Mwanza: Mwanamke amuua mama mkwe wake kwa sumu

Pana changamoto zingine hasa za kiafya zitakulazimu tu ukakae kwa watoto upate uangalizi maalumu na wa karibu.Muhimu ni kumwomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe na uzee usiyo na changamoto hasa za ki afya,hapo ndiyo utaweza kukaa nyumbani kwako chini ya uangalizi wao.
 
Tutakuchukua tu
 
Yaani iwe hakuna jinsi!
 
mkuu shida mabinti wa kichaga weupe tunataka kuchanganya rangi
 
Kumchukia mamamkwe, kugombana na mamamkwe, kumtesa mamamkwe hadi kufikia kumuua ni ushetani mwingine ambao shetani mwenyewe anamtumia mke kumchukia mama ambaye bila yeye asingempata huyo mume.
Mungu tunusuru na vizazi vyetu

Lala salama mama Aneth
Hatari sana
 
Da Nyamizi waambieni kaka zenu wwche uzoba kwenye mapenzi..wakipenda wanakua malofa sana!!yanathamini mke kuliko mama!wakishafiniyiwa kwa ndani wanaona mzazi hana maana!huyo ngosha alipaswa afukuze huyo mke kabla

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Umuhamishie Mama Mzazi chumba cha uani kisa Mke wako hamtaki😳
Utafanyaje sasa, wewe utamwamishia mkeo uani...siyo? uani siyo kwamba ni chooni.......ni nyumba separate kwa hiyo ina sifa zote kama nyumba kubwa. Ukiambiwa kwamba wazungu hupeleka wazazi wao wakishazeeka kutunzwa nyumba za wazee mbali na makazi yao unaweza kuzimia?
 
Kwahiyo angemfukuza mama yake sababu ya mwanamke?
Siyo kumfukuza, anamwekea utaratibu mzuri wa makazi ili aweze kuwa huru na mke wake........au kama vipi amwamishie mke wake nyumba ya uani akae na mama yake nyumba kubwa, hapo vipi?
 
Hili nalo neno mdogo wangu,hawa Kaka zetu akili zote wanawakabidhi Wake zao na hasa akikutana na mjanja wa yale mambo ya Chumbani,matokeo yake ndiyo haya.Ukisoma maelezo ya Mwanaume hapo juu unaona kabisa ile warning aliyokuwa anapewa wala hakujali,na imagine maisha ya huyo Bibi yalikuwaje hasa wakati mtoto wake hayupo,si ajabu alikuwa anapewa chakula mara moja tu kwa siku na siku hiyo Neema akaamua kummaliza Bibi wa watu 😒
 
Hakuna cha kuzimia hapa,au unadhani sijui kuwa Wazungu wana huo utaratibu πŸ˜…? Lakini pia siyo Wazungu wote wanawapeleka hao Wazee kwa hizo nyumba,a good number of them wanawalea Wazazi wao mpaka mwisho wa uhai wao.Huwezi kumtenga Mzazi wako tena wa miaka 79 kisa Mke hamtaki,kwangu Mimi utachagua moja,unataka Ndoa utamlea Mama,hutaki fungasha virago vyako.
 
Mkuu hizi sound zisije zikawa ni nyuma ya keyboard, tukikupeleka um face shemeji unakuwa mdogo kama piriton.......hapa ndo ule msemo wa "za kuambiwa changanya na zako" unapotamalaki......kuna wale wazungu wanao opt kuendelea kuishi kwenye nyumba zao walizojenga hadi wanafika miaka 80 na zaidi hivyo hivyo kibishibishi huku watoto wao wako na maisha yao huko na pengine wameshahama eneo au nchi. Binafsi nilipokuwa majuu nilipanga nyumba ya bibi wa kizungu ambaye alikuwa ana zaidi ya miaka 80, alikuwa anajipikia, kwenda supermarket na kujifanyia kila kitu kwani hakuwa na mtu yoyote wa kumsaidia. Kijana wake alikuwa akimtembelea mara moja moja na alikuwa anaishi jimbo tofauti kabisa. Kwa hiyo tulikuwa vijana wawili ambao alitupangisha ndo akawa angalau kapata kampani ya watu wa kuishi nao, otherwise angeendelea kuishi peke yake........​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…