Dahh hawa manabii hadi wenyewe Kwa wenyewe wanapigana majungu, nipo nyumbani hapa natazama kipindi cha chomoza
Waliunganisha Kanisani kwenye ibada,Kuna Nabii anaitwa Philbert Paschal, na somo alilokuwa anahubiri siku ya leo ni "MAARIFA" baada ya kuona neno maarifa nikasema ngoja niweke Kambi nisikie atahubiri vipi kuhusu Maarifa
Kama kawaida Kwenye Bible kuna andiko linasema Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa, ehhh nikasema hapa hapa ngoja nikae vizuri
Ohhhh si akaanza yani unaenda kanisani unaambiwa sasa hivi tunaanza kombea wachawi wanaotembea mguu mmoja, unaambiwa sasa tunaanza kutoa Nyoka, unaambiwa uombewe Kwa sababu umefungwa na uchawi
Omba Mungu Kwa Akili sio kila kila siku unaomba Kwa roho, jtatu,jnne,jtano, Alhamisi,ijumaa,jmosi we unaomba tu kwa roho, aisee utakuwa ni Yule Mungu aliesema unaangamia kwa kukosa maarifa
Jiombee mwenyewe upate Akili jiombee mwenyewe upate maarifa maana ukipata maarifa huwezi kudanganywa hovyo hovyo,ukipata maarifa huwezi kutumika hovyo hovyo
Alafu baada ya kipindi kuisha yakaanza matangazo ya watu wanaotoa ushuuda tena kama tu vile inavokuwa Kwa Mwamposa, mara mtu aliombewa akapata kazi,mara mtu aliombewa akapata watoto, chini anapitisha namba ya kutuma sadaka ukiguswa na mahubiri yake
Ukiangalia lengo la wanaojiita manabii wote ni kama vile wanafanana tu, sasa wanaenda mbali hadi kuanza kupigana majungu wakiwa Live katika ibada, maana ni wazi kuwa prophet Philbert paschal alikuwa anamuongelea Mwamposa kuwa waumini wake wanaangamia Kwa kukosa maarifa
Kama Akili yako itakuwa huru, mawazo yako yatakuwa huru, basi ukimskiliza huyu Dk Ellie wa kipindi cha chomoza Clouds atakusaidia kubadirisha mtazamo/uelewa wako kuhusu IMANI, maana jamaa ana madini sana na hafungamani na upande wowote