Watu ni wapumbavu sana kuhusu uwezo Wa Mungu.
Hiví Kuna MIUJIZA unaozidi sayansi.Lakini haitumiki kujisifia eti MIUJIZA ya Kutoa mapepo Kwa vitambaa. Aliyetengeneza Ndege inapata hewani ikiwa na abiria mia Tano na mizigo lakini hakuna MTU anayejisifu kuwa Njooni tuone MIUJIZA ya kuwapeleka watu kutoka bara moja mpaka lingine?
Ndege ni kitu kinachoonekana lakini waliopewa Maarifa ya kutengeneza wamepewa na Mungu kama wanaotengeneza MAFUTA ya Kutoa mapepo na kuleta bahati Kwa kuvuta majini.
MTU yeyote akitumia yale MAFUTA anapata kile anachokinuia mana ni mafutaa yanayotengenezwa na watu wenye Elimu ya majini na hulka zake.
Sasa wakiambiwa hawaelewi wanashupaza shingo ZAO walisema ni MIUJIZA ya Mwamposa. Yale MAFUTA Hata yeye anayanunua. Kabla Hata ya Ukristo yalikuwepo na yapo Hata Kwa jamii za kipagani HIVYO kuyaunganisha na Ukristo ni kukosa Maarifa tu na ujinga.
Ni Mbingu tu za Waganga Wa Kienyeji walioamua kuhamia Kwenye majengo wanayoyaita makanisa. Ni Sawa na Babu Wa Loliondo Enzi zake na Kikombe kimoja .
MTU anatumia kitambaa Kutoa majini lakini hawezi kutibu Malaria Kwa kitambaa.
Hawezi kumponya majeruhi aliyevunjika mguu Kwa kitambaa mpaka akafanyiwe operation na madaktari Wa mifupa.
Huyo mungu Wa vitambaa anachagua magunjwa au amezidiwa. Kitambaa kimetengenezwa na mchina halafu eti kina nguvu ya kutibu magonjwa lakini hakitibu Ebola au kipindupindu au hakiwezi kufumbua mvipofu macho Yao .
Ni Waganga Wa Kienyeji kama Waganga Wengine mana wale wakienyeji nao hutumia Jina la Mwenyezi MUNGU kutibu.
Wajapani wameendelea sana Lakini Hawana mambo ya kuuziana vitambaa vya upako.
Waafrika wanahitaji kufundishwa uaminifu ,uadilifu, Upendo,huruma, utu, Kutoa sadaka Kwa Ajili ya kusadia maskini na KUFANYA KAZI Kwa uaminifu na Kwa bidii. Hakuna MIUJIZA zaidi ya Hapo. Watu wanajamiiana hovyo,wanatupa takataka hovyo Hali inayosababisha magonjwa na mazalia ya Mbu na wadudu Wengine, wanatukanana na kuudhiana Kila mara, umaskini na stress za maisha, watu wanalogana na kutiliana fitina, watu Wana chukiana na kubaguana halafu wanadanganywa kuwa tiba ya matatizo Yao ni MAFUTA na vitambaa . Ujinga mtupu.
" Mwenyezi MUNGU alitangulia kusema "Watu wangu wanaangamizwa Kwa kukosa maarifa".
Wanaangamizwa na Shetani na Mawakala wake Kwa sababu tu watu Hawana Maarifa juu ya maisha yanayowazunguka kiimani na kimaarifa. Maarifa SIO vitambaa Bali ni Namna ya KUFANYA Biashara ya vitambaa. YAANI MTU amebuni mradi Wa vitambaa na MAFUTA na amepata soko la uhakika.