Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

Wee mke wake mkubwa ana 39 [emoji849]

Mwanaume 33

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Basi mke ana insecurities na mume wake ndo wa kumuondolea hiyo hali,

ila kuna wanawake wana moyo mi siwezi kumpenda mwanaume naemzidi kiasi hicho miaka 6!!! Akinizidi hata mwaka tu bado naona si sawa,, au nimezoea kutoka na mababa😂😂
 
Ambacho sijasema ni kuwa nilikutana nae akiwa na mtoto, na kibaya nilijua hilo kwa baadae sana kwa hiyo hajazalia kwangu
🤣🤣🤣🤣🤣Kumbe mwanamke mwenyewe ndio mjinga....mzeya piga chini huyo hakufai.
Wee mwanamke gani unazalishwa hovyo na wanaume bila kuwa kwenye ndoa...hajui kutumia akili huyo.
 
HABARI wakuu, kwanza kabla ya yote niwatakieni mfungo mwema,

Umri wangu ni Miaka 33, Nipo katika ndoa pia nina Watoto Wawili na huyu mwanamke, naona nisiandike Mengi kuhusu maisha yangu na huyu Mwanamke ila kimsingi tu ni MTU ambae ninapitia changamoto nyingi sana katika mahusiano haya, yaani kiufupi tu hata sielewi mwelekeo wa ndoa hii, Tulikutana nae tukachukuana nae Tukaamua kuishi pamoja hadi Sasa Tuna watoto wawili, lakini sijamtolea mahali, lakini sio kwamba sina uwezo wa kutoa mahali ila kinachonichelewesha ni aina ya maisha ambayo tunaishi nae, Yaani siku za furaha ni za kuhesebakika kuliko siku za kununiana, ana vijisababu visivyokuwa na mashiko anajinunisha, Mara utastuka usiku unamkuta MTU amekaa kitandani analia bila sababu, Mara atoke akae jikoni usiku, Mara ajidai amepandisha presha nianze kumpepea usiku yaani ni mateso bila ya kifo, Kimaisha siko vibaya ninamtimizia kila hitaji pia ninakaa kwangu sijapanga na Mimi ni MTU wa kutoka asububi narudi jioni kutokana na aina ya harakati zangu zinazoniweka mjini, Sasa kulitokea kasumba Kikitokea kimgogoro kidogo ananinyima unyumba, hadi inafkia mda unazuka ugomvi ndo napewa huwa nawaza namna ya kuachana nae, ila nawaonea huruma sana wanangu, pia hata yy namuonea huruma, maana nishamzalisha watoto Wawili wote alafu nimuache huwa kimsingi naishi nae kwa sababu ya huruma, pia kwa sababu ya kuwaonea huruma wanangu nilitamani wanangu walelewe na wazazi wao ila mwelekeo wa Maisha haya sijajua hatima,

Tangu mwezi wa Pili kuna shida ilitokea nikawa nanyimwa unyumba hadi ikafikia hatua nikakosa namna ikabidi nianzishe uhusiano na mtu mwingine ila kibaya nilianzisha kama njia ya kumaliza haja zangu nikirudi nyumbani najilalia zangu maana sikutaka ugomvi wa kutaka mbususu kwa wife ila kibaya naona nimezama mazima yani huyu mtoto anajua kucare, anajali kiufupi ninapata kila kitu ambacho nilikuwa nakosa awali, lakini kibaya zaidi na bahati mbaya kwa sasa huyu Mtoto ana ujauzito wangu, hapa nipo njia panda, Kusema kweli ingekuwa uwezo wngu ningemuoa huyu mtoto maana kimsingi mke ninaekaa nae ameshindwa kutambua thaman yangu, lakini kila likija swala la wanangu huwa naishiwa nguvu maana siwezi kuruhusu wanangu kukaa mbali na Mimi pia sina imani kama mwanamke huyu ataishi na wanangu vizuri mda ambao Mimi sipo, kusema kweli najikuta naishi katika majuto niliingiaje 18 za huyu mwanamke! Na ni namna gani nitaepuka hili!

Pia kuhusu suala ya yeye Pengine ana mahusiano mengine siwezi jua na huwa sina asili ya kifuatilia maisha yake maana nipo bize sana na pia huwa sitaki kabisa kufanya kumfuatilia maana matokeo ya kumfuatilia MTU siku zote hayawi mazuri,

Kibaya zaidi ni kuwa jamii tunayoishi nayo inatuona tuko vzuri maana mchana tunaigiziana ila ikifika usiku hakuna MTU anamsogelea mwenzie.

USHAURI WENU MHIMU.
Ndio ndoa nyingi zilivyo,hapo ni kuvumilia tu na kumshirikisha Mungu kwa maombi ili alete amani.Huyo huko nje ndio kawaida yao hiyo,ukisema tu naye umuweke ndani anaweza kuwa ndio balaa kuliko hata huyo uliye naye,am talking through experience...
 
Sisi tuonajiandaa kuingia huko mada kama hizi zinatukatisha tamaa sana.
 
Nilishasem uwezo wa kupeleka mahali ninao mda wowote ila changamoto aina ya maisha tunayoyaishi ndio hayaridhishi kabisa nakumbuka alishawahi kunipiga na kukimbia na nilivyotaka kumkimbiza kuna wazo likanijia nitaonekana mjinga mbele ya jamii kwa hiyo huwa namwacha, tu ila ni tukio haliwez kufutika kila nikiwaza kumrasimisha kuwa mke wng
Alikupiga na kitu gani?
 
Una uwezo na huoi
Leo unawaza kuoa mwingine
Na bado unajiuliza mkeo kwa nini ananuna
Nyani haoni kundule

Oa uone km hicho kisirani kitakuwepo

Mtu unajitoa af mwisho mwanaume haoni umuhimu.,mtakuja kuuwawa hivihivi
Anaanzaje kuniua sasa? Niuawe mi lofa? Ukiona dume limeuawa ujue ni lofa na lipumbavu[emoji23]
 
Hata mimi yamenikuta haya ila mimi ni muislaam nilizama kwa mwanamke mwingine baada ya mkewang kuwa anazingua penzi lilivyonoga na huyu mwanamke mwengine ikabidi nimuoe kabisa ila sasa mkewangu wa kwanza hataki uke wenza
 
Hatumtetei; we speak from a woman's perspective

Ushauri tu; ukiona hujamchunguza mwenza wako kiasi cha kujiridhisha; msivutane kuishi kiholela kisa ngono tamu. Wanawake tunapohamia kwenu huwa tunakuja na wazo kuu la kuanzisha familia, wakati nyie ndiyo mnatumia muda huo kutuchunguza. Uchunguzi wako unakamilika tayari mmeshazaa watoto kadhaa na unaona hakufai; utamfukuza huyo mwanamke? Kwa hiyo tupunguze kuishi kiholela, na kuchunguzana tufanye tukiwa huku nje
Aisee nimeipenda hiyo from women's perspective
 
Kilichopo kaa naye chini muwekane sawa utoe mahari na ufunge naye ndoa, kila lakheri.
 
Back
Top Bottom