Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
Wqsiojulikana Tanzania wamejijulisha wazi ni wakina nani, poly ccm kwa kunyakua viongozi wa chama usiku wa manane kinyemela bila ya kutoa taarifa yeyote. Polisi wa Tanzania kwa vitendo hivi mnaonyesha wazi jinsi mnavyolinda maslahi ya ccm wazi wazi na kuchafua taaswira ya nchi kidemokrasia. Polisi wamekuwa watekaji sasa si walindaji wa usalama wa raia. Wanachama wa vyama nnje ya ccm hawana haki ya uraia kwenye nchi yao. Je hii ni mbinu ya makusudi ya kuchafua serekali ya awamu hii, ili ilaumiwe kama awamu iliopita? Kwa jinsi hii mheshimiwa Lisu na Lema bakini mlipo tz bado usalama wenu si shwari. Wanaojulikana bado wanaendeleza udhalimu wao.
 
Hivi DJ mbona amekuja kasi sana kipindi hiki cha Mama, anamwonea mama! Anamchukulia poa siyo? Mbowe aache vurugu! Nchi inataka amani na mshikamano!
Pole mkuu amekula 0713 yako na umeachwa matenga
 
We have been here before: Magufuli hakuanza na kila mtu, alianza na vyama vya upinzani by then wafanyabiashara na taasisi zingine wakawa wanawaona vyama vya upinzani kama wasumbufu pale walipokuwa wanapinga Magufuli kukanyaga kanyaga katiba, mpaka ilipomfikia kila mtu ndipo jamii ikajua kuwa haipo tena kwenye nchi waliyokuwa wameizoea.Kwa sheria za Tanzania CHADEMA wamevunja sheria gani? Hakuna.
 
Duhhh, katiba ikipitishwa kuna shida!


Mama samia hamujamjua tu vizuri, huyu mama hana shida kuna watu nyuma yake wanafanya kipingamizi. Lau wakimwacha aendeshe nchi yeye kama yeye atafanya mazuri, haki itatawala, atasikiliza maono ya wananchi na kuyafanyia kazi..
 
Kwahiyo hata onesho la Fally Pupa nalo kufutwa sababu ni mkusanyiko usio wa lazima
 
Akili zenu sijui kama mnawaza sawa sawa.

Hata akitoka Samia, mnadhani ndio mwisho wa matatizo ?

Hamjawajua CCM nyie.

Subirini mkiwekewa MWIGULU au MPANGO tena ndio mtaanza kukimbia kama DIGI DIGI.
Wewe ndio mtupu kabisa kichwani kwako,
Wazazi wako wametuletea hasara tu mtaani.
Hivi.hicho wewe unachokiita system Ni Nini? Ni hewa? Hujui system inatengenezwa na watu na inalindwa na watu na watu wenyewe ndio hawa sasa akina Rais?
Hivi wakati Makaburu wanawakandamiza akina Mandela walikua wanakandamizwa na system watu au system hewa?
Nakuuliza wewe kilaza wa CCM.
Kaburu Botha alisumbua akina Mandela alipokua De Klerk akawafungulia akina Mandela sasa hapo walifunguliwa na system watu au system hewa?
Jibu wewe msukule wa CCM.
 
Tunaangalia maslahi ya wengi sio wananchi wachache wenye malengo yao ya kisiasa hapo hapana mkikaidi ni nyundo tuu

Wengi ni wepi?

Usiidanganye nafsi yako. Usiidhulumu ukweli nafsi yako...

Kinachofanyika ktk Tanzania hii ya sasa chini ya serikali na utawala huu hakuna cha "kuangalia maslahi ya wengi" wala nini bali ni kulinda maslahi binafsi ya CCM/watawala wachache na ndugu zao na matumbo yao..

Hili kupitia kwetu sisi wananchi tunaoumizwa, MUNGU MUUMBA hataruhusu lifanyike wala kuendelea. Kama tulivyokataa kwa mwendazake na yeye kupata adhabu yake, ndivyo itakavyokuwa na kwa huyu mwanamke na wengine wajinga watakaokuja mpaka Tanzania itakapokuwa fully liberated...!!

Nyongeza:

Kama unataka kujua kuwa tusiokubaliana na serikali hii haramu ya CCM ni wengi na ndiyo tuliobeba maslahi ya Wengi, basi tuendeleeni na mijadala ya amani, acheni kutumia bunduki na polisi...

Ishara kuwa nyie ni WACHACHE sana na hamna uhalali wowote wa ku - impose jambo lolote likakubalika na WENGI, ni matendo yenu...

Hamna hoja, mnaogopa hoja na mnadhibiti hoja kwa mtutu wa bunduki kwa kutumia polisi kitu ambacho aliyekuwa JIWE a.k.a Mwendazake zake alishindwa na badala kuushinda umma (people's power) aliangushwa na kushindwa yeye...!
 
Back
Top Bottom