Artifact Collector
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 6,617
- 10,205
Hakunaga huduma ya mafuta ya upako kwenye bibliaHakuna miujiza dunia ya sasa, hiyo ilipita huko miaka ya nyuma ambapo manabii wa kweli walizawadiwa. Hakuna kipawa cha mafuta ya upako, hayo yanayoonekana ni wizi na ujambazi na utapeli ulokithiri
Sitaki nimhukumu mwamposa Ila ninachojua hakuna huduma ya mafuta ya upako kwenye biblia tokea mwanzo mpaka ufunuoNabii wa KWELI wa MUNGU hutenda miujiza kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU aliyepewa na MUNGU na siyo kwa uwezo wa "mafuta" au "keki" au kitu chochote kile. Tena siyo yeye anayetenda bali ni YULE ROHO wa MUNGU akaaye ndani yake.
Na huduma hiyo hutolewa bure kabisa bila malipo yoyote. YESU KRISTO alisema : "mmepewa bure, toeni bure". Na ndivyo akina Petro na mitume wengine walifanya zamani zile.
Huyo Mwamposa hana ROHO MTAKATIFU. Mwamposa ni mfanyaMAZINGAOMBWE anayetumia jina la YESU KRISTO kama kivuli.
bro si ndio hawa hawa, tunawaita mitume na manabiiHivi wale Wana mazingaubwe wameendaga wapi siku hizi mana siwaskii mitaan Wala mashuleni!
14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.kabisa....ukisoma Biblia manabii walikuwa govermental. kazi yao ilikuwa kuona masuala mazito kwa ajili ya taifa na kuwashauri watawala/wafalme. hleo hawa wahuni kazi yao ni kuuza maombi na bidhaa na kutafuna wake za watu kisha wanajiita manabii.
mtu hujawahi kulitabiria taifa hata jambo moja kisha unajiita nabii
Hapo sinza Vatican hukuambiwa utoe hela?Kuhusu suala la huyu Mwamposa nina ushahidi kabisa ana muunganiko na nguvu za giza.
Kwa sababu kuna siku wakati yupo pale Sinza Vatican nilienda pale akawa anaombea watu na ilipofika kwangu akaniuliza shida yako nini? Nikamwambia nahitaji kazi na maombi nilishapeleka lakini bado kuitwa alichoniambia *NYOTA * zangu zimeshuka zipo chini akaniombea. Halafu kuna Uncle wangu ni Mganga wa Kienyeji haswaa huwa anatoa huduma kwa Viongozi wakubwa wa Serikalini na sifa zake zimewafikia mpaka Waarabu wa Oman, Doha, Bahrain, Qatar kote huko huwa anaenda kutoa huduma ya tiba na watu huwa wanafanikiwa. Sasa huyo Uncle wangu kuna siku nilikutana nae Sehemu ananua dawa kwenye maduka ya dawa za asili na yeye ndiyo aliyeniona akaniita. Tukazungumza pale akaniuliza vipi Kazi ulishaanza? Nikamwambia bado baada ya dakika kadhaa pale pale akaniambia Nyota zako chini.
Sasa Mwamposa aliniambia Nyota zangu zipo chini na huyu Mganga wa Kienyeji Naye aliniambia nyota zangu zipo chini. Kuna nini hapo?
Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Ulichoongea ni kweli ukishaona unaweka Imani yako kwenye vitu kama mafuta ya upako, maji ya upako na sio kwenye damu ya YESU na jina la YESU ujue Kuna shida mahali huna tofauti na mtu anayeabudu sanamuNdugu tofautisha doctrine imani na revelation mafunuo. Doctrine ya mkristo ni kuliamini jina la Yesu Kristo na kuliitia pale inapobidi kwa kukesha na kuomba.
Revelation ni mafunuo ya muda mfupi. Kwa mfano Yesu alipompaka matooe yule kipofu ilikuwa revelation ya muda mfupi sio imani au doctrine. Imani Ni muda wote wa ukristo ila mafunuo ni kwaajili ya muda huo pekee. Ndio maana humuoni Yesu akimpaka matope kipofu mwingine maana ilikuwa kwa wakati na kwa kusudi maalum.
Sasa manabii wa Leo wanatumia mafunuo na kuyanya imani. Yani watu waache kuliitia jina la Yesu Kristo na kuhangaika na mafuta na maji, ukiuliza wanakwambia mbona Yesu alifanya hivi. Njia moja ya kumjua Nabii wa uongo ni pale anapotumia mafunuo kama msingi wa imani.
Uko sahihi kabisa. Hata mitume wa YESU KRISTO hawakufanya huduma ya upako wa mafuta. KRISTO aliagiza watu wabatizwe kwa maji.Sitaki nimhukumu mwamposa Ila ninachojua hakuna huduma ya mafuta ya upako kwenye biblia tokea mwanzo mpaka ufunuo
Haya yoote uliyotaja ilikuwa ni kivuli hayakuweza kukamilisha au kumkamilisha mwanadamu. Muujiza wowote ambao hautokani na kuuhubiri na kumuinua Kristo Yesu ni mazingaombwe maana Kristo ndio utimilifu wa Mungu.Acha kukariri..unaikumbuka story ya naamani yule jemedari?
