Mwanza: Mwanamke amuua mama mkwe wake kwa sumu

Mwanza: Mwanamke amuua mama mkwe wake kwa sumu

Kuna mwingine alikuwa anafunga milango yote anamwacha mama mkwe anapata baridi,jua na mvua nje mpaka anaporudi jion
 
Mauaji meengi yanayotokea yanaonyesha Watanzania wengi wanaakili finyu sana,
kuua ni dhambi kwa mujibu wa imani za kidini na ni kinyume cha sheria lakini hawa wauaji wengi wanatoa taswira za akili zetu watanzania wengi.....wanaua kijinga kiasi kwamba wala huumizi kichwa kujua nani muuaji..
 
Kuna mwingine alikuwa anafunga milango yote anamwacha mama mkwe anapata baridi,jua na mvua nje mpaka anaporudi jion

Hiz ni roho mbaya sana ingekuwa mama ake yeye anafanyiwa hivyo ingekuwaje jmn
 
Wanawake wengi wakiingia kwenye ndoa na mtu mwenye mali wanaanza ushirikina hayo yote ili umsikilize kila anachokwambia anakufanya anavyotaka.
Wacha tuwagegede tuu na kutupa kule...hamna kiweka ndani hawa utakufa kwa presha bure
 
Mkuu, ukitaka twende kwa mtindo huo nitakuambia ndoa ni ya wanandoa. Serikali jukumu lake ni kuzisajili tu. So hata wanandoa wakishindwana serikali haiwalazimishi kuendelea kuishi pamoja. Wanandoa wakiachana serikali itasajili tu ile talaka.
By the way kuna kifungu chochote katika Law of Marriage Act kinachosema ndoa ni ya serikali? Or any case law to that effect?
Hata kama hamuishi pamoja bado ni mkeo/mmeo, huwezi ukaoa/kuolewa bila idhini ya Serikali(Mahakama), short of that one part ana haki ya kukushitaki!
 
Kwa hiyo watoto wamemchoma mama, siyo kawaida hii..........ila jamaa naye aliamua kupuuzia warning za wife, angetafuta hata housegirl wa kuwa anamwangalia mama yake na kumweka chumba hata cha uani, hawa wanawake huwa wanatutaka tupende wazazi na ndugu zao baaasi, ila wa kwetu wanawaona kama nuksi vile, watawazulia hili, mara lile ili mradi taabu tu........wanawake jaribuni kuwa na ustahimilivu kwa ndugu wa mume.
Kwahiyo angemfukuza mama yake sababu ya mwanamke?
 
Yaani mkuu unamuweka mama yako mzazi aliyekuzaa chumba cha uani?
Mama yako ambaye amekulea na kukuza kwa nguvu zote?
Sababu ya kamwanamke kamoja tu ulichokutana nacho ukubwani?

Huyo mwanamke anatakiwa afe kifo kibaya cha kimya'kimya hakuna excuse ya kuhalalisha mauaji ya mzazi tena mzazi mwenyewe ni mama.
Ni wajibu wa kila mwanaume kumlinda mama yake kwa kila njia, huyo jamaa angekuwa anajitambua basi huyo mwanamke angeachana nae kitambo sio binadamu huyo.

Lakini ni vizuri zaidi kuwajengea wazazi nyumba yao na kuwawekea wafanyakazi wa kutosha ili wasipate shida kama hizi kutoka kwa baadhi ya mashetani kama hawa.
nimeshangaa haswaa
 
Hata kama hamuishi pamoja bado ni mkeo/mmeo, huwezi ukaoa/kuolewa bila idhini ya Serikali(Mahakama), short of that one part ana haki ya kukushitaki!
Mkuu, haya maelezo yako yana basis ya Kisheria au ni just your opinion? Kwamba bila idhini ya serikali (mahakama) hakuna kuoa au kuolewa?
Naomba niendelee kujifunza kutoka kwako
 
Kumuuwa huyo mama ni sawa na kumuuwa bwana wake. Akumbuke bila huyo mama hangempata huyo bwana. Ni ushetani wa kutisha, sheria ichukuwe mkondo wake.
 
