Mwendokasi yaua mtu Ardhi-Kivukoni, chanzo kuchat wakati akivuka barabara

Mwendokasi yaua mtu Ardhi-Kivukoni, chanzo kuchat wakati akivuka barabara

Wana jf.

Leo nimeshuhudia kifo cha ajabu mno. Ilikuwa hivi, MTU mmoja akiwa anatokea maeneo ya postal/ mjini alipofika kwa ofisi ya mwanasheria mkuu alivuka barabara ya kwanza inayotoka na kwenda Kivukoni.

Ghafla bila kuangalia huku akiwa anongea na simu ndipo mwendokasi ikampiga na kumzungusha chini ya uvungu na kukanyagwa na tyre lingine LA mbele, kakanyangwa shingo.

Wakati huo dreva tunamwambia rudi nyuma umekanyaga mtu, yeye akakosa nguvu kabisa arudisha kumbukumbu kurudi nyuma tayari damu nyingi zinachuruzika na mtu ajitingishi.

Mpaka sasa polisi ndio wanafika kuuchukua mwili. Funzo usivuke barabara wakati unaongea na simu, kusikiliza mziki na headphone.

[emoji26]
RIP
 
Marehemu ndiye kajiingiza, hata hivyo haya magari NAyO vimeo sana kwenye breki sio ya kuyaamini hata kama huko kwenye zebra, jamaa kabla ya kumgonga alimpigia honi lakini ndio hivyo sikio LA kufa
Makosa watayapima na kuyagundua matrafik police, lakini kuna kasumba ya madereva kutumia honi badala ya breki, hilo nalo ni 'gonjwa'!

Sijawahi ona honi kwenye kampishe mpishe ikisaidia zaidi ya kuchanganya akili za watembea kwa miguu!

Unapiga honi huku upo kasi zaidi ya speed 100, unategemea upishweje!

Makosa yapo kwa watembea kwa miguu pia, lakini mwenye chombo pamoja na kasi ndiye anayetakiwa kuimiliki sawasawa barabara.
Apumzike kwa amani marehemu.
 
Kuna mdogo wangu nilimnasa vibao barabarani kwa ujinga wa kukaa na earphone 24/7 yani ujinga na ulimbukeni hizo simu wanazongangania muda wote sasa hazina ata inshu za maana zaidi ya ma group ya WhatsApp na Instagram
 
...........................Ila tusimlaumu sana marehemu unajua sometimes kama mwanaume unaweza kujikuta kwenye hali mbaya unakuta mfukoni mia huna even nauli tu ya kukufikisha home huna,nako ulipotoka asubuhi mambo umeacha siyo mazuri unadaiwa kodi ya pango kazi yenyewe ya kueleweka town huna so inawezekana simu aliyokuwa anaongea nayo ni msaada aliitiwa mahali sasa ukichanganya na mawazo ya kuwahi msaada wenyewe na maisha yalivyomchanganya marehemu ndo limemkuta hilo.

Mungu anajua,hili la Corona siyo kwa akili zetu kuishi nalo ni Mungu tu ametuacha kutokana na anazijua hali zetu.daily life ya Mtanzania ni kukutana na hatari toka anaamka asubuhi mpaka analala usiku sasa hiyo Corona tupewe ya kazi gani?na hizi ndo style za vifo vyetu,mtu anakuwa stressed kiasi anajikuta anajiendea hovyo tu barabarani kudra za Mungu zinamwokoa akipenda litokee ndo kama hivi.

Inasikitisha sana,marehemu kaondoka na siri yake!
 
Niliwahi shuhudia kifo kilichotokana na fundi gari kutoa rim ya tairi la lori akiwa kainama analielekea basi lilimrusha mpaka angani na alipotua chini akawa amepasuka anamwaga vitu sijui ndio ubongo.

Bila shaka ni ile shanga ya rim ndiyo ilifyatuka na kumpiga
 
Duh siku hizi kila mtu ni mwanahabari.

Gari haliui, ila husababisha kifo/majeruhi.

Ripoti ya dokta ndo itasema kilichomuondoa marehem na kamwe haiwezi kuwa ni hilo gari.

Rip
 
Noma sana mkuu ndo maana Wanaume tunawahi kufa...[emoji46][emoji46][emoji46][emoji46]
 
Niliwahi shuhudia kifo kilichotokana na fundi gari kutoa rim ya tairi la lori akiwa kainama analielekea basi lilimrusha mpaka angani na alipotua chini akawa amepasuka anamwaga vitu sijui ndio ubongo.
Duuh rim ilimuua huyu...!! Ile presha ndani ya tairi ni nomaa
 
Wanahabari wenyewe wanaviz
Duh siku hizi kila mtu ni mwanahabari.

Gari haliui, ila husababisha kifo/majeruhi.

Ripoti ya dokta ndo itasema kilichomuondoa marehem na kamwe haiwezi kuwa ni hilo gari.

Rip
Ia habari za kuletewa, hapo kijiweni samora.
 
Watu wa Dar tumekuwa wajinga na wapumbavu haswa ikija katika matumizi ya barabara na matumizi ya simu. Kwanza hatuogopi magari, mtu anapishana na gari as if anapishana na mwenzake. Tunaogopa mvua kuliko magari na ndio maana kila kona watu wanapigwa balaa. Mbezi njia panda Goba na njia ya kuelekea Goba almost kila wiki anapigwa mtu.

Tuheshimu magari na tuheshimu tukiwa barabarani.
 
Maisha haya. Inatupasa kuishi maisha ya toba kwa kumpokea.Yesu kuwa Bwana na Mwokozi
Kwakua wewe ni mwanamke, sio kosa Yesu akiwa bwana wako, lakini sio kwa kidume kama mimi.
Mkewangu atani elewa vipi nikimwambia nina bwana anaitwa Yesu?
 
Back
Top Bottom