Kimataifa tutaonekana vipi ikiwa kesi hii itafanyiwa mzaha kwa kutumia mbinu chafu
TUANGAZIE OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA WA KIMATAIFA ILIYOPO THE HAGUE NETHERLANDS -
Ofisi ya Mwendesha mashtaka ni moja wa sehemu nne za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Inaongozwa na Mwendesha mashtaka, Luis Moreno-
Ocampo, aliyechaguliwa na Baraza la nchi zinazounda Mahakama, na ana uwezo wote wa menejimenti na uendeshaji wa Ofisi hii, ikiwemo uongozi wa wafanyakazi, wa vifaa na rasilimali nyingine. Mwendesha mashtaka, alichukua madaraka tarehe 16 Juni 2003.
Ofisi ina kazi ya kupokea na kuchambua taarifa za hali
zilizowasilishwa (referrals) na habari ili kuazimu kama kuna msingi elekevu kwa kuanza uchunguzi, kuendesha
uchunguzi katika mauaji ya halaiki, makosa ya jinai dhidi ya
ubinadamu na makosa ya jinai ya vitani na kuwapeleka mbele ya Mahakama walio na jukumu ya makosa hayo ya jinai.
Inapo endesha uchunguzi na mashtaka, Ofisi ya Mwendesha mashtaka inaleta mchango wake kwa kulifikia lengo la jumla la Mahakama, ambalo ni kusaidia kukomesha hali yakutoadhibiwa kwa watendaji wa makosa ya jinai mazito sana yenyi kuathiri jumuiya ya kimataifa kwa jumla, na kusaidia hivi katika juhudi za kuepuka makosa hayo ya jinai.
Kutokana na jukumu lake, Ofisi ya Mwendesha mashtaka inaundwa na idara tatu :
•
Idara ya uchunguzi ina kazi ya kuongoza uchunguzi (kwa mfano kukusanya na kuchambua ushuhuda, kuhoji wanao husika na uchunguzi na pia wateswa na mashahidi). Kwa hiyo, na kusudi ya kuonesha ukweli, Mkataba walazimisha Ofisi ya Mwendesha mashtaka kufanya uchunguzi unaozingatia mambo yanayo thibithisha mashtaka na yale yanayo kanusha mashtaka.
•
Idara ya mashtaka, inakazi katika utaratibu wa uchunguzi, na itakuwa pia na wajibu muhimu wa taratibu za kesi mbele ya Vyumba mbalimbali vya Mahakama.
•
Idara ya mamlaka, kukamilishana na ya uhusiano yafanya uchambuzi wa taarifa za hali zilizo wasilishwa (referrals) na wa habari, ikipewa msaada kutoka Idara ya mashtaka, yatathmini hali ya kukubaliwa kwa mashtaka na yasaidia kuweka ushirikiano unaohitajika katika kazi za Ofisi.
Mwendesha mashtaka aweza kuanzisha uchunguzi kutokana na hali ambayo imewasilishwa kwake na moja wa nchi zinazounda Mahakama wala na Baraza la Usalama likizingatia hatari ambayo ni tishio dhidi ya amani na usalama wa kimataifa.
Kwa nyongeza, Mwendesha mashtaka anaweza, kwa hiari yake mwenyewe, kuanza uchunguzi katika eneo wala dhidi ya raia wa moja wa nchi
zinazounda Mahakama ambao utahakishwa na Chumba cha utangulizi cha Mahakama.
Ni mbinu ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka kuelekeza uchunguzi wake dhidi ya watu wowote wenyi dhima kubwa ya makosa ya jinai yaliyotendeka katika hali ambayo inachunguzwa.
Utangulizi wa
Mkataba wa Roma watambua kwamba Mahakama yenyewe ni nafasi ya mwisho kwa kuwapa haki wateswa wa mauaji ya halaiki,
wa makosa ya jinai ya vitani na wa makosa ya jinai dhidi ya ubinadamu. Kwa hiyo Mkataba wa Roma unapatia Mahakama na Ofisi ya Mwendesha mashtaka kazi ambayo inakamilishana na mifumo ya sheria ya taifa.
Mkataba wa Roma wasema tena kwamba Ofisi ya Mwendesha mashtaka ni huru katika kazi zake. Kutokana na hiyo, mfanyakazi wake hawezi kuomba ao kutumika
kulingana na maagizo kutoka nje kama vile kwa nchi, kwa mashirika ya kimataifa, kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ao kwa watu binafsi.
WASIFU WA WAENDESHA MASHITAKA WAKUU
Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha mashtaka: Tarehe 21 Aprili 2003, Baraza la nchi
zinazounda Mahakama lilimchagua bwana Luis Moreno-Ocampo kutoka Ajentina kama
Mwendesha mashtaka wa kwanza wa Mahakama hii.
Ana ujuzi wenye sifa katika shughuli zake za mwendesha mashtaka, za mwakilishi, za mwalimu wa chuo kikuu na wakupanga hila za kisheria kuhusu maswala ya sheria ya kimataifa ya makosa ya jinai, za sheria ya haki za binadamu, za udhibiti wa rushwa na za utetezi wa waandishi wa habari.
