Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Hi kesi Mahakama ya Rufaa iliamuru ianze upya. Sasa nadhani kwenye process za kuanza nadhani Kuna mazungumzo yalifanyika baina ya mtuhumiwa na familia ya Marehemu wote ndipo wakakubalina fidia, ndio maana kesi imeisha haijafunguliwa Tena.
Yes inawezekana Kuna Mambo nyuma ya pazia hatuyajui.
 
Alafu jamaa analeta habari za scenarios hapaa.

Watu wanahukumiwa kunyongwa kisa wamechoma mwizi mtaani aloiba Kuku akawapikie wanawe.

Alafu aliyeua watu Kwa makusudi anaachiwa??


Aibu aibu aibu ..

ANGEKUWEPO HAYATI MAGUFULI, HUU UJINGA USINGETOKEA KAMWE.
Kuna wakati unaona Kabudi na Bashiru walikuwa na akili kubwa sana ya kupinga huyu mama kuchukua Uraisi kaifanya nchi imekuwa ya kizuzu sana. Magufuli kosa lake kubwa kuona wapinzani ni wabaya wake. Huu ujinga wakati wa Magu kamwe usingefanyika.
 
Acha ujinga wako, haijalishi nyuma ya mauaji Kuna sababu zipi.

Kuua ni kuua tu .... Kwahiyo siku hizi, mtu akikutendea baya, ni Kuua tu, kwakua nyuma yake una sababu?.

Kuua siyo jambo kuu, Jambo kuu ni Yupi ameweza kusimama na kupangua vifungu Vya sheria

Kumbuka mahakama haifanyi Kazi kwa hisia
 
Kuua siyo jambo kuu, Jambo kuu ni Yupi ameweza kusimama na kupangua vifungu Vya sheria

Kumbuka mahakama haifanyi Kazi kwa hisia
Acha masihara , Yaan weee Umeua na imethibitika umeua, ,, alafu kwakua Kuna vifungu Kadhaa Kadhaa, vya kisheria, basi uachiwe huru?.

Inawezekana Sasa, Tanzania ndio Nchi yenye mfumo wa Mahakama wa kijinga kupindukia .

Na ndio maana wanafel sana saana mitihan Yao.
 
Kama familia za wahuka hawatapaza sauti, basi waliitwa mezan mambo yakazungumzwa.
 
Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni ya Mabasi ya J4 Express, alidaiwa kuwaua kwa kuwapiga kwa risasi Ally Abeid Mohamed, mkazi wa Igoma na Claud Sikarwanda, mkazi wa Nyasaka Ilemela, Julai 13, 2015, majira ya saa 4:00 usiku, eneo la Nyakato Boma kwenye ofisi na karakana ya magari ya mfanyabiashara huyo.

J4 alitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ya Ali Abeid na Claude Sikarwanda, hukumu iliyotolewa Machi 13, 2020 na Jaji Mfawidhi wa Makahama Kuu Mwanza, Sam Rumanyika.

Hata hivyo Mahakama ya Rufaa ilibatilisha adhabu hiyo na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu Mwanza,iliagiza kesi hiyo jinai namba 131/2017 isikilizwe upya.

Mahakama imemwachia huru leo, baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo. Upande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.

------


Nyie Mahakama acheni kuona watu ni mbuzi, Acheni Rushwa, Rushwa ni adui wa haki, Rushwa anatesa, Rushwa anaumiza watu

Hivi mtu aliyeua watu wawili kwa risasi , watu wamekufa, wamezikwa , na mmemhukumu kunyongwa hadi kufa, leo hiii kisa rufaa, kwamba meza imepinduka? Mpaka aachiwe huru?

Mbona mnakoswa huruma nyinyi?? Mbona hamuwakumbuki watu walowapoteza wapendwa wao? Tunarudi wapi?

Huu ndo utawala wa Rais Samia, wenye kufuata misingi ya Demokrasia?

Haya basi, jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi, mtufufulie ndugu zetu walouawa basi, na sisi tucheze nao, tupige nao stori, likiwashinda hilo, basi tuambiani, walowaua ndugu zetu wawili kwa risasi ni akina nani?.

Mambo ya ajabu kabisa na aibu ilopitiliza.

Mnatanguliza rushwa mpaka kwenye maisha ya watu, kama mlimuhukumu kunyongwa, leo hii inakuaje mnakoswa nia ya kuendelea na kesi? Kwamba hakukutokea tukio la mauaji? Kwamba hamna aliyekufa? Na kama alikufa nani alimuua?? Kama sio Jumanne, ni nani aliwaua?? Kama ni yeye, imekuaje aachiwe huru? Mtufufulie ndugu zetu .


Shame on you!! Rushwa rushwa mpaka mnauza roho za watu??


Wapumbavu kabisa , mlaaniwe na vizazi vyenu, na hizo rushwa mnazokula, pesa hizo ziendelee kuwapa umasikini wa roho na mpoteze heshima mbele ya watu .


Huyu jamaa alihukumiwa hapa !!👇


Leo kaachiwa Huru, ila Polisi wamejifanya kumkamata Tena, ili kupima upepo, ili hali JAMHURI ndio hiyo hiyo Polisi !!

kibatala kaangukia pua na usomi wake hahaaa yule akaendeshe kesi zake zaa michongo za kina halima tu
 
Nimekuuliza sio ugomvi !! Wangapi wanaachiwa ? Kuna mengi mzee na kuwekwa jela kwa mda ni kama sheria hata ukiua jambazi unaweza kushikiliwa kwa muda then ndo unaachiwa.

Fuatilia sana hizo mambo wengine majambazi.
Hoja yako haina mashiko,kwani alivyowaua walikuwa wamevamia nyumbani kwake kuiba?
Kwa sababu hata walioua bila kukusudia pia huwa wanakaa jela angalau miaka 5 kisha mahakama ikija kuthibitisha kuwa haikuwa makusudi ndipo wanaachiwa.
Sasa mtoa mada anauliza wametumia vigezo gani kufutiwa mashtaka na kuachiwa huru?
 
Huyo bwana baada ya mauaji, alihukumiwaga KUNYONGWA Hadi KUFA.

Amekaa Jela wee, mwaka Jana ndo wakaanza habari za Rufaaa zikiingozwa na Kibatala !!.

Leo jamhuri imesema Haina Nia ya kesi, Mahakama imemuachia huru .

Wakati wanatoka tu, Polisi wakawamkata Tena.
Polisi wana nia ya kumfungulia mashitaka upya?
 
Hoja yako haina mashiko,kwani alivyowaua walikuwa wamevamia nyumbani kwake kuiba?
Kwa sababu hata walioua bila kukusudia pia huwa wanakaa jela angalau miaka 5 kisha mahakama ikija kuthibitisha kuwa haikuwa makusudi ndipo wanaachiwa.
Sasa mtoa mada anauliza wametumia vigezo gani kufutiwa mashtaka na kuachiwa huru?
Haya sielewi umeandika nn? Kwa sababu nimeuliza mazingira ambayo jamaa yalimpelekea mpaka akafanya hilo tukio.
 
Hii ndo inajustify mtu kuua?
Kwani kafanyaje? Uzi si unasema kaua watu .

Kwa Mimi naona kawaida wanamalizana sana kweny ishu za madini no kesi.watu wanatolewa mpaka kafara ..Wapo watu kibao wamemalizana kweny ishu za dhuluna.
 
Back
Top Bottom