Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

naomba unithibitishie ni mganga yupi wa Kienyeji ambaye amemponya mtu akajitokeza hadharani na kusema ameponywa na mganga Fulani? au unaongelea hawa wanasiasa wanaotoa kafara ya ufumbaji wa macho wapiga kura? au?

Kwa kifupi hakuna Mganga wa Kienyeji yeyote ambaye anaweza kuponya Ugonjwa .. Yeye atatibu ila hawezi kumponya.. Mwenye uwezo wa Uponyaji ni Mmoja tu naye niyule aliyempa uhai huyo mganga na huyo Mgonjwa tu ambaye Ni Mungu.
Unajua kwanini waganga hawaishi?
 
Basi kwa hili hakuna imani salama..mana zote zimejengwa kwenye hiyo misingi.

#MaendeleoHayanaChama
Ni kweli, dini ya kweli ni akili yako inayokuunganisha na Mungu (Asili/ Nature).
Huna akili, huna uhusiano na Mungu, utababaishwa na manabii wa uongo na waganga, mwisho wako kwa ibilisi/ jehanam au kuangamia.
 
Kwa mwamposya ulishafika ? Sehemu hata ya kupaki magari shida siku ya jumapili hakuna kanisa lina matajiri wenye magari mengi hadi Park shida kama kwa Mwamposya pamoja na kuweko kiwanja kikubwa sana cha kupaki

Jumapili barabara zote kwenda kanisani kwake hujaa foleni za,magari na wasababishao ni wenye magari waumini wa Kwa Mwamposya waendao kwa Mwamposya au kutoka ibadani

Mimi pia nasali kwake

Maskiki aweza miliki magari ya uhakika la kwenda na kurudi kanisani kwa Mwamposya?

Nenda mwenyewe ukaangalie.Watu wengi wanasali kule ni wenye pesa zao na elimu zao na wana exposure kubwa za kimataifa

Hakuna mtu wa kulaghaiwa

Pale sadaka kukusanywa milioni 50 ibada moja wala sio kitu kikubwa ndio maana unaona yuko kwenye TV,Radio nk watu wanatoa sana kama shukrani ya kutatuliwa changamoto zao

Mtu akitatuliwa changamoto yake kuna matajiri kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu ya milioni 100 ni kitu kidogo mno pale na hawapigi yowe kama wa kwenu huko akitoa elfu moja tu kelele kibao na akitoa elfu 10 sadaka mchungaji au padri anamwabudu huyo mtoa elfu 10

Kama unafikiri kwa Mwamposya wamejaa maskini wa Mali tembelea jumapili yeyote usiingie kanisani pita nje tu ndipo utajua wasali ni watu wa aina gani angalia Park ya magari
Watu wenye akili nzuri ni wachache sana,.
Elimu na utajiri(wa muda), hata majinga na mapumbavu mengi yanayo.
Kweli huwaweka huru wenye akili nzuri inayowaunganisha na Mungu.
Wamelaaniwa wanaomtegemea mwanadamu.
 
Mleta mada nimemwelewa vizuri hatimaye anachotaka kujua Ni Mwamposya katokea wapi kihuduma,baba yake wa kiroho nani aliyemkuza kufikia hapo na elimu yake ya theolojia alusoma wapi na aliwekwa wakfu na nani kuwa na huduma hiyo

Nijibu miswali hiyo ya kidini ya kifarisayo kama ifuatavyo .Mitume waliamini sana kuwa mtu kuwa mhudumu wa Yesu lazima apitie taratibu walipitia wao!!!

Luka 9:49-50​

Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”50Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.

Hajapitia mivyuo yao ya theolojia wakamzuia yule hakuwemo kundi la mitume 12 walioa attend chuo cha Yesu darasani kwao hawajawahi muona au kwenye kidini chao

Yesu akasema ninyi hamumujui mimi.namjua

Ndio maana kazi ya kuweka nani awe kwenye huduma yeyote kati ya tano kazi hiyo hajakabidhi kwa kanisa hasa kabaki nayo mwenyewe mtu alyepewa na Mungu Mwenyewe rahisi kumjua kuliko aliyejipa au kupewa na dini yake kisa kasoma lichuo lao lan theolojia Kazi ya kuweka watumishi Mungu wa kweli Mungu kabaki nayo mwenyewe

