Mleta mada,
Target kubwa mbili za SGR ni kiuchumi na huduma kwa wasafiri (wananchi)
Katika target ya kiuchumi SGR itapita pale Isaka ambapo ndio lango kuu la bandari kavu ktk kuhudumia maeneo hasa ya Kigoma, Kahama, Geita nk nchi jirani kama Rwanda, Burundi nazo zitanufaika pia
Katika kuboresha utoaji huduma ktk usafiri, endapo SGR itafika Mwanza basi wasafiri wa mikoa jirani na Mwanza kama Shinyanga, Mara, Geita, Kagera watakuwa wanufaika wakubwa ktk huduma ya treni hii.
Hvyo kwa namna hiyo utaona ufikaji wa treni mpaka Mwanza utahudumia wasafiri wa mikoa takribani MINNE inayozunguka/jirani na Mwanza
Pia, tusisahau hii SGR ni mpango mkakati wa nchi kuendelea kuwin soko lake la kuzilisha nchi jirani kwasababu mwenzetu Mkenya nae anakimbizana na SGR yake ili apore soko letu hasa nchi ya Rwanda na Burundi,, hvyo natoa raí kwa viongozi wetu waongeze kasi ktk ujenzi wa SGR yetu