Nimekuuliza jina la huyo mtu unayesema aliletwa toka Swaziland. Andika ni nani? Acha hadithi za kutunga. Kama unatamani kwenda Ulaya na njia imekushinda, tangaza una maisha magumu. Acha ulongo eti natafutwa na wasiojulikana. Kuandika kwenye gazeti makara moja tena haina la maana ndo atafutwe.
Narudia tena nani alitetwa na serikali toka Swaziland. Kama huna jina acha kulopoka hadithi.
ko unataka kunambia ni heri kufa kuliko kukimbilia kwa wazungu???!!!
sijui umesoma chuo gani??!!!
Hiyo jamani,mkuu wewe ni ME au KE
Nimekuuliza jina la huyo mtu unayesema aliletwa toka Swaziland. Andika ni nani? Acha hadithi za kutunga. Kama unatamani kwenda Ulaya na njia imekushinda, tangaza una maisha magumu. Acha ulongo eti natafutwa na wasiojulikana. Kuandika kwenye gazeti makara moja tena haina la maana ndo atafutwe.
Narudia tena nani alitetwa na serikali toka Swaziland. Kama huna jina acha kulopoka hadithi.
Njaa bhana.
aaaaah Gavana Mkuuu!! labda ulitaka kumquote [HASHTAG]#Patriot[/HASHTAG] maana hajaelewa kwa nn mwandishi Ngurumo kajificha FINLAND na sio nearby shit hole country!!!!Watu kwa kumsema Papa Doc. vibaya tu wamefunguliwa makesi
Nitafeli mapema kwani kuna kijana alipotea miezi 6 alipoonekana kumbe alikuwa ndani , kosa lake kaenda kuposa mke kwa mtu aliyebambikiziwa kesi ya ugaidi.
Walimwachia siku mbili baadaye kwa kueleza hii habari wamemtia adabu kwa kumfunga tena mpaka leo. Kijana hajui hata siasa ilivyokaa.
Wachilia mbali kesi za wale masheikh walioukosoa muungano kwa kutumia haki yao kikatiba na kubambikiziwa kesi za kigaidi zisizo mashiko
Ofcourse kwa kurushiwa buku saba utakuja kutapika pumba hapa, kwani hujali hayajakufika wala hakuna jamaa yako yamemfika
Angeuwawa ndio ungeamini kuwa alikuwa anawindwa. Hivi ni mpaka watu wangapi wauwawe au wapotezwe ndio muuelewe ukweli. Muwe na huruma na imani,kwa vile we kila usiku upo kitandani na mwenza wako basi unadhihaki wenzio wenye maisha yaliyo hatarini. Amini nakuambia ipo siku yatakukumba, usifurahie tu yakiwa kwa mwingine. Hawa waliopotezwa na kuuawa wangekuwa jamaa zako wa karibu ungedhihaki ? Au ingekuwa ni mwenza mnaechangia kitanda ungefurahia ?Kuwa mkimbizi mnaipigia filimbi kama vile ni wa kwanza duniani.. eeeeeh
Uamuzi wake huo.. alitaka tu kwenda ulaya kuishi huko baada ya kuwa mvivu kufanya kazi kujilisha
Umesema kweli, hata Ndugai alijiuguza tu makusudi ili akatembee India.Kuwa mkimbizi mnaipigia filimbi kama vile ni wa kwanza duniani.. eeeeeh
Uamuzi wake huo.. alitaka tu kwenda ulaya kuishi huko baada ya kuwa mvivu kufanya kazi kujilisha
Huwa inaletwa na uvivu wa fikra.Imeletwa na nani??
Mauzo ya London Stock Exchange mwaka jana ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka ishiriniWazungu wanaihitaji Tanzania zaidi ya Tanzania tunavyo wahitaji hao wazungu.
mi tangu nipo Mdogo nilifundishwa na mzee wangu Uhuru bila mipaka ni fujo,na sasa nakumbushwa kitu kitu kimoja "ukiona mtu alikuwa anapinga serikali ya jk na ya magufuli pia anapinga" mwangalie vizuri ni kuwa hayupo kwenye maslahi ya taifaNi habari mbaya kwa nchi yetu inaendelea kuwa na hadhi mbaya ndani /nje ya mipaka yake. Maisha ya waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati yamekuwa ya mashaka.
Mwanahabari Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi huko, kwa muda alikuwa akisema anatishiwa kuuawa.
Habari zaidi soma=> Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo
UPDATE:
Mwandishi wa Habari mwandamizi nchini, Ansbert Ngurumo amepata hadhi ya kupewa ulinzi nchini Finland, baada ya kudai amekimbia aliowaita "wauaji" wake.
Ngurumo ambaye amewahi kuwa mhariri wa magazeti kadhaa nchini; Mtanzania, Tanzania Daima na MwanaHalisi, ameiambia JamiiForums kuwa amekiepuka kifo kilichopangwa na wale aliowaita "wasiojulikana."
Akizungumza na JamiiForums, Ngurumo alisema ni kweli amekimbia Tanzania ili kuulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.
"Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai," anasema Ngurumo.
Anasema ili kunusuru uhai wake, alilazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kupata kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako amepewa hifadhi.
Ngurumo anasema hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni "hifadhi ya kimataifa," kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.
Vyombo vya Habari vya Finland na mitandao ya kijamii, imeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.
"Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa," anaongeza Ngurumo.
JamiiForums inatambua kuwa Ngurumo alianza kuhofia maisha yake baada ya kudai kupokea vitisho kwa alichodai ni kufuatia kuandika makala kwenye gazeti la MwanaHalisi ikiwa na kichwa cha habari; “Tumuombee Rais Magufuli au Tundu Lissu?”
Mipaka ni ile iliyopo kwenye sheria na katiba sio matamko ya watu tu kila kukicha kutokana na uroho wa madaraka na hulka zao.mi tangu nipo Mdogo nilifundishwa na mzee wangu Uhuru bila mipaka ni fujo,na sasa nakumbushwa kitu kitu kimoja "ukiona mtu alikuwa anapinga serikali ya jk na ya magufuli pia anapinga" mwangalie vizuri ni kuwa hayupo kwenye maslahi ya taifa