapeli, hakuwa anamaanisha, Fukuza, omba Talaka. Tafuta mwingine mnayeendana.
Hivyohivyo Mpaka upate.
Mashetani ndio hugeuza kitu kizuri kuwa Kibaya. Ndio hao wanaokuambia ukiingia ndoani mambo huwa Mabaya.
Haiwezekani wewe kila siku au kwa wiki unaenda Bar kujivinjari, unaenda kuangalia mipira huko kwenye mabanda umiza, unaagiza na bia Moja mbili Tatu alafu Mkeo na familia mwaka mzima umeifungia ndani hutaki kuitoa out. Huo ni USHENZI ambao hata Wanyama na mashetani wenyewe hawawezi kuufanya.
Mtoe Mkeo Out
Itoe Familia yako Out angalau kila baada ya miezi mitatu ikiwa uchumi wenu ni hafifu.
Lakini kama uchumi wenu ni mzuri mtoe Out Kila mwezi.
Kama unamuda zaidi mtoe kila baada ha wiki mbili.
Alafu Kule Out sio lazima muagize vitu vingi vya gharama. Ukiwa na elfu hamsini tuu kama unafamilia ya watu watano inatosha Kabisa.
Kama ni wewe na Mkeo. Wala sio gharama kubwa.
Kilo Moja ya nyama ya mbuzi ya kuchoma ni elfu 16-20. Agiza kilo Moja na nusu. Agiza na kinywaji kama ni mnywaji wa pombe pombe nyingi za kawaida bei yake ni 2000 Mpaka 5000 kama mpo wawili ni Chupa mbili tuu zinawatosha.
Pigeni Stori mfurahie.
Siku nyingine sio lazima muagize nyama. Mnaweza kuagiza tuu juisi hata ya miwa ambayo haizii elfu tano.
Nendeni Beach zipo za bure. Kama mnahitaji Faragha nendeni za kulipia.
Sio mambo mengine muishie kuyaona kwenye Filamu kama watoto. Ninyi tayari ni watu wazima.
Msisubiri muanze kuumwa na uzee uwakabili..
Mwaka 2025 uwe mwaka Mkubwa kwenu. Mwaka wa Familia. Mwaka wa kuifurahisha na kujifurahisha na familia yako.
Maisha ndio hayohayo. Hakuna maisha mengine.
Haiwezekani ufurahishe wanawake wengine huko alafu uache Mkeo aliyekuzalia watoto. Hiyo kama sio Laana ni nini? Huko kama sio kulogwa ni nini?
Haiwezekani ufurahie pesa zako na marafiki mkienda Bar alafu Mkeo na watoto ati wao hawataki hizo Raha. Huko kama sio kulogwa au Laana ni nini?
Angalia jamii zilizobarikiwa ukajifunze kwao.
Jamii zilizobarikiwa kama Watibeli, wazungu, Waarabu, Wairan, Wachina n.k.
Family First.
Yaani Jambo lolote la furaha Familia lizma ifurahie Kwanza ndipo wengine wafuate. Wengine ni ndugu, jamaa na marafiki.
Wazungu wanatoka na Familia Zao maelfu ya kilometres kuja Afrika, kwenda Duniani kujivinjari.
Wewe unashindwaje kutoka out hata mtaa mwingine na familia yako. Lakini wewe huyohuyo ndiye wakwanza kujifanya unalipia Mzunguko ya bia Bar uwapo na marafiki zako. Bado unajiona hujalogwa au hauna Laana?
Mwaka 2025 uwe mwaka wa kulinda kilichochako(familia yako) kuifurahisha familia yako.
Usipomtoa Mkeo na watoto Out Nani mwingine wakufanya hivyo? Embu Acha Ukengemaji.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam