Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Ukali wake ndio ulikuwa unaingilia majukumu ya mihimili mingine.

Kila muhimili unapaswa kuwa huru usiingiliwe na mwingine.
Kwa hiyo na wwe umekubali kua kila muhimili ule kwa urefu wa kamba yake siyo!? Hakuna kuingiliana kwenye ulaji haya twendeni hadi tuone mwisho wake itakuwaje!!
 
Boss usiilaumu mahakama kumbuka mahakama inafata ushahidi na utetezi na mwenendo wa kesi kama mwendesha mashtaka akishindwa kuithibitishia mahakama au vifungu vya sheria visipofatwa MTU anatoka tu

Mahakama ya Rufaa iliamuru kesi ianze upya. Nadhani hapi ndipo pesa ilipenyezwa.
 
Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni ya Mabasi ya J4 Express, alidaiwa kuwaua kwa kuwapiga kwa risasi Ally Abeid Mohamed, mkazi wa Igoma na Claud Sikarwanda, mkazi wa Nyasaka Ilemela, Julai 13, 2015, majira ya saa 4:00 usiku, eneo la Nyakato Boma kwenye ofisi na karakana ya magari ya mfanyabiashara huyo.

J4 alitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ya Ali Abeid na Claude Sikarwanda, hukumu iliyotolewa Machi 13, 2020 na Jaji Mfawidhi wa Makahama Kuu Mwanza, Sam Rumanyika.

Hata hivyo Mahakama ya Rufaa ilibatilisha adhabu hiyo na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu Mwanza,iliagiza kesi hiyo jinai namba 131/2017 isikilizwe upya.

Mahakama imemwachia huru leo, baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo. Upande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.

------


Nyie Mahakama acheni kuona watu ni mbuzi, Acheni Rushwa, Rushwa ni adui wa haki, Rushwa anatesa, Rushwa anaumiza watu

Hivi mtu aliyeua watu wawili kwa risasi , watu wamekufa, wamezikwa , na mmemhukumu kunyongwa hadi kufa, leo hiii kisa rufaa, kwamba meza imepinduka? Mpaka aachiwe huru?

Mbona mnakoswa huruma nyinyi?? Mbona hamuwakumbuki watu walowapoteza wapendwa wao? Tunarudi wapi?

Huu ndo utawala wa Rais Samia, wenye kufuata misingi ya Demokrasia?

Haya basi, jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi, mtufufulie ndugu zetu walouawa basi, na sisi tucheze nao, tupige nao stori, likiwashinda hilo, basi tuambiani, walowaua ndugu zetu wawili kwa risasi ni akina nani?.

Mambo ya ajabu kabisa na aibu ilopitiliza.

Mnatanguliza rushwa mpaka kwenye maisha ya watu, kama mlimuhukumu kunyongwa, leo hii inakuaje mnakoswa nia ya kuendelea na kesi? Kwamba hakukutokea tukio la mauaji? Kwamba hamna aliyekufa? Na kama alikufa nani alimuua?? Kama sio Jumanne, ni nani aliwaua?? Kama ni yeye, imekuaje aachiwe huru? Mtufufulie ndugu zetu .


Shame on you!! Rushwa rushwa mpaka mnauza roho za watu??


Wapumbavu kabisa , mlaaniwe na vizazi vyenu, na hizo rushwa mnazokula, pesa hizo ziendelee kuwapa umasikini wa roho na mpoteze heshima mbele ya watu .


Huyu jamaa alihukumiwa hapa !!👇


Leo kaachiwa Huru, ila Polisi wamejifanya kumkamata Tena, ili kupima upepo, ili hali JAMHURI ndio hiyo hiyo Polisi !!

Tutakutana kwa mungu 😭😭
 
Hakuna Cha scenario aliwalamba risasi wote wawili kisa wanamcheleweshea Deni lake.
Pesa inatafutwa kwamambo mengi haiwezekani uchukue pesa zangu alafu usumbue kurudisha kisa kuna sheria jamaa alifanya Jambo sahihi kwawakati sahihi
 
Wewe ni bure kabisa. Siyo kila kuua kunafanya mtu anyongwe au hata afungwe. Kuna watu wanaua na kuiachiwa, tena wengi tu. Inategemea na mazingira yaliyofanya waue. Kosa lako kubwa wewe unalaani bila kuonyesha marehemu waliuawa kwenye mazingira gani na ni kwa nini. Inawezekana kweli kuwa kuna rushwa imetumika lakini uandishi wako na uking'ang'anizi wako wa kusema kuua ni kuua tu bila kujali mazingira ndiyo kunakuangusha.

Hi kesi Mahakama ya Rufaa iliamuru ianze upya. Sasa nadhani kwenye process za kuanza nadhani Kuna mazungumzo yalifanyika baina ya mtuhumiwa na familia ya Marehemu wote ndipo wakakubalina fidia, ndio maana kesi imeisha haijafunguliwa Tena.
 
Hapana siyo Rufaa. Mahakama ya Rufaa iliamuru kesi ianze upya mahakama kuu . Sasa serikali imesema haina nia ya kuendelea na kesi

Amekata rufaa kaachiliwa.
Wajinga wanaanza ropoka kuwa rushwa
.
 
PUNGUZA UPEPO
HIZI NI ZAMA NYINGINE.

Alihukumiwa kwenye utawala gani?
Unatambua mazingira ya kosa lake?
Unatambua maisha ya wafanyabiashara wa level zake yalikuwaje wakati huo?
Manji UNAMKUMBUKA?
Mo unamkumbua?
Super shem yuko wapi?

Maisha hayako ivo rafiki yangu.

Hivi super shem alienda wapi?
 
BADO SIJAELEWA

Mshtakiwa - at this point muuaji, msubiri kunyongwa, condemned, kijela jela KONDEM - kakata rufaa.

Ina maana kesi anaeileta mahakamani ni KONDEM

Serikali itasemaje haina nia ya kuendelea na kesi, wakati kesi kaianzisha KONDEM ????

Alishaleta Rufaa , mahakam ya Rufaa ikaamua kuwa kesi ianze upya mahakama kuui. Sasa kwenye process ya kuanza kesi Mahakama kuu, DPP kasema Hana nia ya kuendelea na kesi.
 
Sasa kama imeamuliwa kuwa kesi ianze kusikilizwa upya kutokana na kasoro zilizo onekana tatizo liko wapi? hakuna cha rushwa wala harufu ya rushwa.

ila kama hakuwa na hatia basi ni bora angeachiwa tu huru, kwa nini ateseke tena kuanza kusikiliza kesi upya kwa uzembe wa upande mwengine?!

Nadhani kwa kesi yake sio first degree murder Bali Manslaughter
 
Kama alishahukumiwa basi inamaanisha kesi ilishaisha. Na kama kesi ilishaisha basi mwendesha mashtaka hawezi kusema tena ''hana nia ya kuendelea na kesi''. Inaonekana alikata rufaa na akashinda lakini siyo kweli kuwa mwendesha mashtaka amesema hana nia ya kuendelea na mshtaka.

Mahakama ya Rufaa iliamuru tria de novo kwenye mahakama kuu. Sasa DPP kaona usumbufu kuanza kesi upya kaamua kutoa nolle prosequi.
 
Back
Top Bottom