Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Nabii wa KWELI wa MUNGU hutenda miujiza kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU aliyepewa na MUNGU na siyo kwa uwezo wa "mafuta" au "keki" au kitu chochote kile. Tena siyo yeye anayetenda bali ni YULE ROHO wa MUNGU akaaye ndani yake.

Na huduma hiyo hutolewa bure kabisa bila malipo yoyote. YESU KRISTO alisema : "mmepewa bure, toeni bure". Na ndivyo akina Petro na mitume wengine walifanya zamani zile.

Huyo Mwamposa hana ROHO MTAKATIFU. Mwamposa ni mfanyaMAZINGAOMBWE anayetumia jina la YESU KRISTO kama kivuli.
Sitaki nimhukumu mwamposa Ila ninachojua hakuna huduma ya mafuta ya upako kwenye biblia tokea mwanzo mpaka ufunuo
 
kabisa....ukisoma Biblia manabii walikuwa govermental. kazi yao ilikuwa kuona masuala mazito kwa ajili ya taifa na kuwashauri watawala/wafalme. hleo hawa wahuni kazi yao ni kuuza maombi na bidhaa na kutafuna wake za watu kisha wanajiita manabii.

mtu hujawahi kulitabiria taifa hata jambo moja kisha unajiita nabii
14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.
2 Wafalme 5:14

15 Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
2 Wafalme 5:15

16 Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
2 Wafalme 5:16

17 Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana.
2 Wafalme 5:17

18 Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili.
2 Wafalme 5:18

19 Akamwambia, Enenda kwa amani Basi akamwondokea mbali kidogo.
2 Wafalme 5:19

20 Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.
2 Wafalme 5:20

21 Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani?
2 Wafalme 5:21

22 Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.
2 Wafalme 5:22

23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.
2 Wafalme 5:23

24 Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.
2 Wafalme 5:24

25 Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali.
2 Wafalme 5:25

26 Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?
2 Wafalme 5:26

27 Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.
2 Wafalme 5:27
 
Kuhusu suala la huyu Mwamposa nina ushahidi kabisa ana muunganiko na nguvu za giza.
Kwa sababu kuna siku wakati yupo pale Sinza Vatican nilienda pale akawa anaombea watu na ilipofika kwangu akaniuliza shida yako nini? Nikamwambia nahitaji kazi na maombi nilishapeleka lakini bado kuitwa alichoniambia *NYOTA * zangu zimeshuka zipo chini akaniombea. Halafu kuna Uncle wangu ni Mganga wa Kienyeji haswaa huwa anatoa huduma kwa Viongozi wakubwa wa Serikalini na sifa zake zimewafikia mpaka Waarabu wa Oman, Doha, Bahrain, Qatar kote huko huwa anaenda kutoa huduma ya tiba na watu huwa wanafanikiwa. Sasa huyo Uncle wangu kuna siku nilikutana nae Sehemu ananua dawa kwenye maduka ya dawa za asili na yeye ndiyo aliyeniona akaniita. Tukazungumza pale akaniuliza vipi Kazi ulishaanza? Nikamwambia bado baada ya dakika kadhaa pale pale akaniambia Nyota zako chini.
Sasa Mwamposa aliniambia Nyota zangu zipo chini na huyu Mganga wa Kienyeji Naye aliniambia nyota zangu zipo chini. Kuna nini hapo?

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Hapo sinza Vatican hukuambiwa utoe hela?
 
Ndugu tofautisha doctrine imani na revelation mafunuo. Doctrine ya mkristo ni kuliamini jina la Yesu Kristo na kuliitia pale inapobidi kwa kukesha na kuomba.

Revelation ni mafunuo ya muda mfupi. Kwa mfano Yesu alipompaka matooe yule kipofu ilikuwa revelation ya muda mfupi sio imani au doctrine. Imani Ni muda wote wa ukristo ila mafunuo ni kwaajili ya muda huo pekee. Ndio maana humuoni Yesu akimpaka matope kipofu mwingine maana ilikuwa kwa wakati na kwa kusudi maalum.

