Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Mwanausalama Tanzania aaibika kutumia nguvu na mwanausalama wa Obama kumlinda mwandishi

Idara ya usalama ilikufa siku nyingi zilizopita kwa kukosa ueledi kwa watendaji wake na kujipachika na kupeana nyadhifa mbalimbali. Naamini usalama wa viongozi wetu uko mikononi mwa muumba na sio mikononi mwa "makanjanja" wanaojiita usalama wa taifa tanzania. Pfuuuuuu kucha zanguuuuuuuuu
 
tanzania tunatumia nguvu nyingi kuliko akili tukidhani sifa kumbe ujinga

wanausalama wa wenzetu akili zao bado zipo kichwani,za wa kwetu zilihamia maeneo mengine ya mwili kutokana na vita ya msongo wa mawazo kichwani kukawa hakukaliki!
 
Hii sio aibu ya wanausalama Tanzania tu. Ni aibu ya watanzania wote kwa ujumla wakiwemo mimi na wewe. Polisi, JWTZ na taasisi zote za kiserikali nyeti ikiwemo Ikulu pamoja na Rais vinapaswa kuwa alama ya nchi na ni tafisri ya halisi ya taswira ya mwananchi wa kawaida wa Tanzania.

Kitendo cha mwanausalama huyo kumsukuma mwanamke tena mwandishi wa habari ni ishara tu ya utamaduni mbovu wa kimalezi unaonzia katika ngazi ya familia hadi kufika ngzi za juu kabisa za utawala wa kutumia nguvu bila akili:

Mtoto akikosea apigwe fimbo.
Mke akiharibu apigwe makofi.
Mwanafunzi akifeli achapwe viboko.
Polisi akiwa kazini apige raia.
Waziri mkuu Pinda akikasirika kidogo, liwalo na liwe.
Raisi wa nchi akishindwa kazi, anawakata mapembe wote wenye nayo.
CCM ikizidiwa inarusha mabomu na kusingizia kesi wapinzani.

Tumieni akili nyie watu wa serikali na watanzania. Mtashangaa hatua kubwa za kimaendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi nchi yenu, lol!
 
Wanausalama wanatengeneza bifu zisizokuwa na maana kwa wana habari kitu ambacho ni kibaya na kitasababisha matatizo mengi. Sijui kwa nini hawafuati maadili yao ya kazi.
 
Kuna watu wanahoji ukweli wa habari hii. Japo sikuwepo hapo naiamini 99% kwani nimeshuhudia pia Polisi wakiwafokea na kuwasukuma Watz wenzao na wamarekani wakawa wanawazuia na kuwaelekeza wananchi kistarabu mambo yanakwenda. Kiujumla askari wetu ni wakurupukaji ndiyo maana wanakimbilia mabomu na kuua hata sehemu isiyohatarishi.

Nina ushahidi pia kwa kijana aliyedakwa stand Ubungo jana akiwa amekwenda kumsindikiza mgeni. Pamoja na ndugu zake kupeleka vielelezo kadhaa wamegoma kumwachia hadi Ijumaa
 
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.

Ndiyo! Hata Waziri Mkuu katuambia tuwe tunatumia nguvu na kuwapiga...., Na mkuu wa nchi katoa amri ya KUWAKATA MAPEMBE
 
"...NO NO Sir! We are not TEACHED that way. You know, you know we are AMRIzed to KICK if they NOT HEAR, we KICK ONLY, because us TIRED NOW..."

ha ha ha ha ha very cocacolastic! you made me happy!!
 
Ili kuondoa tatizo hili la unyanyasaji toka kwa wanausalama wetu, Papaa Kikwete alitakiwa kuomba msaada wa mafunzo maalumu toka kwa Obama! Wanausalama wa Bongo wamefundishwa kuua. Huruma yao ya mwisho ni kung'oa macho,meno na kucha bila ganzi!
 
Hilo ni dongo kwa mkuu wa nchi.
linamhusu vipi? mkuu wa Nchi
naona hata wasiotaka kufanya kazi na kubakia ushabiki wa upinzani msipoenda choo mtadai ni Mkuu w nchi
 
bora mmarekan kauliza, tungeuliza sisi tungeambiwa n wapinga jk (endapo bomu lisingerushwa au kupigwa)
 
Huyo askari wetu alijibu nini baada ya kuulizwa kwa kimombo ikiwa hayo ndiyo wanayofundishwa katika utendaji wao?

Isije ikawa lugha ilikorofishwa akajibu yes Sir.
yaelekea alikaa kimya au hakuelewa jamaa anamaanisha nini?
 
Jasusi
Mbona haya ya kutumia nguvu huku USA yapo mengi sana unataka tukuwekee data za kiasi police department zinalipa watu kwa makosa ya kutumia nguvu na unyasaji? Mkuu angalia sana kuandika vitu kwa kudakia hao waandishi lugha mgogoro hapo palikosekana mkalimani!
Chama,
Tofauti ya hapa (Marekani) na nyumbani ni kwamba unaweza kumburura polisi aliyetumia nguvu mahakamani na kupata haki yako. Kwa Tanzania hiyo ni ndoto. Hapa polisi anapoua anapelekwa administrative leave immediately na upelelezi kufanyika. Nyumbani anapandishwa cheo. Sijadakia chochote.
 
Ndivyo mnavyofundishwa katika utendaji wenu? Haya ni maneno mazito sana kuhusu maafisa wa usalama wetu.

Fyooooooooooooooooo! aibu iliyoje maspy mengi ya bongo si ma-green guard ya ccm hivyo yamejaa ushabiki na hila wakati wenzao wanatumia weledi..............safi US spy
 
Angemjibu kuwa this is how we are instructed by our prime minister.

te te! umenipa raha sana nadhani unataka kunikumbusha kakibwagizo ka- "piga tu! nasema wapige tu! maana hakuna namna nyingine sisi tumechoka!"
 
haibu kubwa cana inaonesha ni kiaci gani viombo vyetu vya dola vya nchi yetu vinavyopenda kutumia mabavu kuliko akili na sheria zinavyocema lakini tucilaumu cana inawezakana ndio ata mafunzo yanayotolewa kwa hawa watu yana cicitiza matumizi ya nguvu kuliko akili. 😛ainkiller:

Ulipata division ngapi baada ya matokeo kurekebishwa??
 
Wanatimiza amri ya PM..... WAPIGENI tu. SUKUMA, Waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!

Pinda%201(3).jpg
 
Back
Top Bottom