ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Kwani kesi imesikilizwa!?Upande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.
Kuna watu huwa wanabeza uwezo wa Kibatala kuwa hashindi kesi huyu jamaa ni moto
Copy hii imfikie yule kopa gas
Sema wasambaa kwa kesi atakoma
Ova
Huenda hivi vielim vya sheria , ndivo vinavyowatoa kwenye Ubinadamu .
Kosa ni kosa, jinai ni jinai, jinai ilothibitika haikupaswa kutetewa na mapungufu ya sheria ,ushahidi au mashahidi wenyewe.
Wewe, Umeua mtu.... Nani anayeweza kuthibitisha Dhamira yako ya moyon kua hukuua Kwa kukusudia ??. Mazingira ??.
Inawezekana Sijui sheria, ila Sina huo ujinga wa kushindwa kujua kua hapa Kuna RUSHWA NA UHUNI TU.
Majuzi Kati nilikua Kuna Vijana wapatao wanne nmewafikisha Mahakamani
Huwezi amini, Hakimu wa Kesi hiyo, akawa anawapigia simu watuhumiwa anawaambiaje" Huyu Dr kesi yake nyuma yake inawatu wazitk, mkicheza mtapoteaa , Sasa tuongee kiutu uzima".
Fikiria huyo ni Hakimu aliyetakuwa kusimamia haki, ila anataka watuhumiwa, wampe Hela !!.
Kumbe hua kuna scenario wakati mwingine zinazoruhusu kuua?Unajua scenario mpaka akaua hao watu?
Kwa spidi hii ya bwana DPP tegemea yule Mende wa gesi ya mkopo kurudi uraiani January mwakani.
Hivi rushwa wanapokea pesa taslim au benki transfer?
Hili halikubaliki na kiufupi mwenye Pesa awamu hii hawezi fungwa Wala kushtakiwa.Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni ya Mabasi ya J4 Express, alidaiwa kuwaua kwa kuwapiga kwa risasi Ally Abeid Mohamed, mkazi wa Igoma na Claud Sikarwanda, mkazi wa Nyasaka Ilemela, Julai 13, 2015, majira ya saa 4:00 usiku, eneo la Nyakato Boma kwenye ofisi na karakana ya magari ya mfanyabiashara huyo.
J4 alitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ya Ali Abeid na Claude Sikarwanda, hukumu iliyotolewa Machi 13, 2020 na Jaji Mfawidhi wa Makahama Kuu Mwanza, Sam Rumanyika.
Hata hivyo Mahakama ya Rufaa ilibatilisha adhabu hiyo na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu Mwanza,iliagiza kesi hiyo jinai namba 131/2017 isikilizwe upya.
Mahakama imemwachia huru leo, baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo. Upande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.
------
Nyie Mahakama acheni kuona watu ni mbuzi, Acheni Rushwa, Rushwa ni adui wa haki, Rushwa anatesa, Rushwa anaumiza watu
Hivi mtu aliyeua watu wawili kwa risasi , watu wamekufa, wamezikwa , na mmemhukumu kunyongwa hadi kufa, leo hiii kisa rufaa, kwamba meza imepinduka? Mpaka aachiwe huru?
Mbona mnakoswa huruma nyinyi?? Mbona hamuwakumbuki watu walowapoteza wapendwa wao? Tunarudi wapi?
Huu ndo utawala wa Rais Samia, wenye kufuata misingi ya Demokrasia?
Haya basi, jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi, mtufufulie ndugu zetu walouawa basi, na sisi tucheze nao, tupige nao stori, likiwashinda hilo, basi tuambiani, walowaua ndugu zetu wawili kwa risasi ni akina nani?.
Mambo ya ajabu kabisa na aibu ilopitiliza.
Mnatanguliza rushwa mpaka kwenye maisha ya watu, kama mlimuhukumu kunyongwa, leo hii inakuaje mnakoswa nia ya kuendelea na kesi? Kwamba hakukutokea tukio la mauaji? Kwamba hamna aliyekufa? Na kama alikufa nani alimuua?? Kama sio Jumanne, ni nani aliwaua?? Kama ni yeye, imekuaje aachiwe huru? Mtufufulie ndugu zetu .
Shame on you!! Rushwa rushwa mpaka mnauza roho za watu??
