Nadhani mama anaanza sasa kuelewa kwamba JPM hakuwa mbaya bali aina ya nchi aliyorithi ndiyo ilimlazimisha awe tough. Na hiyo ndio siri ya kufanikiwa kwa urais wake.
Usicheke na nyani: sisi raia tunachotaka ni miundo mbinu bora, ni huduma bora za afya, ni kuona pesa ya wavuja jasho inafanya mambo ya maana yatakayobadilisha sura ya nchi.
Dunia haitakuheshimu kwa kuchekacheka na wahuni wanaotumia demokrasia kupenyeza ajenda zao binafsi. Dunia itakuheshimu kwa kuweka malengo na kuyatimiza. Ulaya haikujengwa kwa demokrasia wala nini usidanganyike. Ulaya ilijengwa na wanaume na wanawake wa shoka, ikiwemo hadi ukatili wa kutisha katika kuijenga. Sisemi ili kuijenga Tanzania itabidi ufanye ukatili mama, la hasha, siyo maana yangu hiyo. Ila bila shaka itabidi watu fulani fulani wakuchukie kama kweli unataka kuweka alama kama mtangulizi wako alivyoweka alama isiyofutika vizazi hadi vizazi ndani ya kipindi kifupi. Kama bosi wako walimwita JIWE, basi wewe wakuite CHUMA. Hapo utafanikiwa.