Mwanza: Jiji lenye wakazi Duni na mpangilio wa ovyo wa makazi Tanzania

Mwanza: Jiji lenye wakazi Duni na mpangilio wa ovyo wa makazi Tanzania

Mbona capri point ni milimani na kuna miamba kama yote lakini pamejengeka vizuri tu! Mi naona ni suala la serikali kuamua na kushirikisha wadau ...hapo mabatini panaweza kuwa pa kishua balaa kama serikali ikiamua
Hakuna sehemu isiyokuwa slum ni raha ya jiji, ukitaka maeneo ya hadhi ya juu mbona yapo mengi tu, tatizo mnanongwa sana nyinyi.
 
Endeleeni kujifariji na vichaka vyenu, eti kasoro Dodoma.
Dar, Arusha, Mwanza kote ni uswazi... lakini haimaanishi zimezidiwa na Dodoma kiuchumi (Arusha na mwanza inawezekana zishiapitwa na Dom)...
Ila kwenye suala zima la mipango miji na upya wa majengo haina ubishi hakuna sehemu bongo sasa hivi inazidi Dodoma.
 
Hakuna sehemu isiyokuwa slum ni raha ya jiji, ukitaka maeneo ya hadhi ya juu mbona yapo mengi tu, tatizo mnanongwa sana nyinyi.
Mwanza naijua nje ndani hamna eneo la hadhi ya juu zaidi ya capri point...labda unitajie sehemu nyingine ambayo ina barabara nzuri hotel, migahawa top class, international school, bank, nk nitajie hiyo sehemu labda naweza kuwa siijui
 
Dom ndio Jiji lenye mtandao mpana wa barabara za lami hapa Tanzania....ukiingia city center barabara za vumbi ni za kuhesabu kamwe usilinganishe na Mwanza aisee kwenye upande wa barabara za lami Dom wanapendelewa sana just imagine barabara ya Ring Road zaidi ya kilometer 100 zinajengwa .
Halafu kwa kukusaidia tu Hali ya hewa haijawahi kuwa kigezo cha kupima ubora wa mji.Dubai,Cairo, Windhoek ni semi desert lakini kimaendeleo haikamatiki. Kama Hali ya hewa ingekua ndio kigezo cha kupima ubora wa mji basi Lushoto,Mafinga ,Makete,Njombe zingeongoza Tanzania,😂😂
Ulichozungumza wameshazungumza wenzio na wamejibiwa Dodoma ina wigo mpana sana wa barabara za kiwango cha lami hilo halina ubishi kiasi kuna barabara hazina magari yanayopit, unlike kwa Mwanza barabara zote hata mbovu ni zina magari na yanapita hyo inamaanisha Mwanza inauhtaji mkubwa sana wa barabara za lami ila inapuuziwa.

Let's say barabara za Mwanza ziwekwe km za Dodoma, kuna watu mtajinyonga aseeh 😅

Moreover, Mwanza ni kubwa na pana kias hata sehemu zisizo na tarmac roads ni zimechangamka kuzd sehemu za Dodoma zilizo na lami.

Hapa sasa ni wanaopambaniwa na serikali vs wanaojipambania 😁 na hapo sasa siku serikali iktosha kujenga hzi nyumba zao na wakaona wamemaliza kuweka lami vibarabara vyenu ndio mtasimamia hapo hapo unlike Mwanza😁 soon kunakuwa na Manispaa 3 nyie ni Manispaa 1 hebu peleka uchafu hko mzee 😁
 
Kiufupi Dodoma hakuna "shida" ya maji ila kuna "mgao" wa maji kuna mitaa maji yanatoka marambili kwa wiki ,mingine mara tatu kwa wiki,mingine maranne kwa wiki n.k. Tanzania hii hakuna mji wowote ambao maji yanatoka 24/7 mwakamzima😆😆. Mwanza penyewe licha ya kuzungukwa na Ziwa Victoria bado kuna changamoto ya maji
Ila we jamaa 😅 Dodoma sehemu gani mnapata maji kwa uhakika yani haya maji yanayotoka kwa dk 40 had saa1 kwa siku kwenu ndio uhakika!? Kwann mnaficha shida zenu!? Sema ukweli ujue mm ni mkazi wa Dodoma nlkuwa Ihumwa now npo Makulu au wenzetu sehemu zingine ninyi maji uhakika right.
 
