Mwanaume hodari anajua kumdekeza mke/Mpenzi wake

Mwanaume hodari anajua kumdekeza mke/Mpenzi wake

View attachment 3646447

Nyumba sio kambi ya kijeshi wala sehemu ya kutoa amri. Ni mahali pa upendo, utulivu na furaha.

Mkeo au mpenzi wako ndiye mshirika wako wa maisha.

Baadhi ya wanaume hujifanya ni makamanda wa Jeshi nyumbani kwa kutoa amri za hapa na pale.

Mfano "Nipe maji ya kunywa"
"Niwekee maji ya kuoga"
"Njoo hapa"
"Nipe Mapenzi"
"Huendi"

Kumbuka kuwa huko nje unaweza kuwa bosi lakini nyumbani nyote ni familia Moja. Mwanamke anayehisi anathaminiwa ndiye atakayekupa amani ya akili na moyo.

Anapodekezwa mvuto wake unaongezeka. Anakuwa mtiifu zaidi, msikivu zaidi. Nyumba inajaa baraka, chakula kinakuwa kitamu, na matatizo yanapungua.

Kudekeza sio gharama ni uwekezaji.
View attachment 3646452

Usisubiri afanye kitu kikubwa ndio umpe sifa. Mshukuru hata kwa vitu vidogo. "Ninakushukuru" neno hili lina nguvu kuliko pesa nyingi.

#Mapenzi #Ndoa
Mungu tupe uvumilivu
 
Umenielewa tofauti jamani 😅😅😅
Ukimdekeza nawe utadekezwa 😜
VInginevyo itolewe na mazingira ya nyumbani ya mtoa mada zinazohusiana na mambo haya iliwalio mashimani watupe ukweli halisi kwani haya yatalisaidia taifa na watu wake.Ikiwa jamii fulani ni korofi jawapo iendane na jamii inayoendana ili mambo yasiwe mengi kiasi cha kusambaratisha familia.
 
VInginevyo itolewe na mazingira ya nyumbani ya mtoa mada zinazohusiana na mambo haya iliwalio mashimani watupe ukweli halisi kwani haya yatalisaidia yaifa na watu wake.Ikiwa jamii fulani ni korofi iwapo iendane na jamii inayoendana ili mambo yasiwe mengi kiasi cha kusambaratisha familia.
Kweli kabisa mambo yasiwe mengi sana 😅
 
Back
Top Bottom