Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Mbaya nimekumbuka kumbe hukumu ilishapita kabisa 🙄🙄then kaachiwa .
Huyo bwana baada ya mauaji, alihukumiwaga KUNYONGWA Hadi KUFA.

Amekaa Jela wee, mwaka Jana ndo wakaanza habari za Rufaaa zikiingozwa na Kibatala !!.

Leo jamhuri imesema Haina Nia ya kesi, Mahakama imemuachia huru .

Wakati wanatoka tu, Polisi wakawamkata Tena.
 
PUNGUZA UPEPO
HIZI NI ZAMA NYINGINE.

Alihukumiwa kwenye utawala gani?
Unatambua mazingira ya kosa lake?
Unatambua maisha ya wafanyabiashara wa level zake yalikuwaje wakati huo?
Manji UNAMKUMBUKA?
Mo unamkumbua?
Super shem yuko wapi?

Maisha hayako ivo rafiki yangu.
 
Watakuja wale jamaa sijui wakili msomi na yeye anaangalia pesa tu.
 
Ndugu yangu,kuna issue nilikuwa napigania...pesa zimenitoka kweli
Majuzi Kati nilikua Kuna Vijana wapatao wanne nmewafikisha Mahakamani


Huwezi amini, Hakimu wa Kesi hiyo, akawa anawapigia simu watuhumiwa anawaambiaje" Huyu Dr kesi yake nyuma yake inawatu wazitk, mkicheza mtapoteaa , Sasa tuongee kiutu uzima".


Fikiria huyo ni Hakimu aliyetakuwa kusimamia haki, ila anataka watuhumiwa, wampe Hela !!.
 
Sure thing, chini ya Magu haya maujinga yasingetokea. Aisee nimechefukwa sana
 
Mtu alishahukumiwa KUNYONGWA, wamekuja kusubiri JPM amekufa, ndo wakaamua kurudi kwenye rufaaa, na ujanaujanja na Rushwa Rushwa kibao ,Leo ameachiwa huru..
BADO SIJAELEWA

Mshtakiwa - at this point muuaji, msubiri kunyongwa, condemned, KONDEM - kakata rufaa.

Ina maana kesi anaeileta mahakamani ni KONDEM

Serikali itasemaje haina nia ya kuendelea na kesi, wakati kesi kaianzisha KONDEM ????
 
Inawezekana hii kesi inamuhusu sana, kwa hiyo hawezi kuwa objective.

Anaandika kwa hisia kali na mihemuko.
 
Tena rushwa ni wazwaz
 
Sasa kama imeamuliwa kuwa kesi ianze kusikilizwa upya kutokana na kasoro zilizo onekana tatizo liko wapi? hakuna cha rushwa wala harufu ya rushwa.

ila kama hakuwa na hatia basi ni bora angeachiwa tu huru, kwa nini ateseke tena kuanza kusikiliza kesi upya kwa uzembe wa upande mwengine?!
 
Kama alishahukumiwa basi inamaanisha kesi ilishaisha. Na kama kesi ilishaisha basi mwendesha mashtaka hawezi kusema tena ''hana nia ya kuendelea na kesi''. Inaonekana alikata rufaa na akashinda lakini siyo kweli kuwa mwendesha mashtaka amesema hana nia ya kuendelea na mshtaka.
 
Ingekuwa ni ndugu yangu ameuawa na huyo bwana ningelipa kisasi hadharani kwa risasi za kichwa alafu nisubiri kesi yangu itakavyokuwa
Ningeiomba mahakama itumie kigezo ilichotumia kumwachia huyo bwana watumie hicho hicho kuniachia mimi
Na kama kuna ndugu yake ambaye atakuwa na roho kama yangu aje kufanya nilichofanya kwa ndugu yao na iende hivyo mpaka dunia iishe kama wanaona walichofanya ni sahihi sana
 
Kunamazingira ya mauaji,
Wengine wanaua kwa ajili ya self defense
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…