Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Staki kuongelea hukumu ya court of appeal, wana sababu zao, ila kati ya majaji ambao nawakubali ni mhe Rumanyika, hukumu zake hazinaga wasiwasi, binafdi nilifurahi sana kufanya kazi wakati jaji rumanyika akiwa mfawidhi, ni mtu wa principles siku zingerudi nyuma akarudishwa high court ningefurahi sana ingawa haiwezekani yupo zake CA.
 
Huenda hivi vielim vya sheria , ndivo vinavyowatoa kwenye Ubinadamu .

Kosa ni kosa, jinai ni jinai, jinai ilothibitika haikupaswa kutetewa na mapungufu ya sheria ,ushahidi au mashahidi wenyewe.

Wewe, Umeua mtu.... Nani anayeweza kuthibitisha Dhamira yako ya moyon kua hukuua Kwa kukusudia ??. Mazingira ??.

Inawezekana Sijui sheria, ila Sina huo ujinga wa kushindwa kujua kua hapa Kuna RUSHWA NA UHUNI TU.

Hao ndugu zako inasemekana walikuwa matapeli haswa mwanza inawajua..
Hakuna mtu Ana haki ya kumuua mtu
Huyo J4 asinge waua Wao wangemuua ilikuwa ni kuviziana nani atamuwahi mwingine
 
Majuzi Kati nilikua Kuna Vijana wapatao wanne nmewafikisha Mahakamani


Huwezi amini, Hakimu wa Kesi hiyo, akawa anawapigia simu watuhumiwa anawaambiaje" Huyu Dr kesi yake nyuma yake inawatu wazitk, mkicheza mtapoteaa , Sasa tuongee kiutu uzima".


Fikiria huyo ni Hakimu aliyetakuwa kusimamia haki, ila anataka watuhumiwa, wampe Hela !!.

Ndivyo ilivyo,usitarajie hata siku moja utapata haki mahakamani…
Mwenye pesa ndio Ana haki
 
Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni ya Mabasi ya J4 Express, alidaiwa kuwaua kwa kuwapiga kwa risasi Ally Abeid Mohamed, mkazi wa Igoma na Claud Sikarwanda, mkazi wa Nyasaka Ilemela, Julai 13, 2015, majira ya saa 4:00 usiku, eneo la Nyakato Boma kwenye ofisi na karakana ya magari ya mfanyabiashara huyo.

J4 alitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ya Ali Abeid na Claude Sikarwanda, hukumu iliyotolewa Machi 13, 2020 na Jaji Mfawidhi wa Makahama Kuu Mwanza, Sam Rumanyika.

Hata hivyo Mahakama ya Rufaa ilibatilisha adhabu hiyo na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu Mwanza,iliagiza kesi hiyo jinai namba 131/2017 isikilizwe upya.

Mahakama imemwachia huru leo, baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo. Upande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.

------


Nyie Mahakama acheni kuona watu ni mbuzi, Acheni Rushwa, Rushwa ni adui wa haki, Rushwa anatesa, Rushwa anaumiza watu

Hivi mtu aliyeua watu wawili kwa risasi , watu wamekufa, wamezikwa , na mmemhukumu kunyongwa hadi kufa, leo hiii kisa rufaa, kwamba meza imepinduka? Mpaka aachiwe huru?

Mbona mnakoswa huruma nyinyi?? Mbona hamuwakumbuki watu walowapoteza wapendwa wao? Tunarudi wapi?

Huu ndo utawala wa Rais Samia, wenye kufuata misingi ya Demokrasia?

Haya basi, jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi, mtufufulie ndugu zetu walouawa basi, na sisi tucheze nao, tupige nao stori, likiwashinda hilo, basi tuambiani, walowaua ndugu zetu wawili kwa risasi ni akina nani?.

Mambo ya ajabu kabisa na aibu ilopitiliza.

Mnatanguliza rushwa mpaka kwenye maisha ya watu, kama mlimuhukumu kunyongwa, leo hii inakuaje mnakoswa nia ya kuendelea na kesi? Kwamba hakukutokea tukio la mauaji? Kwamba hamna aliyekufa? Na kama alikufa nani alimuua?? Kama sio Jumanne, ni nani aliwaua?? Kama ni yeye, imekuaje aachiwe huru? Mtufufulie ndugu zetu .


Shame on you!! Rushwa rushwa mpaka mnauza roho za watu??


Wapumbavu kabisa , mlaaniwe na vizazi vyenu, na hizo rushwa mnazokula, pesa hizo ziendelee kuwapa umasikini wa roho na mpoteze heshima mbele ya watu .


