Mwanza: Yaliyojiri kwenye kuaga mwili wa Hayati Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Mwanza: Yaliyojiri kwenye kuaga mwili wa Hayati Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Awali ya yote niwape Watanzania wenzangu POLE kwa msiba wa Rais wa JMT Dr JPM.RIP Nimekuwa nikifuatilia taarifa za Watanzania wa maeneo teule wakitoa heshima zao kwa mwili wa Hayati JPM,aliyekuwa Raisi wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nimesikia wana wa Mwanza wakitamka hilo neno la JESHI muda wote,nikafikiri labda ni kwa kuwa Hayati JPM alikuwa Mwanajeshi?Ama kuna jingine?
Kuuliza si ...
 
Wadau hivi hili gari maalumu la kubeba mwili wa Rais ni jingine au ni lile lile? Na kama ni lile lile vp limekuja na ndege kutoka Zanzibar au? Naona plate namba hii gari ya mbele ni zile zile za tangu siku ya kwanza Dar.
hii gari ni nyingine tofauti na ya mwanzo,mwili unapoingia mwanza watangazaji walilitolea ufafanuzi hili suala
 
Hilo ndo jibu pekee kuwa alikuwa kipenzi cha watu na adui wa vibaraka.
 
Ya mauaji tena ya wapinzani wa Serikali yake? Maana nasikia huyo jamaa yako alikuwa ni kiongozi wa kile kikundi cha watu wasio julikana. Na ushahidi upo!!

Alivamia kituo cha habari cha Clouds usiku akiwa na Askari! Siku ya kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kesho yake aliibukia Msamvu Morogoro akihusishwa kutokea Dodoma! Tukio la kutekwa Msanii Roma Mkatoliki, aliahidi angepatikana kama ya Jpili! Na kweli ikatokea hivyo!

Mpaka hivi sasa tunapo ongea, amepigwa marufuku kuingia Marekani kwa sababu ya makosa lukuki yakiwemo ya uvunjifu wa Haki za Binadamu, nk. Kiufupi tu, Makonda ni mchafu!

Hapa ni nje na kukwepa kodi kupitia yale Makontena, kufoji cheti chake cha elimu, kunufaika binafsi kupitia kampeni ya madawa ya kulevya! Kabla ya Bosi wake kumteua Mkurugenzi wa kudili na hiyo kampeni, amejawa na dharau, nyodo, sifa, unafiki, majivuno, kiburi, ulevi wa madaraka, nk.

Mkuu juzi marekani Kuna mtu kaingia Supermarkt na kuua watu kama kumi na zaidi. Wasalimie
 
Back
Top Bottom