Mwandishi wa Habari Luqman Maloto afungua kesi dhidi ya DCI na DPP kisa Tundu Lissu, Azory Gwanda na Ben Saanane

Hiyo kesi mahakama zitaipokea?
Kila mtanzania anajua hatuna mahakama,Mana zinafanya kazi kwa kusikia Rais anasemaje. It means tunapoona bado mahakama zinaogopa kufanya majukumu yake maana yake bado na Rais Samia anabaliki mfumo wa kidikiteta na anautegemea hapendi kuona haki ikitamalaki katika vyombo vya Haki,,
 
Serikali kama kawaida yake itaweka pingamizi na kesi kutupiliwa mbali!
 
Ingekuwa ni kikulacho muda tu wangeshakamatwa. Kama wamebambikiwa hadi kesi, ingekuwa wamefanya hayo si ingekuwa rahisi zaidi kwa hao wabambikiwa kesi.
Usijibizaje majinga utadhani hayajapita shule,yaani utawala wa CCM ulivyohatari zaidi ya shetani wawe na taarifa za kudhuliwa na mwenzao ndani ya chama nafikiri ndo wangeonesha dunia wanavyojua kushugulika na waharifu,,
 
Sawa kinachotakiwa ni haki iwe ndani ya chama au nje ya chama lakini tujue nani hasa alihusika,kama ni yule wa kuzimu tukafukue kaburi lake tuchape viboko mifupa yake au kuichoma moto.
Kabisa,taifa hili limeharibu kizazi Cha vijana hasa kwa kuwa taifa la hovyo,watu wanatenda mauaji mchana saa saba dodoma penye ulinzi mkali na bunge linaendelea yaani eti gari la wauwaji lipite barabara zote zenye matrafiki na litokomee,hivi wanajiona kujimilikisha hati miliki ya kuishi,,
 
Hii nchi aisee

Wakati Kubenea anafungua kesi ya jinai, dhidi ya Makonda na sijui na akina nani wengine. Kuna watu walitahadirisha kesi za jinai ni jamuhuri pekee inaweza fungua sio raia.

Mahakama zetu kwa kupenda mzaha na kuweka siasa mbele zikaona isikilizwe au ipate airtime wakidhani wanamtisha mtu.

Huku sasa ndio kufunguliwa kwenyewe kwa ‘Pandora Box’ sasa kila mtu anadhani anaweza fungua kesI za jinai mahakamani; yote haya chanzo chake ni mzaha wa mahakama.
 
Vipi Mwangosi, profesa Jwan, Dr Ulimboka au hao siyo binadamu?

Na vipi wengine siyo public figure wamepotea au na wenyewe sio binadamu?

Kuwa biased ndio tunaimaliza hii nchi?
Kwahiyo unailaumu serikali au hao raia wa kawaida wanaojitolea kuhakikisha haki inatendeka ktk vyombo vya kusimamia haki,Kuwa na Akili acha mawazo ya kishirikina
 
Yes, huu ndiyo ujasiri unaotakiwa katika mapambano ya kupigana na utawala wa kiovu na kidikteta..

Mapigano yanapaswa kupiganwa kotekote; ardhini, angani na majini...

Kwa maana kortini, kupitia social medias, main stream medias (tv, redio, na magazeti), kwenye mikutano ya hadhara tunapokutana na wananchi nk nk...

Go.....go....go...goooo... Lukuman Moloto. Tunakuunga mkono....

We know it's not easy but the WIN IS A MUST objective..!!
 
Ngoja tuone
 
Mbinu zote za kimedani.
 
Dpp ataifuta kesi kwa kusema haoni nia ya kuendelea na hii kesi.
 
haki za binadamu zanatolrwa kwa binamu ni haki kwakuwa cc ni binadamu
 
conformation ben aliuwawa na magufuli mwenyewe ikulu
 

Upande Jamhuri hususan wa mawakili wasomi wa serikali ofisi ya DPP / NPS wapikwe vizuri kitaaluma ili kulisaidia jeshi la Polisi ili haki iweze kupatikana inapostahiki.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA​


Mkurugenzi wa Mashtaka​

MKURUGENZI WA MASHTAKA
Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.


Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:
  • (i)Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
  • (ii)Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
  • (iii)Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
  • (iv)Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
  • (v)Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
  • (vi)Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenyetija katika mashtaka ya jinai;
  • (vii)Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
  • (viii)Kuteua na kutenguamamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
  • (ix)Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masualaya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
  • (x)Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
  • (xi)Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
  • (xii)Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiii)Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiv)Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
  • (xv)Kuandaa na kuwasilishakwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
  • (xvi)Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka
Source: https://www.nps.go.tz/pages/director-of-public-prosecutions
 
HAKUNA CASE HAPO ITATUPILIWA MBALI..... MLOTO HANA MAMLAKA YA KUFUNGUA CASE YA JINAI......... WASTAGE OF TIME.........
 
Mtafute Zitto akupeleke Mwisho wa Reli.
 
ngoja ajaribu lakini kwa mahakama zipi? Za huyu Juma? kwa Jaji yupi? hawa wa sasa?
 
Mbona ni jambo la kawaida, hata serikali inshtakiwa kama jamhuri au ndugu yangu wewe bado uko enzi za zamani sana?
Rasta mbona wewe haujafungua kama ni kawaida? Au na wewe ni shujaa wa kwenye keyboard na anonymous ID?
 
Kimataifa tutaonekana vipi ikiwa kesi hii itafanyiwa mzaha kwa kutumia mbinu chafu

TUANGAZIE OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA WA KIMATAIFA ILIYOPO THE HAGUE NETHERLANDS -

Ofisi ya Mwendesha mashtaka ni moja wa sehemu nne za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Inaongozwa na Mwendesha mashtaka, Luis Moreno-
Ocampo, aliyechaguliwa na Baraza la nchi zinazounda Mahakama, na ana uwezo wote wa menejimenti na uendeshaji wa Ofisi hii, ikiwemo uongozi wa wafanyakazi, wa vifaa na rasilimali nyingine. Mwendesha mashtaka, alichukua madaraka tarehe 16 Juni 2003.

Ofisi ina kazi ya kupokea na kuchambua taarifa za hali
zilizowasilishwa (referrals) na habari ili kuazimu kama kuna msingi elekevu kwa kuanza uchunguzi, kuendesha
uchunguzi katika mauaji ya halaiki, makosa ya jinai dhidi ya
ubinadamu na makosa ya jinai ya vitani na kuwapeleka mbele ya Mahakama walio na jukumu ya makosa hayo ya jinai.

Inapo endesha uchunguzi na mashtaka, Ofisi ya Mwendesha mashtaka inaleta mchango wake kwa kulifikia lengo la jumla la Mahakama, ambalo ni kusaidia kukomesha hali yakutoadhibiwa kwa watendaji wa makosa ya jinai mazito sana yenyi kuathiri jumuiya ya kimataifa kwa jumla, na kusaidia hivi katika juhudi za kuepuka makosa hayo ya jinai.

Kutokana na jukumu lake, Ofisi ya Mwendesha mashtaka inaundwa na idara tatu :

Idara ya uchunguzi ina kazi ya kuongoza uchunguzi (kwa mfano kukusanya na kuchambua ushuhuda, kuhoji wanao husika na uchunguzi na pia wateswa na mashahidi). Kwa hiyo, na kusudi ya kuonesha ukweli, Mkataba walazimisha Ofisi ya Mwendesha mashtaka kufanya uchunguzi unaozingatia mambo yanayo thibithisha mashtaka na yale yanayo kanusha mashtaka.

Idara ya mashtaka, inakazi katika utaratibu wa uchunguzi, na itakuwa pia na wajibu muhimu wa taratibu za kesi mbele ya Vyumba mbalimbali vya Mahakama.

