Mwanza: Yaliyojiri kwenye kuaga mwili wa Hayati Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Sipati picha vibaraka wake mna hali gani huko mliko ?: Mwacheni Mungu aitwe Mungu maana ndio hakimu wa haki .
Nipo salama kama mambo yalivyopangwa na tunatarajia kukamilisha yale yote yalioandikwa kwenye ilani ya ccm wembe ni ule ule hatucheki na kima!
 
Leo nimemkataza kabisa mama asiende uwanjani maana najua tunaweza mpoteza tumemuwekea TV kubwa alilie sebuleni yaishe
Umefanya jambo jema sana. hawa wanaomchuuza mwenzetu angani, vichochoroni, darajani, na mitaani wanataka tufiwe wengi. Maana kule dar karibu kila kata kuna msiba wa kukanyagana pale uwanja wa uhuru. Watu wamebaki na vidonda vya kufiwa ndugu zao wa karibu kwa sababu ya wanayezurula naye kila kona. Azikwe ili tupumue na tuwe na amani maana kuna watoto walikuwa wanatoroka na kwenda kukanyagwa huko. Mbaya zaidi wanakataza kusafirisha maiti za ndugu zetu. Eti sharti wazikwe hukohuko Dar. kKwa nini?
 
Hivi hawa wanaovuka barabara ghafla gari za msafara zinapokaribia wanakuwa wanatafuta nini. Watz tupo kama mang'ombe
Waache watu waonyeshe hisia zao kwa mpendwa wao. Kuwaita ndugu zako mang'ombe sio Sawa,lakini wewe utakuwa ng'ombe kasoro mkia.
 
Nawawazia sana wale wote waliohama upinzani kwa lengo la kuunga Juhudi za Hayati Magu.

Sijui watarudi walipotoka ama watatafuta sababu nyingine.
Jerry Murro amekiri wazi kabisa kwamba haelewi maisha atayaendeshaje maana alishikwa mkono na huyu Marehemu na sasa hayupo na hana mtu wa kumshika mkono tena! Halafu huko Yanga ambako angeenda nako timu haifanyi vizuri. Tabu tupu! Halafu Vincent Mashinji alikuwa bado kwenye list ya kupewa cheo. ndio hivyo tena.
 
Mwanza ni soo
Your browser is not able to display this video.
 
Hivi wale Covid-19 walienda kuaga mwili wa aliyewashika mkono?
 
Mods,huu ulikuwa Uzi unaojitegemea ukiwa na kichwa cha habari tofauti na hapa mlikouleta.
Je,hapa ndipo mahali pake?Nilitaka kufahamishwa maana ya neno Jeshi linalotamkwa na waombolezaji,ni sawa kuunganishwa hapa kwa yanayojiri Mwanza?
 
Msukuma mwenzao sharti wamlilie na aliwaweka wengi sana kwenye nafasi. Sikuelewa kabla kwamba wasukuma wana ukabila kiasi hiki
 
Aliwapendelea sana kwenye suala la maendeleo (ukabila) so ni haki yao kuhuzunika, bt wachaga wanakaribia kumaliza stock yote ya tbl.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…