Mleta mada nimemwelewa vizuri hatimaye anachotaka kujua Ni Mwamposya katokea wapi kihuduma,baba yake wa kiroho nani aliyemkuza kufikia hapo na elimu yake ya theolojia alusoma wapi na aliwekwa wakfu na nani kuwa na huduma hiyo
Nijibu miswali hiyo ya kidini ya kifarisayo kama ifuatavyo .Mitume waliamini sana kuwa mtu kuwa mhudumu wa Yesu lazima apitie taratibu walipitia wao!!!
Luka 9:49-50
Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”50Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.
Hajapitia mivyuo yao ya theolojia wakamzuia yule hakuwemo kundi la mitume 12 walioa attend chuo cha Yesu darasani kwao hawajawahi muona au kwenye kidini chao
Yesu akasema ninyi hamumujui mimi.namjua
Ndio maana kazi ya kuweka nani awe kwenye huduma yeyote kati ya tano kazi hiyo hajakabidhi kwa kanisa hasa kabaki nayo mwenyewe mtu alyepewa na Mungu Mwenyewe rahisi kumjua kuliko aliyejipa au kupewa na dini yake kisa kasoma lichuo lao lan theolojia Kazi ya kuweka watumishi Mungu wa kweli Mungu kabaki nayo mwenyewe
Efeso 4:11-13
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo
Waliowekwa na Mungu mwenyewe utaona matokeo na kazi zao.Yesu Mwenyewe alitamka kama hamjuamini angalieni kazi nitendazo
Kanisa lolote kama linadhani laweza pora kazi ya Mungu ya kusimika wahudumu wa kanisa hakitaweza yeye ndie huweka
Kanisa likiweka wake mbeleni lazima wataonaekana kupwaya watashangaa akina Mwamposya ambao hawakusoma mivyuo yao ya theolojia na mitaratibu yao ya kidini yao wanawapiga bao!!
Tatizo la kanisa ineonekana ni kudhani lenyewe ndio lenye mamlaka ya kuweka wahudumu wa huduma tano.Wakati Biblia inaeleza wazi kuwa hiyo ni kazi ya Mungu
Hata mitume kabla kuweka mtu huduma walifunga waliomba na kuongea na Mungu kabla kumwekea mikono mtu kuwa mhudumu huduma yeyote kati ya tani sasa hivi sifa maliza tu chuo cha Biblia au thelojia na kutimiza Vigezo vya kidini wanakupa huduma iwe upadri au huduma tano yeyote!!