Mkuu, maandiko hayajawahi kupinga miujiza mikubwa mikubwa kutokea kwa watu, bali imeonya kuwa hata wasio wa Mungu wanatenda hayo. Maandiko yametuonya tuyapime yote na kama yametokana na Mungu. Ni kosa kubwa sana kujenga msingi wa imani yako kupitia miujiza, ziko sababu nzito tu za kimaandiko.
1. Miujiza ni lazima imbadili mtu imani yake. Hili ni kubwa zaidi, tunaona kwa hiki kizazi cha manabii Waislamu na wapagani wengine wakipokea miujiza na kurejea kwenye imani zao. Wengine wengi wamejenga imani zao kwa mwamposa na maji na mafuta anayotoa. Hii ni hila ya shetani kabisa.
2. Miujiza ya mbinguni imelenga kumpa Mungu utukufu kwa sababu Mungu wa mbinguni hashiriki utukufu wake na kiumbe. Licha ya kauli ya kisanii "nani mtenda miujiza? ", lakini ni ukweli usio shaka wafuasi wa Mwamposa humpa utukufu yeye.
3. Msikilize vema Mwamposa, ni mhubiri mzuri sana wa miujiza na mafanikio. HAHUBIRI INJILI YA UFALME WA MBINGUNI. Wafuasi wake WOTE ni genge la wasaka mafanikio na afya pekee, kwani huhubiri habari za uzima ujao na maisha baada ya kifo. Huyu ni mtu hatari mno kwa ufalme wa mbinguni kwani anawafungia watu mlango wa mbinguni kwakuwaahidi raha ya hapa duniani.
4. Baada ya kushuhudia miujiza wafuasi wake hutoka bila uwezo wala upeo wa kumhubiri Kristo badala yake wana nguvu na mamlaka ya kuhubiri uweza wa Mwamposa kuponya. Hii inasababishwa na kutofundishwa neno la uzima bali majigambo na majivuno ya mhubiri kuponya. Wafuasi wake bila kujua hujifanya mabalozi wakubwa wa Mwamposa kwa watu wengi huku wakimnadi ni jinsi gani anaweza kuponya na kukupatia mali nk. Hii ni hila ya shetani.
Yako mengi ambayo ningeweza kuyaandika hapa lakini naishia hapo nisikie unajibu vipi hoja hizi za kimaandiko.