Mwanza hapajabadilika kwa miaka 13, bado nyumba zinachungulia kutoka milimani

Haya madini ndio huwa nayataka, pia umesahu uchumi wa nchi wameucentaralize Dar, kila muhamala kodi inahesabiwa dar, Dar wanapata mradi wa zaidi ya 2T kwa mwaka majiji mengine kwa pamoja hayafikishi miradi hata ya bilion 100, leo mtu anakuja kulinganisha kasi ya ukuaji wa Mwanza na dar haimake sense, keki ikatwe fair tuanze kuona ukuaji wa majiji yetu kama yalivyo majiji ya kenya.
 
Mwanza na mbeya miradi mnayopaswa kupewa na matundu ya vyoo, zahanati na madarasa na barabara za changarawe

Barabara za lami, flyovers, conference centres, interchange, outering roads na inner ring, viwanja na arena na vyuo vikubwa vinapaswa kupelekwa Dar, Dodoma na Arusha nyie wengine muamie burundi.
 
Nchi ngumu sana, airpot ya mwanza isubiri kwanza tupo bize kuvunja na kujenga terminal II, soko la mwanza lisubiri kwanza kariakoo ifanye kazi, daraja lisubiti BRT phase iv ikamilike.
 
Fafanua hii miradi ilikuwa inaisadia nini au wafanyabiashara walifaidika nayo kivipi? Na iliinua Mwanza kivipi?

Mkuu mbona ni simple economic analysis,mkandalasi akilipwa pesa atanunua materials atalipa wafanyakazi,wafanyakazi watalipa mama ntilie and the cycle goes on and on.
 
Binafsi mwaka 2012 nilikuwa naishi maeneo ya nyegezi malimbe,juzi nilienda tena nikitegemea kumebadilika nilipakuta vilevile nilishangaa sana

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Malimbe hapawezi kubadilika kule maana uwekezaji wa maana unaofanyika ni Hostels nazo zinategemea zaidi wanafunzi wa SAUT.

Malimbe, Luchelele na Sweya sitarajii mabadiliko yoyote makubwa ndani ya miaka (10-20) ijayo.
 
Kwani kule ni hostel tu,we unaijua malimbe kweli?alafu sikuwa mwanafunzi wa kolo

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Ulitaka ukute nyumba za zamani zimebomolewa na kujengwa mpya au maghorofa huko malimbe? Jiji la Mwanza lilishaendelea na lilishajaa toka ukiwa kiunoni mwa baba ako.kinachofanyika inaexpand kwenda Magu na Misungwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…