Idara ya mamlaka, kukamilishana na ya uhusiano yafanya uchambuzi wa taarifa za hali zilizo wasilishwa (referrals) na wa habari, ikipewa msaada kutoka Idara ya mashtaka, yatathmini hali ya kukubaliwa kwa mashtaka na yasaidia kuweka ushirikiano unaohitajika katika kazi za Ofisi.

Mwendesha mashtaka aweza kuanzisha uchunguzi kutokana na hali ambayo imewasilishwa kwake na moja wa nchi zinazounda Mahakama wala na Baraza la Usalama likizingatia hatari ambayo ni tishio dhidi ya amani na usalama wa kimataifa.

Kwa nyongeza, Mwendesha mashtaka anaweza, kwa hiari yake mwenyewe, kuanza uchunguzi katika eneo wala dhidi ya raia wa moja wa nchi
zinazounda Mahakama ambao utahakishwa na Chumba cha utangulizi cha Mahakama.

Ni mbinu ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka kuelekeza uchunguzi wake dhidi ya watu wowote wenyi dhima kubwa ya makosa ya jinai yaliyotendeka katika hali ambayo inachunguzwa.

Utangulizi wa Mkataba wa Roma watambua kwamba Mahakama yenyewe ni nafasi ya mwisho kwa kuwapa haki wateswa wa mauaji ya halaiki,
wa makosa ya jinai ya vitani na wa makosa ya jinai dhidi ya ubinadamu. Kwa hiyo Mkataba wa Roma unapatia Mahakama na Ofisi ya Mwendesha mashtaka kazi ambayo inakamilishana na mifumo ya sheria ya taifa.

Mkataba wa Roma wasema tena kwamba Ofisi ya Mwendesha mashtaka ni huru katika kazi zake. Kutokana na hiyo, mfanyakazi wake hawezi kuomba ao kutumika
kulingana na maagizo kutoka nje kama vile kwa nchi, kwa mashirika ya kimataifa, kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ao kwa watu binafsi.

WASIFU WA WAENDESHA MASHITAKA WAKUU

Luis Moreno-Ocampo
, Mwendesha mashtaka: Tarehe 21 Aprili 2003, Baraza la nchi
zinazounda Mahakama lilimchagua bwana Luis Moreno-Ocampo kutoka Ajentina kama
Mwendesha mashtaka wa kwanza wa Mahakama hii.

Ana ujuzi wenye sifa katika shughuli zake za mwendesha mashtaka, za mwakilishi, za mwalimu wa chuo kikuu na wakupanga hila za kisheria kuhusu maswala ya sheria ya kimataifa ya makosa ya jinai, za sheria ya haki za binadamu, za udhibiti wa rushwa na za utetezi wa waandishi wa habari.

Mwaka 1984, aliongoza uchunguzi katika kesi dhidi ya makamanda wakuu kenda wa jeshi, ikiwemo maraïs watatu wa zamani, baadhi ya viongozi wa kijeshi walioongoza Ajentina tangu mwaka 1976 hadi 1980.

Kesi iliyofuata, ambamo tano kati ya washtakiwa walihukumiwa, ndio ilikuwa ya kwanza dhidi ya watu wanaoshutumiwa kwa mauaji ya wengi tangu kesi ya Nuremberg ya maafisa wa nazi.

Katika taratibu za kesi hii, bwana Moreno-Ocampo alitoa hoja kuhusu mashtaka 700 ya "mauaji, utekaji nyara na mateso", aliita mashahidi 835 na kunukuu maelfu ya hati. Baada ya hayo, alifungua mashtaka dhidi ya wale waliohusika katika mauaji ya wengi wakati wa uasi wa kijeshi wa miaka 1987 na
1992 nchini Ajentina.

