Tuliwaona wazee wetu zamani wajinga kuoa/kuolewa kwenye mikoa yetu ya asili na maeneo yetu ya asili.
Hii iliweka heshima kwa sababu kadhaa;
1. Undani wa muoaji/muolewaji ulijulikana. Kama kuna dosari yeyote ya kitabia ama kimaadili ni rahisi kujulikana.
2. Kutokana wote kutokea sehemu moja, kulifanya kila mmoja katika ndoa kumchukulia mzazi wa mwenzie kama mzazi wake pia. Maana walishajuana toka zamani.
3. Kwa kuwa wote mmetoka sehemu moja, hakuna mambo ya kutishiana kwenda mkoani kwetu. Wote njia moja.
4. Kubwa zaidi la yote, ndoa hazikuruka kipengele chochote. Watu walichumbiana kupitia washenga, harusi zilipangwa kwa maadili ya kiimani na kiroho. Kupelekea ndoa yenye mizizi imara.
Sasa leo hii mtu katoka Kigoma anaoa mtu wa Mtwara. Mila tofauti, mikoa tofauti hata machimbuko tofauti. Na mbaya zaidi wanaokotana wenyewe bila kushirikisha wazazi. Wakwe wanakutana siku ya harusi. Kwa vyovyote hakutokuwa na 'bond' baina ya wazazi wakwe na wakwe zao.