Mwanzoni nilifikiri ni Utani, ikageuka Kero na Sasa nimegundua ni kweli Na kuukubali

Mwanzoni nilifikiri ni Utani, ikageuka Kero na Sasa nimegundua ni kweli Na kuukubali

Akanambia "sasa wewe unafikiri ulivyo leo mi sawa na ulivyokua before ukiwa na mkeo? Now daya mdogo angu ume regain, afya yako imerudi, umependeza sana, hata huyo mke wako hawez tu kukuambia ukifika kwasalikia wanao, tena natamani sana siku hata hao shemeji zako wakuone jinsi walivyotaka kukuua mtoto wa watu" 😂😂

DEAR MEN AND WOMEN
WE LIVE ONCE, LETS LIVE TO THE FULLEST.
DONT FORGET YOUR FAMILLIES BUT LET YOUR FAMILLIES MAKE YOU FORGET ABOUT YOURSELF.

Dont live just to pass days, live to be happy and inspire .
Good day to you all.
Safi sana brother, you're positive optimist. Btw zingatia ule ushauri. 👊🏾
 
Wakuu, mambo salama!?

Kazi ndiyo utu, hivyo niwapongeze na majukumu yenu mnayoendelea nayo.

Kuna suala ambalo siku ya juzi (Jumanne) nimekutana nalo kwa mara ya 5 hivi, na nikaamua kulidodosa kimtindo fulani. Then I realized, it is true.

Nilikuwa jijini for almost a week kwa shughuli zangu tu kimajukumu. Na katika harakati hizi nikalazimika kufika Bank (CRDB Tazara Branch). Ilikuwa mida ya mchana, kama saa 8 hivi.

Kwa utaratibu wangu kibenki ni lazima nikahudumiwe dirishani, hivyo nilipoitwa namba yangu nikasogea kuhudumiwa.

Nikasubmit cheque yangu pamoja na kitambulisho kama utaratibu unavyotaka. Kitambulisho ninachotumia always ni NIDA.

Sasa hapa kwenye kitambulisho ndipo ambapo huwa nakutana na kero ya hili suala ambalo ndilo limenifanya kuandika huu uzi. Swali hili nimekuwa nikikutana nalo zaidi ya mara 4, na hii juzi ilikuwa ya 5. Na zote ni katika branch hizi za CRDB kila ninapofika kutoa pesa. Mara ya kwanza kuulizwa swali hili nilifikiri labda ni utani tu, mshkaji ananizingua kwa kuwa aliyekuwa akinihudumia ni mwanaume. Hivyo sikulichukulia serious.

Mara nyingine likajitokeza tena, na mara hii lilikuwa serious kidogo maana kabla sijapewa pesa (nafikiri na figure ilichangia pia), yule muhudumu nilimuona akinyanyua simu akapiga. Baada ya muda alipomaliza akani-cash out. Sikujua anaongea na nani, lakini ni baada ya kuniuliza swali lile lile ambalo nimekuwa nikikutana nalo kila nifkipo CRDB. Na nilipotoka, mshkaji wangu akanipigia simu (mimi na yeye ni signatories kwenye hii akaunti ya kampuni). Akanambia nimepigiwa simu na jamaa wa CRDB wakitaka nithibitishe ni wewe unatoa pesa. Nikamjibu, “Okay, washanihudumia tayari.”

Sasa na hii juzi nikiwa Tazara Branch, yule mrembo akaniuliza tena:
“MWENYE HII KADI NI WEWE??????”

😂😂😂😂

Kwa kuwa sasa swali hili nimeshalizoea, nikatabasamu na kumjibu kwa upole tu na furaha:
“Yeah, ni mimi dada yangu. Mungu amenihurumia kidogo, amenirudisha umri wangu nyuma.”

Akajibu, akasema:
“Aisee, sio kidogo. Mshukuru Mungu, maana you now are so very much young looking. Na hapa ulikuwa kama umezeeka sanaaa, hamfanani kabisaaaa.”

Nikamwambia:
“Ni kawaida dada yangu. Si unajua sisi wanaume huwa tunaanza kwanza kuzeeka, kisha tunarudi kuwa vijana??”

Akacheka sana. Actually, tulitokea kuwa na maongezi very entertaining japo ya muda mfupi, yeye akiwa anaendelea na kazi. Kisha akanikabidhi cash. Sikuchukua, nikawa namtazama usoni.

Akauliza:
“What?”

