Mwanza: Akutwa amekufa pembeni kukiwa na ujumbe ‘mke wa mtu ni sumu’

Mwanza: Akutwa amekufa pembeni kukiwa na ujumbe ‘mke wa mtu ni sumu’

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40-42 yaliyotokea katika mtaa wa Kanyerere kata ya Mkuyuni mkoani humo.

"Kando ya mwili wa marehemu kulikutwa ujumbe uliosomeka kuwa 'mke wa mtu ni sumu' watuhumiwa wanahojiwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Muliro jana Jumatano Machi 31, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Wakati huohuo, amesema wanamshikilia Mengi Muheta ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kishiri pamoja na wenzake 18 kwa tuhuma za wizi wa vitabu 529 vya shule za msingi.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako ulioendeshwa kati ya mwezi Februari na Machi, 2021 na kwamba vitabu hivyo ni vya shule ya msingi Bujingwa, Igoma na Manguluma zote za wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

Muliro amesema vitabu hivyo viliibwa kwa nyakati tofauti baada ya watuhumiwa kuvunja ofisi za shule hizo.

"Uhalifu huo umefanywa na walimu, walinzi na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wanataka kuvinunua jijini Mwanza ambapo ili kuidhinisha uhalifu huo walikuwa wanafuta alama maalumu inayowekwa kuashiria vinamilikiwa na serikali inayosomeka "hakiuzwi" ili waweze kuviuza kwa urahisi."

"Baada ya kuwakamata tunaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika wote, upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani,” amesema.

Pia, wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusafirisha gunia sita zilizokuwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela.
wapo serious na maisha
 
Kumbe siku hizi ndo wanawatamatisha kwa kuacha ka ujumbe ka kwaberi kuwa "MKE WA MTU SUMU"
 
Huwa ninawambia watu hiki kitu wananiona mjinga, ukioa mke alafu akachepuka achana nae wala hata ukimkuta kitandani kwako na jamaa wewe toka nje alafu rudi baadae mwambie aondoke, kuliko kumuua mtu alafu unaishia jela
Ni ushauri mzuri. Lakini siyo wakati wote inakuwa hivyo. Wakati mwingine unaweza kuwa na rafiki yako na anajua kabisa yule ni mke wako lakini anajitahidi mpaka anatembea naye! Na mbaya zaidi unaweza kukuta ametumia power ya fedha ambayo wewe huna! Hapo ni lazima nitamfundisha adabu. Ila sitatumia hasira. Nitaamwacha mwanamke kwa uzuri tu na baadae nitamtengenezea plani.
 
Hapo mwenyewe mke ni sawa amejiua yeye mwenyewe.
Anaenda jela kwa kosa la mauaji na kifungo chake ni maisha au kunyongwa.
Utakuwa umefanya nn? Unaenda kunyea kwenye ndoo kisa mwanamke? Amemuacha uraiani huyo mke. Ngoja wamzalishe sasa
Mpaka sasa huyo mke atakuwa ameshapata bwana.
Hapa dunia unatakiwa utumie akili na siyo hisia.
Huo utopolo siwezi kufanya. Ngoja akale ugali wa kengele
😂 😂 😂
 
Ili kumjulisha alichofanya ni utopolo.
Ningekuwa karibu, naenda kumtongoza huyo mke wa jamaa. Na siku ya hukumu, naenda naye huku nimemshika kiuno.
Siku akiwa jela, tunaenda kumsalimia jamaa, halafu mbele yake nampiga busu na kumnyonya mate mbele yake. Ili ajue alichokifanya ni utopolo kbsa
Hahahaha hapo ndipo unatakiwa ufikiri kabla ya kutendaa
 
Ili kumjulisha alichofanya ni utopolo.
Ningekuwa karibu, naenda kumtongoza huyo mke wa jamaa. Na siku ya hukumu, naenda naye huku nimemshika kiuno.
Siku akiwa jela, tunaenda kumsalimia jamaa, halafu mbele yake nampiga busu na kumnyonya mate mbele yake. Ili ajue alichokifanya ni utopolo kbsa
😂 😂 😂 Mkuu hawa wanawake ukiwafumania ni bora muachane kuliko kufanya maamuzi magumu mwisho unajikuta hatarini mwenyewe
 
Unaacha watoto, ndugu zako, mali zako ulizozihangaikia miaka yote pamoja na kazi kwasbb ya mwanamke uliyemkuta ukubwani. Cha ajabu kbl yako alikuwa na boyfriend wake wanakulana. Huyo jamaa fala sana
😂 😂 😂 Mkuu hawa wanawake ukiwafumania ni bora muachane kuliko kufanya maamuzi magumu mwisho unajikuta hatarini mwenyewe
 
Hapo mwenyewe mke ni sawa amejiua yeye mwenyewe.
Anaenda jela kwa kosa la mauaji na kifungo chake ni maisha au kunyongwa.
Utakuwa umefanya nn? Unaenda kunyea kwenye ndoo kisa mwanamke? Amemuacha uraiani huyo mke. Ngoja wamzalishe sasa
Mpaka sasa huyo mke atakuwa ameshapata bwana.
Hapa dunia unatakiwa utumie akili na siyo hisia.
Huo utopolo siwezi kufanya. Ngoja akale ugali wa kengele
Mwamba nakukubali sana ka mke kicheche achana naye utadili na wanaume wangapi ka mkeo mama huruma...

Ukifumania piga moyo konde chapa lapa jiweke bize tafuta kidemu cha kumbato wakati una recover..

Inauma sema ukikaza linapita kama kufuwa vile
 
Wanawake wangekua na wivu wa kimapenzi kama wanaume sijui nini kingetokea

Pole kwa wafiwa na muuaji maana atapatikana tuu, heri angeachana na huyo mwanamke kuliko kufia jela
Zizini dume moja majike mengiiii na Wala hayagombani, ila hata Kama Kuna majike mengi lete dume lingine zizini uone Vita Yake.
NI tabia ya asili tuwagonge wengi.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
MwanaFA ashatoa ushauri mzuri tu wa haya mambo sijui kwa nini watu bado wanauana

na we tafuta mnyonge wako um...
 
Hao jamaa waliotekeleza ili tukio ni wajinga. Inamaana hawakujua kama huo ujumbe walioacha ndio itakuwa starting point ya uchunguzi?
Kwenye issue ya mauaji huwa pamejificha mambo mengi sana.Na huenda waliandika huo ujumbe " mke wa mtu ni sumu" ili kupindisha tu kusudio la mauaji hayo.
 
Unatetea nini, angeweza kupiga nae selfie vilevile kuchapiwa kunauma,
Bado ni fikirishi ... Kama kauliwa na wahuni tu wakaamua kutia bosheni kwa kuandika kikaratasi na kukitupa !!?? Mme gani huyo aandike hivyo baada ya mauaji !!!?? Si anakuwa amejilengesha !!??
 
Back
Top Bottom