Efeso 4:11-13​

Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Waliowekwa na Mungu mwenyewe utaona matokeo na kazi zao.Yesu Mwenyewe alitamka kama hamjuamini angalieni kazi nitendazo

Kanisa lolote kama linadhani laweza pora kazi ya Mungu ya kusimika wahudumu wa kanisa hakitaweza yeye ndie huweka

Kanisa likiweka wake mbeleni lazima wataonaekana kupwaya watashangaa akina Mwamposya ambao hawakusoma mivyuo yao ya theolojia na mitaratibu yao ya kidini yao wanawapiga bao!!

Tatizo la kanisa ineonekana ni kudhani lenyewe ndio lenye mamlaka ya kuweka wahudumu wa huduma tano.Wakati Biblia inaeleza wazi kuwa hiyo ni kazi ya Mungu

Hata mitume kabla kuweka mtu huduma walifunga waliomba na kuongea na Mungu kabla kumwekea mikono mtu kuwa mhudumu huduma yeyote kati ya tani sasa hivi sifa maliza tu chuo cha Biblia au thelojia na kutimiza Vigezo vya kidini wanakupa huduma iwe upadri au huduma tano yeyote!!
Hao mitume hawakuibukia tu kama uyoga.

Yesu aliwachagua mwenyewe. (Vetting).

Akaaa nao kipindi chote kabla ya kupaa. ( walipitia training).

Hivyo ni muhimu sana kupata mafunzo na kukidhi vigezo vya kazi husika kabla ya kuifanya.
 
Hata Nabii Tito alikuwa na mashabiki , ila walipomgundua wakamkimbia.
 
Hao mitume hawakuibukia tu kama uyoga.

Yesu aliwachagua mwenyewe. (Vetting).

Akaaa nao kipindi chote kabla ya kupaa. ( walipitia training).

Hivyo ni muhimu sana kupata mafunzo na kukidhi vigezo vya kazi husika kabla ya kuifanya.
Sio mafunzo pekee ndio mwamuzi

Yuda Iskariote akiposalisiti Yesu replacement yake kanisa lilifunga na kuomba Mungu nani ashike nafasi yake

Mungu akawaambia akawaonyesha kuwa mpeni Matiya

Sasa hivi mivyuo ya theolojia mtu akidoma mivyuo ya dini yao wanamuweka kazini bila hata kuomba Mungu kuwa huyo mtu kweli Mungu kamuita ili Mungu aseme mwenyewe sababu kazi ya kuweka wahudumu hudums tano yoyote ni yake

God factor imeachwa ndio masna makanisa ulaya na marekani waliingiza hadi mishoga kanisani kuwa mapadri au wachungaji matokeo ikapigania ndoa za jinsia moja na ushoga na usagaji ikiwa na mivyeti yoye ya digrii za vyuo vya theolojia vya dini zao
 
Sio mafunzo pekee ndio mwamuzi

Yuda Iskariote akiposalisiti Yesu replacement yake kanisa lilifunga na kuomba Mungu nani ashike nafasi yake

Mungu akawaambia akawaonyesha

Sasa hivi mivyuo ya theolojia mtu akidoma mivyuo ya dini yao wanamuweka kazini bila hata kuomba Mungu kuwa huyo mtu kweli Mungu kamuita ili Mungu aseme mwenyewe sababu kazi ya kuweka wahudumu hudums tano yoyote ni yake

God factor imeachwa ndio masna makanisa ulaya na marekani waliingiza hadi mishoga kanisani kuwa mapadri au wachungaji matokeo ikapigania ndoa za jinsia moja na ushoga na usagaji ikiwa na mivyeti yoye ya digrii za vyuo vya theolojia vya dini zao
Yuda alikua na jukumu lake maalum.

Yesu alimchagua na alifahamu kuwa hiyo ndio kazi yake.
 
Hajakosoa kipawa, Bali kasema kwamba kipawa kinakaa ndani ya mtu sio kwenye mafuta na udongo au maji.
Kinaweza tumika kwa namna mbalimbali. Yesu alitemea mate udongo akampaka mtu akaona. Eliya/Elisha alimwambia mtu akaoge mto yordan mara 7. Na mafuta yamezungumziwa mara nyingi ktk biblia kuwapaka wagonjwa, wafalme n.k na hata sisi Waroman huwa tunapakwa mafuta wakati flani mapadre.
 
