Pole zote ziwaendee familia za mpoteaji pia kwa waandishi wote wa habari, ila kuna haja ya waandishi wa habari nchini kuwa na msimamo wa kukemea masuala ya kinyama kwa pamoja maana wakiachiwa Mtu mmoja mmoja madhara yake ni haya ya kutekwa na mafedhuli na kudanganyana eti wasiojulikana, mtoa taarifa za kubomoka kwa ukuta wa hostel apatikane lakini watekaji na wauaji wasipatikane wala kujulikana, kweli? Nchi hii tunakwenda wapi kufanya nini kwa matarajio gani? Kwanini isifikie mahali viongozi na waratibu matukio ya kinyama wasitambue wamepitwa na wakati? Inaumiza sana kuona nchi inayo nadiwa kuwa na amani kuwa na matukio ya makusudi kama haya halafu yeyote anaekaribia kutambua siri hizi za kiharamia anakuwa adui wa serikali kweli tuna nia ya dhati kujenga nchi au tunazugana ili wapige zao wasepe?