Hii sio aibu ya wanausalama Tanzania tu. Ni aibu ya watanzania wote kwa ujumla wakiwemo mimi na wewe. Polisi, JWTZ na taasisi zote za kiserikali nyeti ikiwemo Ikulu pamoja na Rais vinapaswa kuwa alama ya nchi na ni tafisri ya halisi ya taswira ya mwananchi wa kawaida wa Tanzania.
Kitendo cha mwanausalama huyo kumsukuma mwanamke tena mwandishi wa habari ni ishara tu ya utamaduni mbovu wa kimalezi unaonzia katika ngazi ya familia hadi kufika ngzi za juu kabisa za utawala wa kutumia nguvu bila akili:
Mtoto akikosea apigwe fimbo.
Mke akiharibu apigwe makofi.
Mwanafunzi akifeli achapwe viboko.
Polisi akiwa kazini apige raia.
Waziri mkuu Pinda akikasirika kidogo, liwalo na liwe.
Raisi wa nchi akishindwa kazi, anawakata mapembe wote wenye nayo.
CCM ikizidiwa inarusha mabomu na kusingizia kesi wapinzani.
Tumieni akili nyie watu wa serikali na watanzania. Mtashangaa hatua kubwa za kimaendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi nchi yenu, lol!