Jeshi la polisi linamshikilia mwanadada NEEMA MWAMBUSI USWEGE(29) mkoani Mwanza kwa kosa la kumlisha mama mkwe wake sumu kwenye chakula na kumsababishia umauti.

Inadaiwa kuwa mama wa JAMES BULAYA (38) bi ANETH MANYIRIZU umemkuta umauti huo tarehe 13/1/2022 saa 12:00 mchana alipopelekwa hospitali baada ya kutapika damu nyingi nakupoteza uhai, bi ANETH MANYIRIZU amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 katika hosipitali inayodaiwa siyo ya Serikali.

Hata hvyo uchunguzi wa polisi umethibitisha kuwa NEEMA MWAMBUSI USWEGE ndiye muhusika mkuu kwani watoto wake walitoa maelezo kuwa mama ndiye alimpikia chakula bibi yao na kuwakataza wasije wakathubutu kula chakula kile.

Watu wa jirani wametoa maelezo kuwa ugomvi wao na mumewe ulikuwa ukijirudia mara kwa mara huku mwanamke alikuwa akimjibu mumewe kuwa yeye kwake siyo kituo cha kulelea wazee tofauti na hivyo atarudi kwao Mbeya.

Bwana JAMES ni mfanyabishara mkubwa wa dagaa tz na nje ya nchi amesikitishwa kwa tukio hilo la kufiwa mama yake ambaye ndiye mzazi pekee aliyekuwa amebaki


Kumchukia mamamkwe, kugombana na mamamkwe, kumtesa mamamkwe hadi kufikia kumuua ni ushetani mwingine ambao shetani mwenyewe anamtumia mke kumchukia mama ambaye bila yeye asingempata huyo mume.
Mungu tunusuru na vizazi vyetu

Lala salama mama Aneth
 
Ndiyo. Ndiyo maana unapoandikisha ndoa lazima upite muda kwanza ili kujiridhisha(pasiwepo malalamishi mmoja wenu ni mume/mke wa mtu mwingine) iwapo hiyo ndao ni halali au batili!
 
Kwa sisi tulio na umri mkubwa humu, na kwa wengine pia kwani panapo majaliwa pia watafikia uzee - tupate funzo hapa.

Mimi binafsi sipendi na sitapenda kuhamia kwa mtoto wangu yeyote. Nitabaki kwangu. Nafahamu zaweza kujitokeza changamoto za kiafya, lakini kuhamia kwa watoto labda iwe sina kauli. Wanihudumie watakavyoweza nikiwa kwangu au hospitali.

Sina mashaka na mkwe wangu yeyote - ila hayo ndio mapenzi yangu.
 
Dunia imevurugwa
Miaka 79 unamuua wa nini wakati hapo kabakiza masaa kadhaa tu??
Mwache akaozee jela ndiyo atajua hajui,Bibi wa umri huo kwanza hata hawasumbui kabisa zaidi ya kumwekea uangalizi mzuri tu,na inaonekana uwezo upo,basi angemwekea dada maalumu wa kumwangalia kama yeye Neema alikuwa anaona taabu.Butimba ndio yashakuwa makao yake ya kudumu,akibahatika kutoka si chini ya 10yrs,wakati huo unakuta na Mume alishaoa,ndoa hakuna unarudi kwenu Mbeya mikono mitupu.
 
Kwa hiyo watoto wamemchoma mama, siyo kawaida hii..........ila jamaa naye aliamua kupuuzia warning za wife, angetafuta hata housegirl wa kuwa anamwangalia mama yake na kumweka chumba hata cha uani, hawa wanawake huwa wanatutaka tupende wazazi na ndugu zao baaasi, ila wa kwetu wanawaona kama nuksi vile, watawazulia hili, mara lile ili mradi taabu tu........wanawake jaribuni kuwa na ustahimilivu kwa ndugu wa mume.
Umuhamishie Mama Mzazi chumba cha uani kisa Mke wako hamtaki😳
 
Back
Top Bottom