Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

Umeshajiandaa kisaikolojia lakini? Endeleeni kujifanya mnawapenda wanawake.
 
Iwapo kama alikuwa anafanya huo ukorofi kabla ya kuanzisha uhusiano na huyo mchepuko wako hapo itakuwa siyo sababu ya kurogwa na mchepuko lakini iwapo hayo yameanza kujitokeza baada ya wewe kuwa na huo mchepuko basi ujue ni wazi kuwa hiyo ni kazi ya uchawi alowaroga mchepuko!

Try to be honest Kwa kuchunguza hiyo hali imeanza lini na kwanini?!
 
Hata hivo siku zote mshtaki ndio kaonewa mkuu kwa hiyo Mimi nimeleta shtaka langu huku ingefaa ushaur kama lilivyo hadi atakapokuja yy nae aseme kwa upande wake
Terminator unajua ulikosea kitu kimoja. Huyu mwanamke ungemuacha tu baada ya kuchoshwa naye then ukaendelea na maisha yako. Lakini inaonekana ulimvumilia pamoja na kukudanganya kuhusu umri na mtoto; na bado unamsaidia kulea hata mtoto wake inapobidi; nini kinakufanya ushikilie kumuacha sasa hivi? Definitely ni huo mchepuko wako ndiyo unakufanya upambane sana kumuacha mkeo, ili uishi nao kwa amani.

Lakini najiuliza tu binti mwenye maadili anaanzaje kutembea na mume wa mtu na kumbebea mimba juu within a short time? Mbona anaonekana kama yupo calculated sana? Na usikute uliyamwaga madhaifu ya mkeo kwake so kaona akijiongeza na kukubebea mimba, akijua utamfukuza tu mwenzie then yeye aingie ndani. Na bado unafanya kosa lilelile; unakurupuka kumuoa mchepuko ilhali hujamjua vizuri tabia yake; hata yeye ana tabia nzuri sasa hivi mwanzoni kama ambavyo mkeo naye mwanzoni alivyokuwa mwema. Subiri muanze kuishi pamoja; usije ukawa umeruka mkojo na kukanyaga mavi.

All in all; mwambie mkeo ukweli, muache, aendelee na maisha yake. Na usitegemee kuwe na amani kati yenu kwa sababu naamini kabisa atajua umeamua kumuacha kwa sababu ya mchepuko wako. Usitegemee pia kuwa na mahusiano mazuri na watoto wako; mkeo lazima atamalizia uchungu wake kwa kukutenga na watoto wenu. Na usitegemee pia m(wa)toto wa mchepuko kuja kuwa in good terms na watoto wa huyu mkeo wa sasa. Wanawake huwa chuki zetu tunazihamishia hadi kwa watoto. So jiandae vizuri kisaikolojia.

Halafu usiniambie kuwa unataka umuondoe mkeo na watoto kwenye nyumba uliyojenga naye afu uje uishi hapo na familia yako mpya. Ondoka wewe hapo nyumbani, kaanze maisha mapya na mchepuko. Kila la kheri
 
Yote tisa kumi tatizo ni wewe....unamzalishaje mtoto wa watu watoto wawili wote hujamtolea mahari....hakika kilio chake ni majuto ayapatayo ... Anatamani nae aonekane mwanamke...ni sahihi unavyombeza.wanawake na sisi bhana

Huyo mwanamke Ndio boya anaishi Vipi na mtu ambae hajamuowa?! Alitakiwa sahizi awe kwao kiherehere chake cha kuishi na mtu Aja kuowa
 
Mkuu unahangaika saana, lakini majibu ni simple.
1. Nenda msikitini, badilisha dini, waoe wote wawili maana inaruhusiwa. Ya nini kuchanganyikiwa na mmoja, bora wakuchanganye wote wawili ujue moja kua unaenda kuokota makopo. Au wachanganyane wao kwa wao we ubaki unakula popcorn na kufurahia movie
2. Wacha uoga wa kusema unasitiri sijui kuna mengi, we yaweke yote wazi, maana mwanzoni ulianza na machache, ghafla ukaja na ishu ya mtoto mkubwa, mara umri kuzidi, unawachanganya wana bodi, we sema yote tu tujue. Mficha uchi hazai, samahani, mficha maradhi kifo humuumbua.
 
Mbombo ngafu...mkuu unaishi ila huna namna kazi sana!!
 
Sasa mzeya kama ulikuwa nje unaenda kutaka kupata mbususu inakuwaje tena mpaka unatia mimba mzeya au mtoto tako zuri mpaka ukaamua kunyumyuzia mazima🤣🤣🤣🤣
 
Dah kumbe wanawake ndoa mnaitaka hivyo alafu humu jf mnajidaigi manunda 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Dah!... Ulikuwa na haraka Sana ya kumiliki jiko, hivyo baadhi ya mambo hukufatilia kwa undani.
 
Yote tisa kumi tatizo ni wewe....unamzalishaje mtoto wa watu watoto wawili wote hujamtolea mahari....hakika kilio chake ni majuto ayapatayo ... Anatamani nae aonekane mwanamke...ni sahihi unavyombeza.wanawake na sisi bhana
[emoji16] mwalimu bana.Ko kutomtolea mahali ndo kunafanya apandishe presha,akae kitandani na kulia,aende kukaa jikoni usiku kununiana ugomvi mpaka kumnyima Mume wake unyumba?

Kama alipenda kutolewa mahali,angekataa kuzalishwa.Kwani alilazimishwa?[emoji848]

Labda ndivyo walivyo kubaliana kwenye swala la mahari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…