Mwanza: Yaliyojiri kwenye kuaga mwili wa Hayati Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Katoro iko wilaya ya Geita siyo Chato
 
Hivi huyu jamaa aliyevaa sijui ni ngozi ameshika ngao anaonyesha maneno fulani kuhusu mwendazake ni nani maana kila sehemu yupo au ni mjumbe wa kamati ya mazishi?
 
Mbona shughuli za kuaga mpendwa wetu hayati JPM leo CCM Kirumba, Zimesimamishwa ghafla na mwili unabebwa kurudishwa kwenye gari?
 
Hiyo ni protocal ya Mazishi ya watu mashuhuri mkuu!! Sisi kwamba Nani anachagua bali Ni Sheria iliyotungwa tangia hapo awali nadhani hata Yeye hayati JPM alikuwa akiifahamu
 
Wadau hivi hili gari maalumu la kubeba mwili wa Rais ni jingine au ni lile lile? Na kama ni lile lile vp limekuja na ndege kutoka Zanzibar au? Naona plate namba hii gari ya mbele ni zile zile za tangu siku ya kwanza Dar.
 
Huyu P.M amini mama atampa nafasi kubwa kwenye serikali yake

Ova
Ya mauaji tena ya wapinzani wa Serikali yake? Maana nasikia huyo jamaa yako alikuwa ni kiongozi wa kile kikundi cha watu wasio julikana. Na ushahidi upo!!

Alivamia kituo cha habari cha Clouds usiku akiwa na Askari! Siku ya kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kesho yake aliibukia Msamvu Morogoro akihusishwa kutokea Dodoma! Tukio la kutekwa Msanii Roma Mkatoliki, aliahidi angepatikana kama ya Jpili! Na kweli ikatokea hivyo!

Mpaka hivi sasa tunapo ongea, amepigwa marufuku kuingia Marekani kwa sababu ya makosa lukuki yakiwemo ya uvunjifu wa Haki za Binadamu, nk. Kiufupi tu, Makonda ni mchafu!

Hapa ni nje na kukwepa kodi kupitia yale Makontena, kufoji cheti chake cha elimu, kunufaika binafsi kupitia kampeni ya madawa ya kulevya! Kabla ya Bosi wake kumteua Mkurugenzi wa kudili na hiyo kampeni, amejawa na dharau, nyodo, sifa, unafiki, majivuno, kiburi, ulevi wa madaraka, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…