Unaikumbuka habari ya nyoka wa shaba?
Unakumbuka yule kipofu aliyepakwa tope?
Unafahamu wafalme walikua wakipakwa mafuta kwaajili ya upako wa kuwa wafalme?
Kama unaamini hizo story kwanini usiamini la mafuta na maji ya upako?
YESU alibatiza kwa Roho, ndo maana yohana mbatizaji alisema mim nabatiza kwa maji Ila Yuko anayebatiza kwa Roho atakuja akimaanisha YESUUko sahihi kabisa. Hata mitume wa YESU KRISTO hawakufanya huduma ya upako wa mafuta. KRISTO aliagiza watu wabatizwe kwa maji.
Lakini fahamu kwamba kusema ukweli au kukemea maovu ndani ya jamii sio "kuhukumu". Kuhukumu ni kutoa adhabu kwa muhusika. Na sisi hatujatoa adhabu yoyote ile kwa Mwamposa.
Anakama miaka 50huyu ndugu ninamfahamu tangia akiwa kijana alipotoka tukuyu safari yake ya huduma kabla hajafahamika ilianzia tunduma akiwa na sambamba na mchungaji efraim mwaitebele wa kanisa la restoration bible church tunduma ,alikuwa mpenda maombi sana hasa ya kwenda milimani, alikuwa anafanyabiashara pale soko la black tunduma amewahi kuuza viatu pia, kwa sisi vijana wa kipindi kile maombi mengi tulikuwa tunafanyia milimani,mwamposa alikuwa kiongozi wa maombi nawakumbuka vijana kama pasta mwankenja ambae kwa sasa ni mchungaji kitunda tulikuwa nao pamoja .badae alipata wito akawa anaalikwa sehemu mbalimbali kanisa lake kubwa na mahali watu walianza kumjua ni moshi ,pale jamaa alipiga kazi sana na alikuwa na waumini wengi mno sikuwahi fikiria kama angehama moshi.inasemekana badae ilitokea migogoro flani ya kifamilia kati yake na mke wake,mwamposa aliamua kuondoka moshi kwa hasira na kuamua kwenda dar kuanza huduma upya.haikuwa kazi rahisi maana alikuwa hana hata mahali pakufanyia huduma,alianzia sebulen kwa mtu akiwa n
Kabla hajafika sinza alikuwa anafanya ibada zake kwenye hema chafuchafu pale moshi, ndani ya soko la maimoria. Akawa anapaka watu mafuta, na kuwaombea kwa mafungu, mwenye milioni, mwenye laki 5 mwisho elfu 50 chini ya hapo hakuna maombi. Alipozichanga ndio akahamia huko sinza vatcan. Baadae akarudi kuchukua u phd kwa kukanyagisha watu mafuta ambapo kulipelekea watu 20 kuaga dunia.
Asie wee acha kuwananga watumish wa mungu ,muachie mungu awahukumuHuyu kachangia Sana kupotosha injili anayo sehemu yake kwenye moto wa kiberiti kama yule wa Nigeria baba yao wa uongo aliyekufa.
Ilikuwa siku ya jumanne hakuniambia kutoa hela.Hapo sinza Vatican hukuambiwa utoe hela?
Chochote kilichopo nje ya mafundisho ya Mungu ni ubatiliAsie wee acha kuwananga watumish wa mungu ,muachie mungu awahukumu
Hapa imethibitisha hujui biblia Ile nafasi ya yuda aliyetakiwa kuichukua ni Paulo na sio metiya, metiya alipatikana kwa wanafunzi kupiga Kura wala hawakumuomba MunguSio mafunzo pekee ndio mwamuzi
Yuda Iskariote akiposalisiti Yesu replacement yake kanisa lilifunga na kuomba Mungu nani ashike nafasi yake
Mungu akawaambia akawaonyesha kuwa mpeni Matiya
Sasa hivi mivyuo ya theolojia mtu akidoma mivyuo ya dini yao wanamuweka kazini bila hata kuomba Mungu kuwa huyo mtu kweli Mungu kamuita ili Mungu aseme mwenyewe sababu kazi ya kuweka wahudumu hudums tano yoyote ni yake
God factor imeachwa ndio masna makanisa ulaya na marekani waliingiza hadi mishoga kanisani kuwa mapadri au wachungaji matokeo ikapigania ndoa za jinsia moja na ushoga na usagaji ikiwa na mivyeti yoye ya digrii za vyuo vya theolojia vya dini zao
Bonge la point yaan metiya sio chaguo la MunguNikusahihishe kuhusu matiya, mitume walipiga kura na kura ikamwangukia matiya. Lakini kazi ya matiya haikuwa na matokeo, ndio maana Mungu mwenyewe akaamua kumleta Mtume Paulo.