Sasa manabii wa Leo wanatumia mafunuo na kuyanya imani. Yani watu waache kuliitia jina la Yesu Kristo na kuhangaika na mafuta na maji, ukiuliza wanakwambia mbona Yesu alifanya hivi. Njia moja ya kumjua Nabii wa uongo ni pale anapotumia mafunuo kama msingi wa imani.
Ulichoongea ni kweli ukishaona unaweka Imani yako kwenye vitu kama mafuta ya upako, maji ya upako na sio kwenye damu ya YESU na jina la YESU ujue Kuna shida mahali huna tofauti na mtu anayeabudu sanamu
 
Sitaki nimhukumu mwamposa Ila ninachojua hakuna huduma ya mafuta ya upako kwenye biblia tokea mwanzo mpaka ufunuo
Uko sahihi kabisa. Hata mitume wa YESU KRISTO hawakufanya huduma ya upako wa mafuta. KRISTO aliagiza watu wabatizwe kwa maji.

Lakini fahamu kwamba kusema ukweli au kukemea maovu ndani ya jamii sio "kuhukumu". Kuhukumu ni kutoa adhabu kwa muhusika. Na sisi hatujatoa adhabu yoyote ile kwa Mwamposa.
 
Acha kukariri..unaikumbuka story ya naamani yule jemedari?
Unaikumbuka habari ya nyoka wa shaba?
Unakumbuka yule kipofu aliyepakwa tope?
Unafahamu wafalme walikua wakipakwa mafuta kwaajili ya upako wa kuwa wafalme?


Kama unaamini hizo story kwanini usiamini la mafuta na maji ya upako?
Haya yoote uliyotaja ilikuwa ni kivuli hayakuweza kukamilisha au kumkamilisha mwanadamu. Muujiza wowote ambao hautokani na kuuhubiri na kumuinua Kristo Yesu ni mazingaombwe maana Kristo ndio utimilifu wa Mungu.

Matendo 8:4 Hata hivyo, wale waliotawanyika wakapita katika nchi wakitangaza habari njema ya lile neno. 5 Sasa Filipo akashuka kwenda jiji la Samaria akaanza kuwahubiria kumhusu Kristo.
Umati wote kwa pamoja ulikazia fikira mambo ambayo Filipo alikuwa akisema huku wakisikiliza na kutazama ishara alizokuwa akifanya. 7 Kwa maana wengi walikuwa na roho waovu, na roho hao walipaza sauti kubwa na kutoka. Isitoshe, wengi waliokuwa wamepooza na vilema waliponywa. 8 Basi kukawa na shangwe kubwa sana katika jiji hilo.

Acha kukalilishwa na Mwamposa na doctrine ya mafuta, udongo, na maji. Utasema mbona Bwana Yesu alitumia udongo?. Swali hili ni sawa na kusema mbona Petro alitembea juu ya maji ati nawe uende ziwani utazama. Imani na utendaji wa Roho hauna mfanano Katu kuna uniqueness bali msingi ni katika kumuinua Kristo
 
Uko sahihi kabisa. Hata mitume wa YESU KRISTO hawakufanya huduma ya upako wa mafuta. KRISTO aliagiza watu wabatizwe kwa maji.

Lakini fahamu kwamba kusema ukweli au kukemea maovu ndani ya jamii sio "kuhukumu". Kuhukumu ni kutoa adhabu kwa muhusika. Na sisi hatujatoa adhabu yoyote ile kwa Mwamposa.
YESU alibatiza kwa Roho, ndo maana yohana mbatizaji alisema mim nabatiza kwa maji Ila Yuko anayebatiza kwa Roho atakuja akimaanisha YESU
 