Wapumbavu kabisa , mlaaniwe na vizazi vyenu, na hizo rushwa mnazokula, pesa hizo ziendelee kuwapa umasikini wa roho na mpoteze heshima mbele ya watu .
Huyu jamaa alihukumiwa hapa !!👇
Leo kaachiwa Huru, ila Polisi wamejifanya kumkamata Tena, ili kupima upepo, ili hali JAMHURI ndio hiyo hiyo Polisi !!
Scenario ndio inahalalisha mauaji? Kwani alivamiwa?Unajua scenario mpaka akaua hao watu?
Kutetea uhalifu Ni upuuziUpande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.
Kuna watu huwa wanabeza uwezo wa Kibatala kuwa hashindi kesi huyu jamaa ni moto
Sasa hii inahalalisha vipi muuaji kuwa huru?Marehemu walimuuzia mzigo wenye carat/quality ndogo wa dhahabu, wakalipwa %, fedha nyingine zikabaki, jamqa kuupeleka sokoni, ndio anagundua tayari ameshawalipa jamaa ela nyingi.
Jamaa nao wanaendelea kumdai, yeye hataki walipa tena fedha iliyobaki maana mzigo quality ilikuwa ndogo. Majibizano ndio hadi kuwaua.
Ndio maana Ndumba Ni muhimu San kulipa kisasa..wachukur sheria mikononi tu kama serikali imeshindwa kufanya kazi yake, simple.
Sawa Ila kwa kuvamiwa usiku it makes sense..Wekeni hukumu hapa tuone ni mazingira gani jamaa kachomoa pini. Inatokea kabisa mzee mmoja aliachiwa huru baada ya kumchapa shaba askari polisi aliekuja mkamata usiku nyumbani kwake amelala na mke wake. Mzee akawaambia polisi wasithubutu kugusa geti, jamaa wakazama ndani kibabe. Akawachapa risasi mmoja akakata moto pale pale.
Mzee alikomaa kwamba hawakuwa polisi ila majambazi,jamhuri inakazania ni polisi,mzee alipigwa kifungo cha maisha badae akachomoa pini huko huko kwa pilato kwa rufaa. Japo mzee alijua kweli ni askari ila akaamua kuwachapa shaba kibabe!
This makes sense kwamba wamemalizana nje Jambo ambako Ni sahihi kisheriaHi kesi Mahakama ya Rufaa iliamuru ianze upya. Sasa nadhani kwenye process za kuanza nadhani Kuna mazungumzo yalifanyika baina ya mtuhumiwa na familia ya Marehemu wote ndipo wakakubalina fidia, ndio maana kesi imeisha haijafunguliwa Tena.
Unaona ilivo ngumu kutaja bei ya roho yako lakini kuuawa kwa ajili ya pesa unaona ni sawaKama unataka kununua tutafutane personal biashara itafanyika usijali
Unawajua? Maana wanahamishwa hao afu inakuwa Ni pannel,tafuta mmja ndio awe wa mfano.Rushwa inaanzia polisi! Kwenye kesi hizi za mauaji wakishalamba rushwa wanavuruga sana ushahidi. Tangu wamevuruga kesi ya kuuawa kwa dadangu sina hamu kabisa! Ushahidi ulikuwa wazi kabisa mpaka simu waliikamata yenye mawasiliano ya kuua na mtuhumiwa walipomkamata alikiri kuua. Sasa jamaa amewekwa ndani muda wa miaka minne huku nyuma polisi wakavuruga ushahidi wote hata haya maelezo wameyaficha mpaka mtuhumiwa amekuja kuachiwa! IPO siku nitashughulika na mmoja mmoja! Kila nitakapommaliza mmoja nitasema bado mmoja mpaka waishe! Polisi pumbavu kabisa!
Huu mzaha hata Kama Sina hela nitakutafuta kwa Ndumba mzee unless iwe muuaji ame kompromise na familia wakamalizana sio kuhonga mapolisi afu wenye ndugu wakaachwa pembeni.Sometime haya mambo yanafkrisha Sana , J4 tangu afungwe gari zake zote hazionekan barabarani , watu wengi wamelost ajira , ni kweli Kaua watu wawili , sasa mnaenda kumuua tena na yeye , Hz ni hesabu mbovu , Bora arud watu wapate ajira maisha yaendelee...!!