Yes mke hana,ila kuna mdada kazaa nae kamjengea kighorofa huku Goba Kulangwa,alafu ni wale wadada wa mjini kishenzi.Alianza uinjilist wa kukaa na kuhubiri barabarani Mke wake akawa anaona aibu akasema tutafute kazi akasema hayupo tayari Mke wake akamtosa naye akajiwekea nadhiri kuwa hatuaacha kumtumikia Mungu hadi Ajue Mungu huyu ni nani ndiyo akampa hicho kipawa Chake..
I do not know lakini I think hadi leo hana Mke tena hata yule alipotaka kumrudi alikataaa.. A little I know though sina uhakika ready to be corrected
Kuna Mzee kila usiku saa nne sio Mara zote ni baadhi ya siku utamkuta na maji ya upako ya mwamposa anamwaga kwenye ukuta wake swali ambalo najiuliza kwanin asitumie jina la YESU au damu ya YESU kukilinda nyumba, inamaana anaamin maji ya upako kuliko damu ya YESU ukishaona hivyo uju Kuna shida mahali kubwa sanaNaomba nijibu kidogo ulichosema.
1. Kwanza kuhusu Luka 9:49-50, Yule mtu walimkuta anatoa pepo kwa jina la Yesu Kristo. Hilo ndilo la muhimu, alitumia Jina la Yesu Kristo kutoa mapepo na sio maji Wala mafuta. Kama wanafunzi wa Yesu wangemdaka huyo jamaa anatumia maji kuponya watu basi jibu la Yesu Kristo lingeweza kuwa tofauti.
Lazima ujue kwamba kuendelea kutumia zana za upako ni dalili za kuonesha kwamba Jina la Yesu Kristo alijitoshelezi hivyo tunalisaidia kwa kutumia chumvi au maji au mafuta.
Kuna maeneo wanatumia Hadi pipi au keki za upako. Shida ipo wapi kutumia jina la Yesu Kristo?. Kwanini usitumie jina la Yesu pekee mpaka uanze kuwambia watu wakanyage mafuta na kunyunyiza mafata kwenye majumba yao?.
Kazi ya shetani ni kulishusha jina la Yesu Kristo na kulifanya halina nguvu.
2. Pili, kuhusu Waefeso 4:11-13. Lazima uelewe zile ni huduma tano.
Mitume
Manabii
Waalimu
Wachungaji
Wainjilisti
Hizo huduma tano unapewa na Mungu sio unajipa mwenyewe. Baada ya kuokoka na ukajazwa Roho Mtakatifu Kuna huduma Mungu anakupa na wewe utaifahamu maana itakuwa ina imba ndani yako. Sasa hizi ni huduma sio vyeo au ngazi za madaraka.
Naomba nitoe mifano;
A. Kwanza mitume, mitume kazi yao kubwa ni kutembea ulimwenguni kote na kufungua kazi ya Mungu. Tena hutakiwa kwenda maeneo yaliyoshindikana au yasiyomjua Kristo Yesu. Ndio maana Paulo Kama mtume alitembea karibia dunia nzima akifungua kazi ya Bwana Hadi uarabuni. Sasa Leo tuna mitume wa vyeo sio huduma, ndio maana utakuta mtu anajiita mtume ila anasimamia kanisa. No mtume kwa huduma Hana kanisa bali anazunguka sehemu mbali mabli kufungua makanisa. Mitume wanatakiwa kwenda Somalia au Sudan au Iraq ambako injili haijafika, lakini leo ili utambulike kama mtume lazima ufanye miujiza au uponyaji basi.
B. Pili, manabii, manabii kihuduma Ni Jicho na mdomo wa Mungu. Kihuduma nabii hawezi kuchunga kanisa , Bali anaweza kuwa mshirika wa kawaida kanisani lakini mwenye uwezo wa kuona mambo ya mbele au mambo ambayo wengine hatuyaoni. Pia nabii husema Yale ambayo Mungu anataka kuonya kanisa au nchi au kundi fulani etc. Hivyo nabii kihuduma sio wa kuchunga kanisa bali kutoa mafunuo ambayo yanatoka kwa Mungu, kunifahamisha taifa yatakayokukuta mbele, kulionya taifa kuhusu dhambi na etc. Hivyo ni muhimu kuwa na huduma ya kinabii kanisani ili kanisa likomae.
Tatizo ni kwamba unabii wa Leo umekuwa ni cheo. Unabii Kama hudumu ni mchache Sana, ndio maana manabii wengi Leo hawaoni ya mbele au kkusema ya kutoka kwa Mungu ili kunenga ufalme wake. Utasikia Nabii anakuuliza unanifahamu au tunafahamian, anaanza ninakuona upo Mwanza, Mara naona jina Grace halafu watu wanachanganyikiwa. Kuna uganguzi na unabii. Uganguzi unabase kwa mwanadamu basi ila unabii ni kutoka mbinguni ili kuujenga ufalme wa Mungu duniani na kuonya kuhusu dhambi.
Niishie hapo kwa leo, ila ni muhimu kutofautisha utume na unabii wa kihuduma na utume na unabii wa kicheo.