Mwendokasi yaua mtu Ardhi-Kivukoni, chanzo kuchat wakati akivuka barabara

Mwendokasi yaua mtu Ardhi-Kivukoni, chanzo kuchat wakati akivuka barabara

Na kuna wale watembea kwa miguu wanaovuka huku taa zipo kijani unakuta gari imechochea inawahi taa mtu anajitupa barabarani avuke..

Afu trafic hawatoi elimu yoyote kwny hili wao kazi kubeba buku mbili za kiwi
 
Acheni kumshambulia marehemu. Alipangiwa atakufa hivyo pindi tu alipozaliwa. The forces of nature
Mkuu Hakuna mahali Nimesema marehemu alikuwa kwa earphones,nimetoa tahadhari kwa wengine wenye tabia hiyo.
Suala kwamba kifo na mambo mengine yako pre determined na nature ni mjadala wa kifalsafa na kimtazamo,unaweza kuanzisha uzi wake
 
Wana jf.

Leo nimeshuhudia kifo cha ajabu mno. Ilikuwa hivi, MTU mmoja akiwa anatokea maeneo ya postal/ mjini alipofika kwa ofisi ya mwanasheria mkuu alivuka barabara ya kwanza inayotoka na kwenda Kivukoni.

Ghafla bila kuangalia huku akiwa anongea na simu ndipo mwendokasi ikampiga na kumzungusha chini ya uvungu na kukanyagwa na tyre lingine LA mbele, kakanyangwa shingo.

Wakati huo dreva tunamwambia rudi nyuma umekanyaga mtu, yeye akakosa nguvu kabisa arudisha kumbukumbu kurudi nyuma tayari damu nyingi zinachuruzika na mtu ajitingishi.

Mpaka sasa polisi ndio wanafika kuuchukua mwili. Funzo usivuke barabara wakati unaongea na simu, kusikiliza mziki na headphone.
Dooh
Ndo nagundua tuna msiba kwa jirani baba amefariki leo kwa kugongwa na Mwendokasi.

Mungu amlaze pema
 
Mimi navaa earphone nikiwa nayo siwezi iacha kamwe ila nikivaa hizo earphone hata sisimizi atoe sauti namsikia sauti yoyote kutoka maeneo yanayonizunguka naisikia kimsingi nasikiliza sauti ndogo sana.

Tatizo sio earphone mtumiaji.
Sio tu kuongea na simu,kuna ulimbukeni na ushamba wa kuvaa earphones 24/7 kwa watumiaji wa Barabara
 
Hilo ni eneo baya sana, binafsi nimewahi kukoswa kwa dereva kunikwepa, ilhali nilikuwa nimeangalia pande zote na hakukuwa na gari.

Ni kona moja hatari sana, na baada ya hapo mara kadhaa nimeshuhudia watu wakikoswa koswa

Ni BLIND CORNER kwa watembea kwa miguu

Believe and Trust me guys...

USHAURI:
Madereva wawekewe alama ya kupunguza mwendo kwani ni kona ambayo mtemnea kwa miguu haoni
 
Na kuna wale watembea kwa miguu wanaovuka huku taa zipo kijani unakuta gari imechochea inawahi taa mtu anajitupa barabarani avuke..

Afu trafic hawatoi elimu yoyote kwny hili wao kazi kubeba buku mbili za kiwi
Tatizo hakuna taa za watembea kwa miguu.Nchi zilizoendelea ni kosa kuvuka kwenye junction kubwa bila taa za miguu wanaita jaywalking

Sasa hapa bongo kwenye mataa kuna zebra halafu raia anavuka tu bila kujali kama taa za magari zimeruhusiwa.wanajua wao ndio wana haki peke yao kuliko magari.

Pale ilala boma pale pana hatari sana
 
Dooh
Ndo nagundua tuna msiba kwa jirani baba amefariki leo kwa kugongwa na Mwendokasi.

Mungu amlaze pema
msiba huko wapi jamani bado nasikia uchungu sana maana nilitaka kumwokoa namwambia dreva arudi nyuma dreva ameshangaa tuu taili lipo shingoni .......
 
msiba huko wapi jamani bado nasikia uchungu sana maana nilitaka kumwokoa namwambia dreva arudi nyuma dreva ameshangaa tuu taili lipo shingoni .......
Msiba upo Kigamboni maeneo ya Mikadi

Maziko ni leo saa kumi alasiri.

Mungu ampokee mja wake
 
Msiba upo Kigamboni maeneo ya Mikadi

Maziko ni leo saa kumi alasiri.

Mungu ampokee mja wake
mbona wanasema eneo la kwa urasam marehemu alikuwa ameoa mke na bado hawajapata mtoto
 
Tatizo hakuna taa za watembea kwa miguu.Nchi zilizoendelea ni kosa kuvuka kwenye junction kubwa bila taa za miguu wanaita jaywalking

Sasa hapa bongo kwenye mataa kuna zebra halafu raia anavuka tu bila kujali kama taa za magari zimeruhusiwa.wanajua wao ndio wana haki peke yao kuliko magari.

Pale ilala boma pale pana hatari sana
Taa zipo za watembea kwa miguu sema hawazifatiliii
 
Maisha haya. Inatupasa kuishi maisha ya toba kwa kumpokea.Yesu kuwa Bwana na Mwokozi
Safi, na vitendo hivi vya KIFEDHULI vya kuzuia haki za wengine kuishi, vinavyoendelea chini ya utawala huu DHALIMU wa CCM vinapaswa kupingwa kwa nguvu zote na kila mpenda haki na mwenye HOFU YA MUNGU.

ITOSHE TU KUSEMA, MITANO YA UTAWALA HUU WA MKONO WA CHUMA SASA BASI...
 
Back
Top Bottom