Mwanza kuzuri especially hali ya hewa. Huko milimani ni hela tu! Panaweza kujengeka vizuri tu kama Capri point kukawa na mitaa iliyopangika vizuri na barabara nzuri
Hawa washamba hawajui kitu bas wakipita road wakaona hzo nyumba wanajua kote ni hvo, hawajui hata kuangalia miji mizuri aseeh yan hapa Dodoma ndio unafananisha na Mwanza huu si uchawi kbs nmelia sana mm.
 
Mipango miji ndiyo wa kulaumiwa. Wanaangalia watu wanajenga kiholela. Wao ndiyo kazi yao kupanga hapa kuwe hiki na kile.

Dar yenyewe iangalie toka juu, hakuna mpangilio, watu wamejenga kama uyoga pori, unavyojiotea porini. Mipango miji ndiyo mchawi wetu, wanakula mishahara ya bure tu.
Tatizo ni siasa na wanasiasa akifuatiwa elimu.

Nenda Skanska au Mtongani ya kunduchi
 
Dom baada ya miaka 10 ijayo hata dsm itaisubiri, jamaa anataka kulinganisha dom na uchafu,,, mwanza hata kufkia hadhi ya mtaa mmoja wa michese tu bado ikasome,
Hata Dsm ikisimama leo bado Dodoma haiwezi ipita kwa lolote lile ndani ya miaka 50
 
Habari wakuu,

Katika Pitapita zangu Juzi nilibahatika kupita Jiji la Mwanza baada ya miaka mingi kupita, Ni wazi kwamba niliwahi kuishi Mwanza miaka kadhaa nyumba baada ya kutoka mkoani, Kusema kwel kwa Umri ule na kipindi kile kwa kuwa nilikuwa sielewi lolote kuhusu Jiji nilitokea kupapenda sana,

Kwa kuwa ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kushuhudia Eneo lenye mpangilio wa makazi ya karibukaribu na changanyikeni ya watu nilipenda sana na niliamini Mjini kunapaswa kuwa namuonekano ule.

Ila baada ya kukaa na kubahatika kwenda Majiji mbalimbali ya Tanzania na baadae Kutia Nanga Dodoma na kuwa mkazi wa kudumu wa Jiji la Dodoma na kuzoea maandhari ya makazi ya watu na jinsi Jiji lilivyopangika,

Hakika jana baada ya kubahatika kupita Mwanza nilibaki kinywa wazi baada ya kuona majengo ya hovyo na vinyumba vya kizaman vilivyojengwa bila mpangilio maalumu kuonekana Maeneo ya Mjini kati tena makazi ya watu Duni na vinyumba vya hovyo sana.

Nilipita njia ya Kutoka Nyamongoro Stand mpya Mabus hadi Nyegezi Stend kuu ya mabasi Hakika mitaa niliyopita kwenye Gari ilikuwa inatisha kwa mwonekano, kuanzia Igoma, Nyakato, Buzuruga, Mabatini, Nata, Nyakabungo, Sahara, had Nyegezi ni vijumba vya hovyo sana vilivyoegeshwa pembeni ya mawe na kuezekwa kwa Bati kuukuu na Mawe Juu,

Hamna hata barabara za mitaa za kueleweka, na hakuna hata mpangilio wa makazi vinyumba vimekaa kutazama jirani anamwangalia Mwingine na choo cha jirani kipo mlangoni mwa Jrani kuna watu wanaishi Juu ya milima kiasi kwamba hata wamiliki wa maeneo yale hawana accessories ya kumiliki usafiri, Maana hawana njia za kupita,