huyu ndugu ninamfahamu tangia akiwa kijana alipotoka tukuyu safari yake ya huduma kabla hajafahamika ilianzia tunduma akiwa na sambamba na mchungaji efraim mwaitebele wa kanisa la restoration bible church tunduma ,alikuwa mpenda maombi sana hasa ya kwenda milimani, alikuwa anafanyabiashara pale soko la black tunduma amewahi kuuza viatu pia, kwa sisi vijana wa kipindi kile maombi mengi tulikuwa tunafanyia milimani,mwamposa alikuwa kiongozi wa maombi nawakumbuka vijana kama pasta mwankenja ambae kwa sasa ni mchungaji kitunda tulikuwa nao pamoja .badae alipata wito akawa anaalikwa sehemu mbalimbali kanisa lake kubwa na mahali watu walianza kumjua ni moshi ,pale jamaa alipiga kazi sana na alikuwa na waumini wengi mno sikuwahi fikiria kama angehama moshi.inasemekana badae ilitokea migogoro flani ya kifamilia kati yake na mke wake,mwamposa aliamua kuondoka moshi kwa hasira na kuamua kwenda dar kuanza huduma upya.haikuwa kazi rahisi maana alikuwa hana hata mahali pakufanyia huduma,alianzia sebulen kwa mtu akiwa n
Anakama miaka 50
 
Kabla hajafika sinza alikuwa anafanya ibada zake kwenye hema chafuchafu pale moshi, ndani ya soko la maimoria. Akawa anapaka watu mafuta, na kuwaombea kwa mafungu, mwenye milioni, mwenye laki 5 mwisho elfu 50 chini ya hapo hakuna maombi. Alipozichanga ndio akahamia huko sinza vatcan. Baadae akarudi kuchukua u phd kwa kukanyagisha watu mafuta ambapo kulipelekea watu 20 kuaga dunia.

Hapa ndo alitoa kafara la uhakika
 
Juz nilikuwa nasikiliza radio yake nikasikia anaagiza waumini wake waende kanisani na udongo kutoka eneo la nyumba wanazoishi, sehemu ya KAZI au biashara.


Nikasema Huyu ni tapeli kama Tapeli wengine WA Tandale.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Sio mafunzo pekee ndio mwamuzi

Yuda Iskariote akiposalisiti Yesu replacement yake kanisa lilifunga na kuomba Mungu nani ashike nafasi yake

Mungu akawaambia akawaonyesha kuwa mpeni Matiya

Sasa hivi mivyuo ya theolojia mtu akidoma mivyuo ya dini yao wanamuweka kazini bila hata kuomba Mungu kuwa huyo mtu kweli Mungu kamuita ili Mungu aseme mwenyewe sababu kazi ya kuweka wahudumu hudums tano yoyote ni yake

God factor imeachwa ndio masna makanisa ulaya na marekani waliingiza hadi mishoga kanisani kuwa mapadri au wachungaji matokeo ikapigania ndoa za jinsia moja na ushoga na usagaji ikiwa na mivyeti yoye ya digrii za vyuo vya theolojia vya dini zao
Hapa imethibitisha hujui biblia Ile nafasi ya yuda aliyetakiwa kuichukua ni Paulo na sio metiya, metiya alipatikana kwa wanafunzi kupiga Kura wala hawakumuomba Mungu
 
Alianza uinjilist wa kukaa na kuhubiri barabarani Mke wake akawa anaona aibu akasema tutafute kazi akasema hayupo tayari Mke wake akamtosa naye akajiwekea nadhiri kuwa hatuaacha kumtumikia Mungu hadi Ajue Mungu huyu ni nani ndiyo akampa hicho kipawa Chake..

I do not know lakini I think hadi leo hana Mke tena hata yule alipotaka kumrudi alikataaa.. A little I know though sina uhakika ready to be corrected
Yes mke hana,ila kuna mdada kazaa nae kamjengea kighorofa huku Goba Kulangwa,alafu ni wale wadada wa mjini kishenzi.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Naomba nijibu kidogo ulichosema.

1. Kwanza kuhusu Luka 9:49-50, Yule mtu walimkuta anatoa pepo kwa jina la Yesu Kristo. Hilo ndilo la muhimu, alitumia Jina la Yesu Kristo kutoa mapepo na sio maji Wala mafuta. Kama wanafunzi wa Yesu wangemdaka huyo jamaa anatumia maji kuponya watu basi jibu la Yesu Kristo lingeweza kuwa tofauti.

Lazima ujue kwamba kuendelea kutumia zana za upako ni dalili za kuonesha kwamba Jina la Yesu Kristo alijitoshelezi hivyo tunalisaidia kwa kutumia chumvi au maji au mafuta.

