Mwandishi mkongwe Abdallah Majura, ahoji kuhusu redio kujadili michezo asubuhi

Mwandishi mkongwe Abdallah Majura, ahoji kuhusu redio kujadili michezo asubuhi

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
 
Akili za vijana zinatakiwa kufanyiwa rehabilitation juu ya hii michezo 24hrs.
 
Kipindi cha miaka ya nyuma, watu walikuwa wanatenga muda kabisa wa kusikiliza redio,.

Imebakia uchambuzi uchwara wa mpira, kusomewa magazeti na uchawa mwingi

Pamoja na kujisifu maisha binafsi ya huko majumbani mwao, mfano; nanyumba kali, gari Kali, watt wangu wanasoma shule EM, mke wangu mzuri duniani 😂😂 n.k
 
Mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Abdallah Majura amehoji kuhusu radio kuwa na vipindi vya michezo asubuhi na kujadili mambo ya Simba na Yanga.

“Tangu asubuhi watu wanatangaza michezo tu, lakini siamini kwamba Watanzania wote wanapenda michezo tu”

Nafikiri Majura atakuwa anawalenga, Crown FM, Wasafi FM, Clouds Fm na Efm
Hoja yake ina mashiko lkn hawezi sikilizwa.
 
Asubuhi mtu anaanza kusikiliza michezo ukianza na Wasafi, Crown, Clouds, EA Radio, Bongo FM, EFM vipindi vinaisha saa 6 mchana. Halafu hao EFM wanahamia kwenye TV yao sijui kuna yule Dada anaitwa Maongezi kipindi hadi saa 9 mchana. Then kuanzia saa 8 mchana zinaanza mechi za ligi kuu hadi 3 usiku. Baadae unakutana na ligi za Ulaya, EPL, La Liga, UCL, sijui Europa... aiseeh hili taifa sijui kama tutapata maendeleo maana vijana wengi wameangukia huko afu hapo jumlisha na kubeti sasa, bado hawajaanza kubishana kwenye vijiwe na mitandaoni, bado hawajacomment kwenye page za CAF hahahaaaa 😀 😀 😀, hatutoboi!!
 
Wale wanafanya biashara siku wakiona Habari za Siasa ndio zina wasikilizaji wengi Radio zitahamia huko.
Kinachoangaliwa ni Wapi pana walaj wengi na sio weledi wa kazi.
Nchi haina viongozi wenye maono. Wanadhani ni wajanja kumbe ndivyo wanavyozidi kudidimiza vijana wa nchi hii. Michezo inatumika kama magc ya kupumbaza watu wasikumbuke mambo mengine.
 
Back
Top Bottom