Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea. Ni siku 10 na hajulikani alipo

Sasa nimeanza kuelewa zile maiti zinazookotwa kwenye viroba kule ufukweni hua zinatoka wapi.
 
Huyo mwandishi wa habari ana kazi gani Kibiti? Kwa maelezo ya mkewe amekuwa anachukuliwa na 'watu' huko Kibiti, sasa swali alikuwa anachukuliwa na nani na alikuwa anapelekwa wapi na kwa kazi gani? KIBITI?

Gazeti la Mwananchi nalo lilikuwa na kazi gani KIBITI?
Yule si ni mwandishi wa kujitegemea au sijasoma vizuri?
 
Pole zote ziwaendee familia za mpoteaji pia kwa waandishi wote wa habari, ila kuna haja ya waandishi wa habari nchini kuwa na msimamo wa kukemea masuala ya kinyama kwa pamoja maana wakiachiwa Mtu mmoja mmoja madhara yake ni haya ya kutekwa na mafedhuli na kudanganyana eti wasiojulikana, mtoa taarifa za kubomoka kwa ukuta wa hostel apatikane lakini watekaji na wauaji wasipatikane wala kujulikana, kweli? Nchi hii tunakwenda wapi kufanya nini kwa matarajio gani? Kwanini isifikie mahali viongozi na waratibu matukio ya kinyama wasitambue wamepitwa na wakati? Inaumiza sana kuona nchi inayo nadiwa kuwa na amani kuwa na matukio ya makusudi kama haya halafu yeyote anaekaribia kutambua siri hizi za kiharamia anakuwa adui wa serikali kweli tuna nia ya dhati kujenga nchi au tunazugana ili wapige zao wasepe?
 
Ni tukio la kusikitisha japokuwa hatujui mini has a ki.etokea.
Haitakuwa vema kuinyoshea kidole serikali
 
Mungu amlinde huko aliko, tunaishi TANZANIA yenye miiba, watawala hawataki kusikia wasichokitaka.
 
2.jpg
 
Back
Top Bottom