Huyu jamaa alihukumiwa hapa !!👇


Leo kaachiwa Huru, ila Polisi wamejifanya kumkamata Tena, ili kupima upepo, ili hali JAMHURI ndio hiyo hiyo Polisi !!

Hili halikubaliki na kiufupi mwenye Pesa awamu hii hawezi fungwa Wala kushtakiwa.

This is bad
 
Marehemu walimuuzia mzigo wenye carat/quality ndogo wa dhahabu, wakalipwa %, fedha nyingine zikabaki, jamqa kuupeleka sokoni, ndio anagundua tayari ameshawalipa jamaa ela nyingi.

Jamaa nao wanaendelea kumdai, yeye hataki walipa tena fedha iliyobaki maana mzigo quality ilikuwa ndogo. Majibizano ndio hadi kuwaua.
Sasa hii inahalalisha vipi muuaji kuwa huru?
 
wachukur sheria mikononi tu kama serikali imeshindwa kufanya kazi yake, simple.
Ndio maana Ndumba Ni muhimu San kulipa kisasa..

Haki ya Mungu hata Mimi ikinikuta nalipa kisasi Cha radi asambaratike ili iwe onyo kwa wengine maana Kama huna Pesa utaonewa.
 
Wekeni hukumu hapa tuone ni mazingira gani jamaa kachomoa pini. Inatokea kabisa mzee mmoja aliachiwa huru baada ya kumchapa shaba askari polisi aliekuja mkamata usiku nyumbani kwake amelala na mke wake. Mzee akawaambia polisi wasithubutu kugusa geti, jamaa wakazama ndani kibabe. Akawachapa risasi mmoja akakata moto pale pale.
Mzee alikomaa kwamba hawakuwa polisi ila majambazi,jamhuri inakazania ni polisi,mzee alipigwa kifungo cha maisha badae akachomoa pini huko huko kwa pilato kwa rufaa. Japo mzee alijua kweli ni askari ila akaamua kuwachapa shaba kibabe!
Sawa Ila kwa kuvamiwa usiku it makes sense..
 
Hi kesi Mahakama ya Rufaa iliamuru ianze upya. Sasa nadhani kwenye process za kuanza nadhani Kuna mazungumzo yalifanyika baina ya mtuhumiwa na familia ya Marehemu wote ndipo wakakubalina fidia, ndio maana kesi imeisha haijafunguliwa Tena.
This makes sense kwamba wamemalizana nje Jambo ambako Ni sahihi kisheria
 
Rushwa inaanzia polisi! Kwenye kesi hizi za mauaji wakishalamba rushwa wanavuruga sana ushahidi. Tangu wamevuruga kesi ya kuuawa kwa dadangu sina hamu kabisa! Ushahidi ulikuwa wazi kabisa mpaka simu waliikamata yenye mawasiliano ya kuua na mtuhumiwa walipomkamata alikiri kuua. Sasa jamaa amewekwa ndani muda wa miaka minne huku nyuma polisi wakavuruga ushahidi wote hata haya maelezo wameyaficha mpaka mtuhumiwa amekuja kuachiwa! IPO siku nitashughulika na mmoja mmoja! Kila nitakapommaliza mmoja nitasema bado mmoja mpaka waishe! Polisi pumbavu kabisa!
Unawajua? Maana wanahamishwa hao afu inakuwa Ni pannel,tafuta mmja ndio awe wa mfano.
 
Sometime haya mambo yanafkrisha Sana , J4 tangu afungwe gari zake zote hazionekan barabarani , watu wengi wamelost ajira , ni kweli Kaua watu wawili , sasa mnaenda kumuua tena na yeye , Hz ni hesabu mbovu , Bora arud watu wapate ajira maisha yaendelee...!!
Huu mzaha hata Kama Sina hela nitakutafuta kwa Ndumba mzee unless iwe muuaji ame kompromise na familia wakamalizana sio kuhonga mapolisi afu wenye ndugu wakaachwa pembeni.
 
Alikusudia kuuwa!! Ina maana alikuwa na akili timamu! Huyo sio wa kuachia. Labda waliomuachia ni hawa wa vyeti fake
 
“Justice must not only be done, but must also be seen to be done”. This dictum was laid down by Lord Hewart, the then Lord Chief Justice of England in the case of Rex v. Sussex Justices, [1924] 1 KB 256.

Watu wakiendelea kukosa Imani na Mahakama ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi...
 
Back
Top Bottom