Majengo ya kizaman yenye Bati za kizamani zilizojaa kutu na Kupambwa na vivyesi vya ndege, Aslimia kubwa ya Eneo ni majarubani wakazi na watu wote wanaokalia jiji wanaonekana ni watu hawana Nuru nyusoni mwao, Wanaonekana ni watu wenye maskitiko mda wote, asilimia kubwa ya Vijana wadogo wanaonekana ni watumiaji wa Mihadarati usela mavi na Usela Nya.

Kusema kweli nipongeze sana Dodoma ni Moja kati ya Majiji Bora yenye mpangilio wa mzuri wa makazi ya watu na hadhi ya kukalika na watu Kuanzia Mtumba, Ihumwa, Nzuguni, Swaswa, Kisasa, Meliwa, Ipagara, Area C, Area A, AreaD, Makulu, Ostabey, Mkalama, Mkonze, Ntuka, Nkuhungu, Mnada mpya hadi Nala, Dodoma haichoshi hata mgeni akizungushwa jiji halimchoshi anataman kuendelea kutaliii,

Changamoto Dodoma hakuna Refreshing Area za Maana kama Mwanza, ila katika upande wa Makazi Dodoma is the Best.
Unaongelea Mwanza ipi?
 
Hv kwann kila Jiji hupenda kulinganishwa na Mwanza tuanzie hapo kwanza 😅 yaan hadi Mbeya tena mwisho wale wa Kahama na wao waje na uzi wa kutaka battle na Mwanza.
Ukiondoa dar, MWANZA inabakia kipimo Tosha kwa majiji na miji yote iliobaki, usishangae hawa jamaa kujaribu kulinganisha ingawa mimi naona Mwanza is the best.
 
Kwa sababu Mwanza inajiita Jiji la pili Kwa Ukubwa Tanznaia lakini halifananii na hiyo hadhi ndio maana inalinganishwa.

Mfano Magorofa Arusha,Tanga, Kilimanjaro na Dodoma zote zimezidi Mwanza Sasa hapo ndio Jiji la pili Hilo? 😂😂😂

Pili angalia ujenzi wa mabanda ulivyo,hivi ndio Jiji la pili linakuga hivyo?

Kiuchumi Mkoa wa Mwanza ni namba 2 lakini nyuma yake kuna Mbeya,mpaka hapo hakuna kuzidiana kokote Kwa maana ku justify hadhi ya namba 2

Sababu zingine ongezea 🤣🤣🤣🤣😁
Dodoma kwa magorofa gani
? Ukiondoa majengo ya serikali hamna lolote hapo dodoma.
Kwa mbeya ndio unyamaze kabisaa maana haina mpangilio wowote kuzidi mwanza, kiuchumi pia mwanza iko vizuri kuliko mbeya,
Arusha hakuna jipya kabisa,
Mwanza ni Jiji namba 2 ukiondoa dar es salaam ambayo ndio namba moja kama ukibisha na hapo rudi darasani🤣🤣🤣🤣
 
Naona unataka battle ya Mwanza na kijiji chenu cha Dodoma
🤣🤣🤣🤣🤣, tena kijiji haswa Dodoma nimeishi na Mwanza nimeishi, hawa malimbukeni wanataka kuleta battle za hovyohovyo, Dodoma inatakiwa ibatle na akina arusha,tanga sababu hata mbeya bado Dodoma haiwezi ipata
 
Mwanza naijua nje ndani hamna eneo la hadhi ya juu zaidi ya capri point...labda unitajie sehemu nyingine ambayo ina barabara nzuri hotel, migahawa top class, international school, bank, nk nitajie hiyo sehemu labda naweza kuwa siijui
Taja dodoma sehemu zenye hadhi 🤣
 
Back
Top Bottom