Mwanza: Mwanamke amuua mama mkwe wake kwa sumu

Mama walahi
 
Kwa hiyo watoto wamemchoma mama, siyo kawaida hii..........ila jamaa naye aliamua kupuuzia warning za wife, angetafuta hata housegirl wa kuwa anamwangalia mama yake na kumweka chumba hata cha uani, hawa wanawake huwa wanatutaka tupende wazazi na ndugu zao baaasi, ila wa kwetu wanawaona kama nuksi vile, watawazulia hili, mara lile ili mradi taabu tu........wanawake jaribuni kuwa na ustahimilivu kwa ndugu wa mume.
 
Imani mkuu waislaam wamejazwa imani ya Dini kwamba kuua au kujiua ni dhambi kubwa
 
Yaani mkuu unamuweka mama yako mzazi aliyekuzaa chumba cha uani?
Mama yako ambaye amekulea na kukuza kwa nguvu zote?
Sababu ya kamwanamke kamoja tu ulichokutana nacho ukubwani?

Huyo mwanamke anatakiwa afe kifo kibaya cha kimya'kimya hakuna excuse ya kuhalalisha mauaji ya mzazi tena mzazi mwenyewe ni mama.
Ni wajibu wa kila mwanaume kumlinda mama yake kwa kila njia, huyo jamaa angekuwa anajitambua basi huyo mwanamke angeachana nae kitambo sio binadamu huyo.

Lakini ni vizuri zaidi kuwajengea wazazi nyumba yao na kuwawekea wafanyakazi wa kutosha ili wasipate shida kama hizi kutoka kwa baadhi ya mashetani kama hawa.
 
Tuliwaona wazee wetu zamani wajinga kuoa/kuolewa kwenye mikoa yetu ya asili na maeneo yetu ya asili.

Hii iliweka heshima kwa sababu kadhaa;

1. Undani wa muoaji/muolewaji ulijulikana. Kama kuna dosari yeyote ya kitabia ama kimaadili ni rahisi kujulikana.

2. Kutokana wote kutokea sehemu moja, kulifanya kila mmoja katika ndoa kumchukulia mzazi wa mwenzie kama mzazi wake pia. Maana walishajuana toka zamani.

3. Kwa kuwa wote mmetoka sehemu moja, hakuna mambo ya kutishiana kwenda mkoani kwetu. Wote njia moja.

4. Kubwa zaidi la yote, ndoa hazikuruka kipengele chochote. Watu walichumbiana kupitia washenga, harusi zilipangwa kwa maadili ya kiimani na kiroho. Kupelekea ndoa yenye mizizi imara.

Sasa leo hii mtu katoka Kigoma anaoa mtu wa Mtwara. Mila tofauti, mikoa tofauti hata machimbuko tofauti. Na mbaya zaidi wanaokotana wenyewe bila kushirikisha wazazi. Wakwe wanakutana siku ya harusi. Kwa vyovyote hakutokuwa na 'bond' baina ya wazazi wakwe na wakwe zao.
 
Mke alishamkataa Mama mkwe wake jamaa akaendelea kuwa nae.kwa hiyo ajilaumu yeye mwenyewe kwa uzembe wake.
 
So sad 4 sure
 
Yaan ni ukatili wa hali ya juu mama wa mume ni sawa na mama mzazi kabisa kaka ilitakiwa mke ajishushe tu ampotezee na amjali maana watu wakizeeka ni wasumbufu unamchukulia kama mtoto tu
Sasa hapo mume hatompenda tena
Kaharibu maisha yake kwa hasira
Dah.....jela inamuhusu 🤭
 
Imani mkuu waislaam wamejazwa imani ya Dini kwamba kuua au kujiua ni dhambi kubwa
Mkuu Hivi Iraq, Afghanistan, Somalia , Sudan nk Ni watu wa Imani gani wanaishi nchi hizo? Mbona kila siku nasikia mauaji huko?
 
Mkuu, wazungu kwa kutambua kwamba vijana wanapooa wanatakiwa kuwa huru na wenza wao na watoto watakaopata, wakaanzisha utaratibu wa makazi ya wazee........kwa sisi huduma za social security bado hazina nguvu kuweza kuanzisha huu utaratibu na pia kutokana na tamaduni zetu, lakini ukweli ni kwamba siyo mara zote watu wanakuwa na uvumilivu kukaa na members from extended family ukichukulia na maneno maneno ambayo yanaweza kupelekea hata wanafamilia hasa mke na mume kutoelewana sababu ya ndugu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…