Alikuwa mfanyabiashara, akaacha biashara, akaanza utume akiwa Moshi chini ya ulezi wa Askofu Dastan Maboya wa Arusha. Kanisa la kwanza alianzisha Moshi viwanja vya maimoria, likakuwa ila bado alikuwa chini ya Askofu Maboya.
Akapiga hesabu akaona akimbilie Dar akaenda kuanzisha kanisa eneo ambalo usingewaza kama kungegeuka kanisa, kifupi jamaa alicheza kama Pele, akaruhusu kuja kanisani utakavyo, akapata waumini wengi.
Akaja na agenda ya mafuta, baada ya Dar watu wengi kutokumiliki ardhi, udongo sio dili huko, akapata wazo la kukanyaga mafuta likawa ndio kama utambulisho wake rasmi, mwamba anazidi toboa tu.
Huyo ndio bulldoza ninayemfahamu mimi kwa ufupi.