Kuna maeneo wanatumia Hadi pipi au keki za upako. Shida ipo wapi kutumia jina la Yesu Kristo?. Kwanini usitumie jina la Yesu pekee mpaka uanze kuwambia watu wakanyage mafuta na kunyunyiza mafata kwenye majumba yao?.

Kazi ya shetani ni kulishusha jina la Yesu Kristo na kulifanya halina nguvu.

2. Pili, kuhusu Waefeso 4:11-13. Lazima uelewe zile ni huduma tano.
Mitume
Manabii
Waalimu
Wachungaji
Wainjilisti

Hizo huduma tano unapewa na Mungu sio unajipa mwenyewe. Baada ya kuokoka na ukajazwa Roho Mtakatifu Kuna huduma Mungu anakupa na wewe utaifahamu maana itakuwa ina imba ndani yako. Sasa hizi ni huduma sio vyeo au ngazi za madaraka.

Naomba nitoe mifano;

A. Kwanza mitume, mitume kazi yao kubwa ni kutembea ulimwenguni kote na kufungua kazi ya Mungu. Tena hutakiwa kwenda maeneo yaliyoshindikana au yasiyomjua Kristo Yesu. Ndio maana Paulo Kama mtume alitembea karibia dunia nzima akifungua kazi ya Bwana Hadi uarabuni. Sasa Leo tuna mitume wa vyeo sio huduma, ndio maana utakuta mtu anajiita mtume ila anasimamia kanisa. No mtume kwa huduma Hana kanisa bali anazunguka sehemu mbali mabli kufungua makanisa. Mitume wanatakiwa kwenda Somalia au Sudan au Iraq ambako injili haijafika, lakini leo ili utambulike kama mtume lazima ufanye miujiza au uponyaji basi.

B. Pili, manabii, manabii kihuduma Ni Jicho na mdomo wa Mungu. Kihuduma nabii hawezi kuchunga kanisa , Bali anaweza kuwa mshirika wa kawaida kanisani lakini mwenye uwezo wa kuona mambo ya mbele au mambo ambayo wengine hatuyaoni. Pia nabii husema Yale ambayo Mungu anataka kuonya kanisa au nchi au kundi fulani etc. Hivyo nabii kihuduma sio wa kuchunga kanisa bali kutoa mafunuo ambayo yanatoka kwa Mungu, kunifahamisha taifa yatakayokukuta mbele, kulionya taifa kuhusu dhambi na etc. Hivyo ni muhimu kuwa na huduma ya kinabii kanisani ili kanisa likomae.

Tatizo ni kwamba unabii wa Leo umekuwa ni cheo. Unabii Kama hudumu ni mchache Sana, ndio maana manabii wengi Leo hawaoni ya mbele au kkusema ya kutoka kwa Mungu ili kunenga ufalme wake. Utasikia Nabii anakuuliza unanifahamu au tunafahamian, anaanza ninakuona upo Mwanza, Mara naona jina Grace halafu watu wanachanganyikiwa. Kuna uganguzi na unabii. Uganguzi unabase kwa mwanadamu basi ila unabii ni kutoka mbinguni ili kuujenga ufalme wa Mungu duniani na kuonya kuhusu dhambi.

Niishie hapo kwa leo, ila ni muhimu kutofautisha utume na unabii wa kihuduma na utume na unabii wa kicheo.
Kuna Mzee kila usiku saa nne sio Mara zote ni baadhi ya siku utamkuta na maji ya upako ya mwamposa anamwaga kwenye ukuta wake swali ambalo najiuliza kwanin asitumie jina la YESU au damu ya YESU kukilinda nyumba, inamaana anaamin maji ya upako kuliko damu ya YESU ukishaona hivyo uju Kuna shida mahali kubwa sana

Lengo la shetani ni kuhakikisha wakristo hawatumii either jina la YESU au damu ya YESU na watumia vitu vingine, kwa shetani hakuna vitu ambavyo ni tishio kama jina la YESU au damu ya YESU na mpaka sahivi ameshafanikiwa pakubwa sana

Mafuta ya upako na vitu vingine vyote vyenye jina la upako havina tofauti na mtu anayeabudu sanamu
 
Back
Top Bottom