Jeshi la Polisi kwa kiasi kikubwa Sana haliaminiki, watu Wana haki ya kutilia mashaka kuhusu taarifa zao wanazotoa kwa sababu nyingi ya taarifa hizo ni za kutengenezwa (fabricated news).
Baada ya kuuawa hao Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi, Askari Polisi waliotekeleza tukio hilo walipaswa kuwaita watu(majirani) pamoja na Waandishi wa Habari muda huo huo ili kuuthibitishia umma juu ya kutoa ushiriiiano wa kutoa taarifa za Wahalifu kwa Jeshi hilo la Polisi kwa lengo la kudhibiti matukio ya Uhalifu Kama hayo yaliyopelekea vifo vya watu hao Watuhumiwa. Kitendo hicho kingesaidia kusababisha Watu/Wananchi pole pole kuanza tena upya kuliamini Jeshi la Polisi juu ya utendaji kazi wao, pia Kitendo hiki kingesaidia kujenga public awareness juu ya UMUHIMU na wajibu wa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu na wahalifu.
Watu wengi Sana wamepoteza kabisa imani dhidi ya Jeshi la Polisi.