Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Jamaa baada ya kugundua Mambo yameumana aliwaita ndg wa marehem akawaambia nawapa 600M kila mmoja afu huku serikalini niachieni Mimi ntamaliza!! Ndg wa marehem wakakomaa asulubiwe asulubiwe
Kuchukua hela ya ndugu aliyeuawa inahitaji moyo haswaa
 
Hujawahi kupata Kesi hivyo ni vema utulie,katika watu ambao HAWAWAPENDI MAWAKILI wa kujitegemea kama hao kina Kibatala ni Askari Polisi,mfano katika wale Askari wanaotuhumiwa kumuua kijana wa Madini Mtwara,kuna rafiki zangu wawili tena ni Senior Officers miongoni mwa wale 7 na walikuwa wanawachukia sana MAWAKILI WA KUJITEGEMEA,lakini tangu wakamatwe na kuwekwa Mahabusu sasa hivi ndugu huku nje wanahaha kutafuta Wakili mzuri wa kujitegemea ili awatetee Mahakamani,hivyo fanya jambo lolote lakini Jela ni mahali pabaya asikwambie mtu,wewe unadhani Sabaya alikuwa anawapenda MAWAKILI WA KUJITEGEMEA enzi alipokuwa DC??si alikuwa anawaona takataka tu,lakini leo hii Mpira umegeuka yeye ndie anawategemea MAWAKILI WA KUJITEGEMEA,acha masihara ya Jela ndugu
Mawakili ni wazuri sana na ndo maana kuna watu hulipa pesa za kila mwezi kwenye kampuni za mawakili ili ikitokea lolote lifanyiwe kazi. Kuliko kupata tatizo afu ndo uanze tafuta wakili
 
Hujaelewa Point yangu ndugu, huyo jamaa inasadikika alifanya tukio hilo wenyeji wa Mwanza tunafahamu, mazingira ya kesi na mwenendo unatia shaka.

Njoo Mwanza Leo uulize habari zake halafu kama utarudia kuandika hapa wewe ndio unatakiwa utulie .
Akiwa ndani unafaidika na nini?

Akiwa nje unakosa nini?
 
Sababu ya Pili ni kwamba Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 38 inaruhusu Mkuu wa Kituo cha Polisi kufanya UPEKUZI,lakini akiwa na udhuru SHERIA inamruhusu kumteua Askari mwingine na kumpa RUHUSA YA MAANDISHI kwenda kufanya Upekuzi nyumbani kwa Mtuhumiwa,lakini Askari wote walioenda kufanya Upekuzi nyumbani kwa hao watuhumiwa hakukuwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi yeyote,na pia hao walioenda hawakuwa na Ruhusa ya Maandishi kutoka kwa Mkuu wa Kituo,hilo tayari ni kuvunja SHERIA hivyo Majaji wakaawaachia huru wale jamaa,hivyo kikubwa ni kucheza na SHERIA tu na si vinginevyo
Nakuelewa na pia Nafahamu Sheria , unachoeleza hakinatofauti

MTU KUPATA AJALI AU KUPIGWA NA KUUMIZWA HALAFU AKIPELEKWA HOSPITAL HAPATI MATIBABU MPAKA IPATIKANE PF3 .

SHERIA ZETU NI MBOVU. MLOLONGO MREFU USIO NA MAANA
 
Kinachoumiza kwenye kesi kama hizi, mawakili wenye weledi wanaenda kutetea wahalifu .

Hilo ndio tatizo langu na kibatala, japo ni wakili mzuri njaa zinafanya wakili unaenda kutetea wezi na wauwaji .
Hakuna wakili anayekataa kesi inayompa hela
 
Nimekuuliza sio ugomvi !! Wangapi wanaachiwa ? Kuna mengi mzee na kuwekwa jela kwa mda ni kama sheria hata ukiua jambazi unaweza kushikiliwa kwa muda then ndo unaachiwa.

Fuatilia sana hizo mambo wengine majambazi.
Wale walikuwa wafanyakazi wake
 
Majaji wakasema taratibu za Upekuzi NYUMBANI kwa hao watuhumiwa hazikufuatwa kama CPA inavyoelekeza,kwanza Upekuzi uliofanywa na Polisi Nyumbani kwa watuhumiwa Tegeta ulifanyika USIKU badala ya Mchana,hilo lilikuwa Kosa la kwanza,Upekuzi NYUMBANI kwa Mtuhumiwa SHERIA inaelekeza ufanyika wakati wa jua kutoka na jua kuzama na sio USIKU,kama ni USIKU basi Askari ni lazima wawe na KIBALI CHA MAHAKAMA kuwaruhusu kufanya Upekuzi Usiku,na Askari waliowapekua hawakuwa na Kibali cha Mahakama cha kuwaruhusu kufanya Upekuzi Usiku,hio ilikuwa sababu ya kwanza ya kuwaachia huru
Pitia proceedings za hiyo case, alafu njoo utupe maamuzi yako tuachane na hizo reference kuwa kama unatoa elimu kwa layman. Maana court of appeal wao wameangalia sheria ya CPA inasemaje.
 
Back
Top Bottom