Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Umaarufu huo utawafikisha wapi akina Mbowe? Walikuwepo akina Lisu wakatengenezewa na majukwaa Ulaya na USA saizi wako wapi? Ccm si bado iko ulingoni?

Ukiwaacha watahamia nje wewe pimbi lazima wadhibitiwe mapema.
Ungetakiwa useme magufuli ndo Yuko wapi na sio lisu ambaye yupo na buheri wa afya
 
View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
Walianza kumbeep mama, sasa ameanza kuwapigia. Hawa watu siyo wa kucheka noa, la sivyo nchi utakuwa ya maandamano na harakati kila kukicha. Walisema watamnyoa mama, sasa ngoja awanyoe wao
 
Wananchi wana mahitaji yao ndio maana wakiguswa wanalalamika lakini madai ya Chadema sio ya wananchi
Eti uñasema nini wewe?

Kwamba;

å Wananchi wana mahitaji yao (SAWA)

å Hawa wananchi wakiguswa wanalalamika (SAWA)

HALAFU UMESEMAJE HAPO MWISHONI?

å Ila madai ya CHADEMA siyo ya wananchi...!!

MASWALI KWAKO:

1. Hivi kwa akili yako na kwa kauli yako ya "madai ya CHADEMA si ya wananchi" una maana kwamba "wananchi" kwa mtazamo wako ni serikali au wabunge wa CCM au wana CCM siyo..?

2. Kama unafikiri hivi, basi wewe ni "mjinga" na unastahili kuelimishwa ili ujue "wananchi" ni kina nani...!!

3. Kwani hao CHADEMA ni mawe au miti? Je, si kwamba nao ni wananchi?

4. Kama unakubali kuwa ni "wananchi", basi wanapo launch madai/malalamiko yao juu ya serikali au nchi yao basi wanafanya vile kama wananchi wenye haki zote ktk nchi yao...!

Kwa maelezo haya, utetezi na hoja zako ni irrelevant na hazina maana wala nguvu..
 
Mbona meco alikufa kwa koroona lkn bado watu waliendelea na maisha yao na hukuuliza wala kutoa tahadhali?
Unaonaje jinsi mama anavyowakomesha mataga na sukuma gang?
 
Eti uñasema nini wewe?

Kwamba;

å Wananchi wana mahitaji yao (SAWA)

å Hawa wananchi wakiguswa wanalalamika (SAWA)

HALAFU UMESEMAJE HAPO MWISHONI?

å Ila madai ya CHADEMA siyo ya wananchi...!!

MASWALI KWAKO:

2. Wananchi hao ni kina nani kwani?

3. Kwani hao CHADEMA ni mawe au miti? Je, si kwamba nao ni wananchi?

4. Kama unakubali kuwa ni "wananchi", basi wanapo launch madai/malalamiko yao juu ya serikali au nchi yao basi wanafanya vile kama wananchi wenye haki zote ktk nchi yao...!

Kwa maelezo haya, utetezi na hoja zako ni irrelevant na hazina maana wala nguvu..
Tunaangalia maslahi ya wengi sio wananchi wachache wenye malengo yao ya kisiasa hapo hapana mkikaidi ni nyundo tuu
 
Mmmmm yeye mgeni Mwanza kaenda kwenye mambo ya Katiba sasa afikie wapi wakati wako ki chama wanalipiwa wote ??? Mbona maswali kitoto labisa na yeye huyu eti ni GT
 
Muulize polepole au bashiru majibu wanayo

Nyie washabiki wa ccm ndo mlikua mnaimba ngonjera kwamba mambo ni mazuri amefariki ghafla yamekua mabaya
Pitia comments zangu zote awamu ya tano utajua kama mimi ni ccm au hapana.

Sikuwa nakubaliana na sera za Uchumi za Magu ,hayo ya kisiasa mtajuana wenyewe kwa sasa Madam President kabadili mambo kwangu is okay
 
Wanahusikaje hapa? Relax kunywa maji ya baridi halafu rudi hapa!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Wanahusikaje hapa? Relax kunywa maji ya baridi halafu rudi hapa!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Wanahusikaje hapa? Relax kunywa maji ya baridi halafu rudi hapa!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Wao ndo walikuwa washauri wa dikteta magufuli, kawatesa wakina mbowe na lisu Leo hayupo
 
Weka picha
Namuona ukiwa kazini maana biashara ni matangazo
tapatalk_1549972891359.jpg
 
Back
Top Bottom