Mwanza: Askofu Mwamakula na Dkt. Lwaitama wakamatwa na Polisi

Mwanza: Askofu Mwamakula na Dkt. Lwaitama wakamatwa na Polisi

Hapana.

Tanzania polisi inatumika kisiasa.

Wameingia kwa sababu rais kasema, kinyume na katiba, kwamba mijadala ya katiba isimamishwe nchi itengeneze uchumi. Bila kutoa timeline wala metrics....
Polisi sehemu yoyote duniani ni mali ya wanasiasa,sisemi kwAmba ni haki au siyo lkni ndo inavokua,,yoyote atakaeingia madarakani polisi huyu huyu atatekeleza maagizo yake
 
kwA comments nyingi nilizo na nnaziona duh,, hivi kweli tunachukiana kiasi hicho WaTanzania!?😟😟, Hadi matusi kwa wazazi
 
Actually makongamano na mikutano ni haki ya kikatiba, bila kibali.

Kuna utaratibu wa kutoa taarifa polisi kama unahitaji ulinzi wa polisi.

Ukianza kuweka habari za vibali unaanza kuiminya haki ya kikatiba.
Vipi kama nikiamua kufanyia kongamano langu nyumbani kwako bila wewe kujua, kwakua tu katiba imeniruhusu?

Katiba imeruhusu ndiyo, lakini lazima vyombo vya ulinzi viwe na taarifa na utaratibu upangwe Ili kongamano lenu lisije kuingilia hali yoyote ile ya kijamii(kiusalama, kimazingira nk).

Sasa utakapoamua tu kwenda sehemu kufanya kongamano ilihali vyombo vya usalama sehemu husika vimekupa mwongozo wa kusubiri, ni lazima uchezee vitasa tu

Ndiyo katiba imeruhusu lakini kila kitu kifanyike kwa mpangilio.
 
Tofauti na tweeter na Jf vyombo vya habari ikiwemo tv na radio hazijaripoti kilichotokea Mwanza wala kufanya mahojiano na RPC Mwanza kujua sababu za kukamatwa kwa viongozi hao na wamefanya kosa gani, hii inanifanya nianze kutafakari kuhusu utendaji wa vyombo hivi awamu ya Tano.

Lakini pia kukaa kimya kwa vyombo hivi kunaashiria Wana maelekezo juu ya suala hili isipokuwa maelekezo yanatoka wapi hakuna anayejua.
 
Iko hivi dalili zinazojionyesha,yale ya awamu iliyopita ,huenda yakaboreshwa na kutuadhibu vilivyo mara nyingi zaidi ya awamu tangulizi,mpango wa siku mia za mwanzo ilikuwa ni kuwapumbaza watanzania ,ili baada ya hapo ni kurejea utaratibu wa awali uliowaumiza wengi kwenye nyanja zote na hakunaruhusa ya kuuongea ukweli.
 
Wanaumizwa kwa vipi hao wengi?
 
Wanaumizwa kwa vipi hao wengi?
Kwa wakati huu kuna nini,na wakati ulipita hapa karibuni kulikuwa na nini,tafakari tu kwa rejea miaka 3 Hadi 6 iliyopita linganisha tofauti na na muda wa hivi karibuni zaidi,zingatia dalili za sasa,matendo na matukio ya wakati uliopita katika muda tajwa linganisha na uje na mtazamo huru.
 
Ingependeza dini na siasa visiingiliane

Km wewe Ni askofu/shekhe basi ng'ang'ania hapo hapo

Achana na siasa
 
Back
Top Bottom