Asubuhi mtu anaanza kusikiliza michezo ukianza na Wasafi, Crown, Clouds, EA Radio, Bongo FM, EFM vipindi vinaisha saa 6 mchana. Halafu hao EFM wanahamia kwenye TV yao sijui kuna yule Dada anaitwa Maongezi kipindi hadi saa 9 mchana. Then kuanzia saa 8 mchana zinaanza mechi za ligi kuu hadi 3 usiku. Baadae unakutana na ligi za Ulaya, EPL, La Liga, UCL, sijui Europa... aiseeh hili taifa sijui kama tutapata maendeleo maana vijana wengi wameangukia huko afu hapo jumlisha na kubeti sasa, bado hawajaanza kubishana kwenye vijiwe na mitandaoni, bado hawajacomment kwenye page za CAF hahahaaaa 😀 😀 😀, hatutoboi!!