Mwaka 1984, aliongoza uchunguzi katika kesi dhidi ya makamanda wakuu kenda wa jeshi, ikiwemo maraïs watatu wa zamani, baadhi ya viongozi wa kijeshi walioongoza Ajentina tangu mwaka 1976 hadi 1980.
Kesi iliyofuata, ambamo tano kati ya washtakiwa walihukumiwa, ndio ilikuwa ya kwanza dhidi ya watu wanaoshutumiwa kwa mauaji ya wengi tangu kesi ya Nuremberg ya maafisa wa nazi.
Katika taratibu za kesi hii, bwana Moreno-Ocampo alitoa hoja kuhusu mashtaka 700 ya "mauaji, utekaji nyara na mateso", aliita mashahidi 835 na kunukuu maelfu ya hati. Baada ya hayo, alifungua mashtaka dhidi ya wale waliohusika katika mauaji ya wengi wakati wa uasi wa kijeshi wa miaka 1987 na
1992 nchini Ajentina.
Miaka kumi baada ya kesi ya wanajeshi 'Junta Trials', bwana Moreno-Ocampo alijishughulika na kesi za hali ya juu katika sheria ya kimataifa ya makosa ya jinai, ikiwemo kurejesha kwa nguvu kwa afisa wa zamani
wa Nazi Erich Priebke nchini Italia; kesi ya polisi ya siri ya Chile kuhusu mauaji ya jemadari Carlos Prats na kesi dhidi
ya makamanda walioshutumiwa mwenendo mbaya kazini wakati wa vita vya Malvinas/Falklands. Bwana Moreno-Ocampo alikuwa mwanamemba wa halmashauri kuu ya uongozi ya Transparency International, na profesa wa kuzuru katika vyuo vikuu vya Stanford na Harvard.
Fatou Bensouda, mwendesha mashtaka makamu (mashtaka): Tarehe 8 Septemba 2004,
bibi Bensouda kutoka Gambia alichaguliwa kama mwendesha mashtaka makamu na Baraza la nchizinazounda Mahakama.
Yeye ni mkuu wa Idara ya mashtaka katika Ofisi ya Mwendesha mashtaka.
Kabla ya kuchaguliwa kwake, bibi Bensouda alifanya kazi kama mshauri wa kisheria na kama mwakilishi kwenyi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) mjini Arusha nchini Tanzania, akapandishwa cheo hadi kuwa mshauri mkuu wa kisheria na mkuu wa Kitengo cha ushauri wa kisheria. Kabla ya kufanya kazi katika Mahakama ya Kimataifa ya jinai ya Rwanda, alikuwa meneja mkuu wa benki moja ya biashara nchini Gambia.
Kati ya miaka 1987 na 2000,
alikuwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (Senior State Counsel), mwendesha mashtaka wa serikali (Principal State Counsel), mkurugenzi makamu wa mashtaka, msaidizi wa mwendesha mashtaka (Solicitor General), katibu wa kisheria wa Jamhuri (Legal Secretary of the Republic), halafu mwendesha mashtaka mkuu (Attorney General) na waziri wa sheria, wakati ambapo alihudumu pia kama mshauri mkuu wa kisheria wa Raïs na wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Gambia.
Bibi Bensouda alishiriki pia kwenyi majadiliano kuhusu Mkataba wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya magharibi (ECOWAS), Bunge la Afrika ya magharibi, na Mahakama ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya magharibi.
Alikuwa pia mjumbe katika mikutano ya Umoja wa Mataifa ili kuzuia uhalifu, katika mikutano ya mawaziri wa Shirika la Umoja wa Afrika kuhusu haki za binadamu, na mjumbe wa Gambia kwenye mikutano ya
Komisheni ya matayarisho ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Bibi Bensouda ana digrii ya shahada ya pili (masters
degree) katika sheria ya kimataifa ya bahari na sheria ya uziwa, na kwa hiyo yeye ndiye mstadi wa kwanza wa sheria ya
kimataifa ya bahari nchini Gambia.
Tawi la huduma Utawala wa jumla
Kitengo cha huduma za lugha
Kitengo cha msingi wa ujuzi
Kitengo cha habari na ushuhuda
Idara ya mamlaka, kukamilishana na ya ushirikiano
Tawi la maoni ya kisheria
Idara ya mashtaka
Tawi la mashtaka
Tawi la rufaa
Ofisi ndogo ya Mwendesha mashtaka
Idara ya uchunguzi
Timu ya wachunguzi 1
Timu ya wachunguzi 3
Timu ya wachunguzi 2
Tawi la mpango wa
uchunguzi na msaada
Kitengo cha msaada kwa harakati
Kitengo cha jinsia na watoto
Kitengo cha mbinu na uchambuzi
kuhusu uchunguzi (Makao makuu)
Tawi la uchambuzi wa hali
Tawi la ushirikiano wa
kimataifa
Source :
www.icc-cpi.int | Hii haiko dokima ya serkali. Niya yake ni kupana tu habari ku batu bote.