Miaka kumi baada ya kesi ya wanajeshi 'Junta Trials', bwana Moreno-Ocampo alijishughulika na kesi za hali ya juu katika sheria ya kimataifa ya makosa ya jinai, ikiwemo kurejesha kwa nguvu kwa afisa wa zamani
wa Nazi Erich Priebke nchini Italia; kesi ya polisi ya siri ya Chile kuhusu mauaji ya jemadari Carlos Prats na kesi dhidi
ya makamanda walioshutumiwa mwenendo mbaya kazini wakati wa vita vya Malvinas/Falklands. Bwana Moreno-Ocampo alikuwa mwanamemba wa halmashauri kuu ya uongozi ya Transparency International, na profesa wa kuzuru katika vyuo vikuu vya Stanford na Harvard.


Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka makamu (mashtaka): Tarehe 8 Septemba 2004,
bibi Bensouda kutoka Gambia alichaguliwa kama mwendesha mashtaka makamu na Baraza la nchizinazounda Mahakama.

Yeye ni mkuu wa Idara ya mashtaka katika Ofisi ya Mwendesha mashtaka.
Kabla ya kuchaguliwa kwake, bibi Bensouda alifanya kazi kama mshauri wa kisheria na kama mwakilishi kwenyi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) mjini Arusha nchini Tanzania, akapandishwa cheo hadi kuwa mshauri mkuu wa kisheria na mkuu wa Kitengo cha ushauri wa kisheria. Kabla ya kufanya kazi katika Mahakama ya Kimataifa ya jinai ya Rwanda, alikuwa meneja mkuu wa benki moja ya biashara nchini Gambia.

Kati ya miaka 1987 na 2000,
alikuwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (Senior State Counsel), mwendesha mashtaka wa serikali (Principal State Counsel), mkurugenzi makamu wa mashtaka, msaidizi wa mwendesha mashtaka (Solicitor General), katibu wa kisheria wa Jamhuri (Legal Secretary of the Republic), halafu mwendesha mashtaka mkuu (Attorney General) na waziri wa sheria, wakati ambapo alihudumu pia kama mshauri mkuu wa kisheria wa Raïs na wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Gambia.

Bibi Bensouda alishiriki pia kwenyi majadiliano kuhusu Mkataba wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya magharibi (ECOWAS), Bunge la Afrika ya magharibi, na Mahakama ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya magharibi.

Alikuwa pia mjumbe katika mikutano ya Umoja wa Mataifa ili kuzuia uhalifu, katika mikutano ya mawaziri wa Shirika la Umoja wa Afrika kuhusu haki za binadamu, na mjumbe wa Gambia kwenye mikutano ya
Komisheni ya matayarisho ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Bibi Bensouda ana digrii ya shahada ya pili (masters
degree) katika sheria ya kimataifa ya bahari na sheria ya uziwa, na kwa hiyo yeye ndiye mstadi wa kwanza wa sheria ya
kimataifa ya bahari nchini Gambia.

Tawi la huduma Utawala wa jumla
Kitengo cha huduma za lugha
Kitengo cha msingi wa ujuzi
Kitengo cha habari na ushuhuda
Idara ya mamlaka, kukamilishana na ya ushirikiano
Tawi la maoni ya kisheria
Idara ya mashtaka
Tawi la mashtaka
Tawi la rufaa
Ofisi ndogo ya Mwendesha mashtaka
Idara ya uchunguzi
Timu ya wachunguzi 1
Timu ya wachunguzi 3
Timu ya wachunguzi 2
Tawi la mpango wa
uchunguzi na msaada
Kitengo cha msaada kwa harakati
Kitengo cha jinsia na watoto
Kitengo cha mbinu na uchambuzi
kuhusu uchunguzi (Makao makuu)
Tawi la uchambuzi wa hali
Tawi la ushirikiano wa
kimataifa
Source : www.icc-cpi.int | Hii haiko dokima ya serkali. Niya yake ni kupana tu habari ku batu bote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…