The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Ndiyo maana ya mjadala...Mbona husemi bwana Ladogosa amejibuje hilo, unakuja na maoni ya upande mmoja?
Kama na wewe ulifuatilia mjadala huo, ungeweza kusema tu kuwa, hata hivyo DG wa TRC ktk kulitolea ufafanuzi hilo, amejibu hivi na vile...
Anyway vyovyote iwavyo...
Wote tunajua kuwa mpango ni kujenga reli ya SGR kwenda hadi huko Kigoma...
Kinachogomba hapa ni vipaumbele (priorities). Kwamba, tunajua kama kweli tutasambaza SGR nchi nzima, basi itatuchukua miaka hata 30 ijayo kukamilisha project hii...
Jambo muhimu ilikuwa tuanze kujenga kuelekea wapi ili tuanze kuvuna faida haraka...
Ni ujinga kuanza kuelekeza reli ya SGR utakayoijenga kwa awamu kadhaa na kuchukua miaka 30 kuikamilisha awamu zote, kwenye eneo ambalo mahitaji yake ya usafirishaji mizigo ni 10% badala ya kuanza na eneo ambalo linasafirisha mizigo 41% kuelekea huko...!!