Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Lawama zote kwa Magufuli kwa kuwa na upendeleo na ubinafsi! Alidhani kwa upendeleo huo atapendwa na wasukuma matokeo yake wanashangilia kutoweka kwake kuzimu!
 
Mleta mada,

Target kubwa mbili za SGR ni kiuchumi na huduma kwa wasafiri (wananchi)

Katika target ya kiuchumi SGR itapita pale Isaka ambapo ndio lango kuu la bandari kavu ktk kuhudumia maeneo hasa ya Kigoma, Kahama, Geita nk nchi jirani kama Rwanda, Burundi nazo zitanufaika pia

Katika kuboresha utoaji huduma ktk usafiri, endapo SGR itafika Mwanza basi wasafiri wa mikoa jirani na Mwanza kama Shinyanga, Mara, Geita, Kagera watakuwa wanufaika wakubwa ktk huduma ya treni hii.

Hvyo kwa namna hiyo utaona ufikaji wa treni mpaka Mwanza utahudumia wasafiri wa mikoa takribani MINNE inayozunguka/jirani na Mwanza

Pia, tusisahau hii SGR ni mpango mkakati wa nchi kuendelea kuwin soko lake la kuzilisha nchi jirani kwasababu mwenzetu Mkenya nae anakimbizana na SGR yake ili apore soko letu hasa nchi ya Rwanda na Burundi,, hvyo natoa raí kwa viongozi wetu waongeze kasi ktk ujenzi wa SGR yetu
 
Kuna wakati niliweka bandiko humu kuhusu upendeleo uliofanywa na serikali ya awamu ya 5 kupeleka SGR Mwanza badala ya Kigoma ambapo ndiko economic viable kwa huo mradi. Kikundi fulani kikiongozwa na Mgambilwa ni muntu wakapinga hoja hiyo na kushadadia kuwa kupeleka SGR Mwanza ni bora zaidi.

Kwa takwimu hizi nathubutu kukitambua kukundi cha kina Mgambilwa kuwa ndio wale Sukumagang.

Vv
 
Hivi wewe unafikiri SGR inajengwa kwa ajili ya nchi jirani tu??!! Mbona hujaelezea mizigo ya ndani ya nchi upande wa Kanda ya Ziwa??
Nchi jirani ndiko kuna biashara zaidi na zenye kipato ambacho kingerejesha gharama za mradi kwa haraka.

Vv
 
Mwenzake alikuwa na fikra zenye ukakasi mwingi sana

Do we still have the same hangover? SGR ni mradi wa Tanzania na kuna namna uchumi unavyoendeshwa.
Mahojiano ya saa chache ndio yanatoa hatima ya project kubwa kama SGR?
 


Kigoma ni nchi jirani iliyopakana na Tanzania kwa upande wa magharibi.--- watu wa kigoma ni Warundi, kwanini maendeleo ya Tz yapelekwe nchi jirani???---- mmelogwa?!!
 
Mkuu, unapoleta mada ya aina hii ni muhimu utoe taarifa kamilifu kama unataka ijadiliwe kwa kina.

Huyo mtaalam aliyesema hayo ni nani ni wewe mwenyewe, maanake tayari inaonekana umedakia alipoishia.

Kama unayo shule, elimu hiyo haikusaidii chochote kuhusu uelewa wa mambo ya takwimu. Kigoma inachukuwa asilimia 41, na inayoelekea Upande wa Zambia ni asili mia ngapi, maanake nayo hupitia bandari ya Dar es Salaam, na ni sehemu ya "central corridor". Taarifa yako haisemi hiyo mizigo ni ile inayosafirishwa kwa njia ya gari moshi pekee, au pamoja na usafirishaji mwingine?

Je, mtaalam kaeleza kwamba uwepo wa SGR hauwezi kuongeza hiyo 10% inayoelekea Mwanza, itabaki tu ni ileile?

Shida yako kubwa hapa ni kuzipambanisha Mwanza na Kigoma? Unataka tujadili hilo?

Huyo mtaalam kasema reli kwenda Kigoma haitajengwa?

Hebu soma tena kichwa cha mada yako:

"Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41%..."

Halafu na wewe unajihesabu kwamba unaelewa kitu unachotaka watu wakijadili!
 
Uchumi wa Rwanda na Burundi kwa pamoja ni sawa na asilimia 17 ya uchumi wa Tanzania. Wakati huo huo mikoa ya Mwanza, Shinyanga,Geita, Mara na Bukoba kwa pamoja zinachangia asilimia 11 katika uchumi wa Tanzania.

Hata kama tumeamua kufikiria kibepali namna gani, it does not make economical sense to direct such an infrastructure towards foreign countries sababu tu uchumi wao unauzidi uchumi wa sehemu ya nchi kwa asilimia 6 by comparizon.

hiyo idadi ya mizigo wanayozungumzia hao bbc waeleze inathamani kiasi gani au inachangia kwenye uchumi wa nchi yetu kwa kiasi gani?
Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi.
 
Natoa ushauri mmoja kwa serekali yetu tukufu, hatujachelewa sana!! Contract ya Isaka to mwanza ibadilishwe iwe Makutopora to Isaka!! Gharama zote za Isaka to Mwanza kujenga reli ya kuwa white elephant, hayo mabehewa yatapitia wapi hadi isaka kama huna sgr maktopora Isaka!!!???
 
Ihamishe upeleke kwenu
 
Wivu wivu wivu!
Hizo asilimia zimepatikanaje? Na kwa kipindi gani?
Hayo maendeleo unayoongelea yanaahusu vitu gani?

utakuwa na matatizo yaa akiri hasa yaakichangiwa na matatizo ya kurithi kwenye ukoo wenu.
Nenda kwa Mungu utubu
 
Sgr haijajengwa kwa ajili ya nchi za nje tu ila ili kusisimua ukuaji uchumi wa ndani. Ukilinganisha uchumi wa ndani mwanza iko juu kwa potential kuliko kigoma. Hata hivyo mpango wa sgr hauishii mwanza tu ila ni hadi kigoma mpanda hadi kalema. Kwa hivyo ni suala la mpango tu.
 
Miradi ya kipuuzi na isiyo na tija kama hii hata kwa wanaoishabikia sio ya kuipelekea pesa.

Hivi huko serikalini kuna watu kweli wanaofikiria? Yaani baada ya kukamilika waanze tena kutuongezea kodi eti kulipia kujiendesha? Huu ni wehu
Vyombo vya usafiri tupanda kwa kuchagua kitachokuwa kizuri kurahisisha safari zetu, tunahitaji na viwanja vya ndege Kila wilaya Kila mtu anapenda raha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…