Yuda alikua na jukumu lake maalum.

Yesu alimchagua na alifahamu kuwa hiyo ndio kazi yake.
Mpaka leo Yesu ndio anatakiwa kuwa consulted nani aingie kwenye utumishi kanisani wa kudumu hata kama kamakiza midomo yote ya kidini vyuo vya theokojia vya kidini na kufaylu viwango vya juu mno
 
Hapa unamtetea Mwamposa sio Mungu.
Unatetea matumizi ya maji na mafuta.
Hata hili hujui kutofautisha?
Lakin anatumia mafuta na maji kwa jina la nani jomba
 
JF,

Kwa heshima na taadhima ningependa kujua Nabii Mwamposa amefikaje fikaje hapo alipo na namna Mungu anavyoendelea kumtumia.

Nadhani ni muhimu watumishi Hawa wawe wanatuwekea historia zao ili kuweka mazingira halisi ya mahusiano yao na Mungu wetu kabla ya kufikia hatua hiyo...wengine utakuta waliishi maporini na milimali wakimtafuta.

Mungu kabla hawajafanikiwa
Mwamba alipambana Sana. Mwacheni ale mema ya Mung u.
 
Attachments

  • IMG_20220831_142831.jpg
    IMG_20220831_142831.jpg
    77.3 KB · Views: 17
Kuna namna mbili ya kuwapima watu ea Mungu
1. Mtazamo wa kibinadamu , ambapo kwa mtazamo huu hakuna mbinguni, dunia wala kuzimu aliekamilika mbele za watu wote.
2. Mtazamo wa Mungu: hapa unaweza pata watu waliokamilika, Mungu mwenyewe malaika na wanadam wenye kumpendeza.

Anachokifanya mwamposa sio kigeni
hata Yesu mwenyewe alikua akiongelewa hivi.

Yohana 7:45-52
[45]Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?

[46]Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.

[47] Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! NYINYI NANYI MMEDANGANYIKA?

[48]Ni NANI KATIKA WAKUU AMWAMINIYE, AU KATIKA MAFARISAYO?

[49] LAKINI MAKUTANO HAWA WASIOIFAHAMU TORATI WAMELAANIWA.

[50]Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),
[52]Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.
 
Kinaweza tumika kwa namna mbalimbali. Yesu alitemea mate udongo akampaka mtu akaona. Eliya/Elisha alimwambia mtu akaoge mto yordan mara 7. Na mafuta yamezungumziwa mara nyingi ktk biblia kuwapaka wagonjwa, wafalme n.k na hata sisi Waroman huwa tunapakwa mafuta wakati flani mapadre.
Nashkur kwa ufafanuzi huu mujarab..Sasa ngoja tuwasikilize wenye mawazo tofauti
 
Kuna namna mbili ya kuwapima watu ea Mungu
1. Mtazamo wa kibinadamu , ambapo kwa mtazamo huu hakuna mbinguni, dunia wala kuzimu aliekamilika mbele za watu wote.
2. Mtazamo wa Mungu: hapa unaweza pata watu waliokamilika, Mungu mwenyewe malaika na wanadam wenye kumpendeza.

Anachokifanya mwamposa sio kigeni
hata Yesu mwenyewe alikua akiongelewa hivi.

Yohana 7:45-52
[45]Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?

[46]Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.

[47] Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! NYINYI NANYI MMEDANGANYIKA?

[48]Ni NANI KATIKA WAKUU AMWAMINIYE, AU KATIKA MAFARISAYO?

[49] LAKINI MAKUTANO HAWA WASIOIFAHAMU TORATI WAMELAANIWA.

[50]Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),
[52]Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.
Nimekuelewa jomba
 
Hao mitume hawakuibukia tu kama uyoga.

Yesu aliwachagua mwenyewe. (Vetting).

Akaaa nao kipindi chote kabla ya kupaa. ( walipitia training).

Hivyo ni muhimu sana kupata mafunzo na kukidhi vigezo vya kazi husika kabla ya kuifanya.
Umesoma na kuelewa hiyo
Luka 9:49-50 ?
 
Back
Top Bottom