Nikamjibu:
“Tazama cash counter yako vizuri.”

Basi akaishia kusema:
“Ooohh aisee, imekuaje hii mpaka nakuzidishia pesa? Au ndiyo nataka kukuhonga jamani?”

Nikasema:
“Usijali.”

Nikachukua cash yangu nikaondoka.

On the same day nikawa ninageuza zangu mkoa usiku.

Sasa jana, nikiwa naongea na sister baada ya kupita home kuwasalimia, nikawa nampa hii habari.

Akanambia:
“Sasa wewe unafikiri ulivyo leo mi sawa na ulivyokuwa before ukiwa na mkeo? Now, dada mdogo angu, ume-regain. Afya yako imerudi, umependeza sana. Hata huyo mke wako hawezi tu kukuambia. Ukifika, wasalimie wanao. Tena natamani sana siku hata hao shemeji zako wakuone jinsi walivyotaka kukuua mtoto wa watu.” 😂😂

Akaendelea:
“Basi tu tulikuwa hatuemi kwa kuwa tunajua labda ni maisha. Ila ulikuwa umechoka, umechakaa sana, huvai ukapendeza. Yaani dogo ume-change completely. Ni wewe tu sasa uamue kurudi gerezani au ubaki uraiani.” 😂

Nikaona ooohhhohh!! Mwaka sijamaliza na this comes up!??

Anyway, wito wangu kwenu wanaume na wanawake mlioko kwenye ndoa na familia:
MSIJI SACRIFICE kupitiliza mpaka mkajisahau kuwa nanyi mnapaswa kufaidika na hustle zenu.

Take time kujali familia yako, lakini kama baba na kama mama pia, take time kujipamba, nunua nguo nzuri, kula vizuri, pata muda wa kupumzika, na sometimes pata muda wa JUST KU DO NOTHING AT ALL.

Usiwe na ratiba serious all the time. Sawa, tunajua kuna watoto, kuna familia, kuna kazi, ndiyo… but DON’T FORGET YOURSELF.

Actually ni kitu ambacho kwetu wanaume hasa huwa ni kawaida: nguo chache, viatu vichache, yani hatujipi sana kipaumbele. But we should change. Hata mimi nimeishi maisha haya miaka almost yote: pair 1 au 2 za viatu, suruali 2 au 3 na you’re just fine, no shida at all. But…

Nimekaa jana nikajichunguza, ndipo nikagundua dooh, now ni kama nime-overdo kiukweli, kila upande. Nikajiuliza why? Nikaja kugundua now niko much more flexible na pesa yangu. Sijiulizi mara 2 ninunue kipi. Kitakachopita mbele yangu na kikanivutia, ninabeba, iwe ni kiatu au nguo. Zamani hii mindset sikuwahi kuwa nayo at all. I have time to rest. I have time kujali even ratiba zangu za saloon—kitu ambacho zamani niliona kama mambo ya kike sana. Na hii mindset nafikiri wanaume wengi tunayo. We better change for good.

As a result, I am completely changed—typically. Kuna vitu ambavyo zamani nilikuwa sijali kabisa, but now, being alone, nimejikuta nina utaratibu wa tofauti kabisa. I care about my health, hasa mazoezi. Siku hizi, mfano ninaposafiri, siwezi kufikia lodge yoyote. Lazima niulize:
“Je, kuna gym nearby?”
Cz lazima every day ni lift weights every morning and evening.

So nikaja ku-conclude kuwa kumbe mabadiliko haya SIO BY CHANCE, BUT BY PURPOSE.

DEAR MEN AND WOMEN,


WE LIVE ONCE, LET’S LIVE TO THE FULLEST.

DON’T FORGET YOUR FAMILIES, BUT LET YOUR FAMILIES NOT MAKE YOU FORGET ABOUT YOURSELF.

Don’t live just to pass days; live to be happy and inspire.

Good day to you all.
Tatizo wanaume tukianza kujua wanawake tunajikuta tunawazingatia sana wao huku sisi tukijitesa maisha yetu.
 
Thank youuuuuu.
Thiis is what am saying my friend.
Na sio kama tuna penda ila inatokea tu.
Ujue sometimes hata mwenza wako anaweza anza kukuchukulia poa kisa tu hii kitu,
Ukishazoe divorce lazima mtu anenepe mkuu.. Kipengele kwenye initiations ya divorce na zile violence zake.. lazima mwili upauke 😅
 
Back
Top Bottom