Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Anapokosea
1. Hajaombea watu Sala ya Toba
2. Hajawahi batiza
3. Hajawahi ombea watu wajazwe Roho Mtakatifu.
4. Hajawahi fundisha watu kuishi utakatifu na kwenda mbinguni.
5. Anasema Yesu ni WA dhehebu zote yaani hata ukiwa mpagani wewe pokea mafuta kaendelee na maisha Yako.

Je Kuna kipawa cha kupotosha injili?
Kimsingi yeye injili yake ameijenga kwe helaa na uponyaji,juuu ya kukemea dhambi hiyo usimuulizee
 
Huna Hoja kuoa sio Lazima
Mtu wa Mungu Yesu Mbona hajaoa?!
Yesu hakuwahi kuoa wala kujihusisha na wanawake kabisa,. Mwamposa alioa na alizaa maana yake ni rijali ana matamanio ya kimwili
 
Ila ingekuwa katoliki wangetangazwa kuwa watakatifu ili mradi wamefia kanisani. Hakuna kanisa lenye usanii Kama katoliki na mapadre wao walawiti
Vipi yule jabir wa geita aliekuwa anafundisha watoto wadogo kuwa mashoga mnatangaza lini kuwa mtume?
 
Hawata kuelewa.
Wote wanaojiita mitume na manabii most of them ni fake
kabisa....ukisoma Biblia manabii walikuwa govermental. kazi yao ilikuwa kuona masuala mazito kwa ajili ya taifa na kuwashauri watawala/wafalme. leo hawa wahuni kazi yao ni kuuza maombi na bidhaa na kutafuna wake za watu kisha wanajiita manabii.

mtu hujawahi kulitabiria taifa hata jambo moja kisha unajiita nabii
 
Kipindi hicho Yeau alikuwa hajadhirishwa.

Soma kwa umakini Ebrania Sura ya 5
Umeongea point ambayo ni wachache watakuelewa YESU alivyotoa damu yake inatakiwa tuitumie hiyo na sio kitu kingine tatizo watu wamestuck kwenye agano la kale na wakati tupo agano jipya
 
Mkuu, maandiko hayajawahi kupinga miujiza mikubwa mikubwa kutokea kwa watu, bali imeonya kuwa hata wasio wa Mungu wanatenda hayo. Maandiko yametuonya tuyapime yote na kama yametokana na Mungu. Ni kosa kubwa sana kujenga msingi wa imani yako kupitia miujiza, ziko sababu nzito tu za kimaandiko.

1. Miujiza sio lazima imbadili mtu imani yake. Hili ni kubwa zaidi, tunaona kwa hiki kizazi cha manabii Waislamu na wapagani wengine wakipokea miujiza na kurejea kwenye imani zao. Wengine wengi wamejenga imani zao kwa mwamposa na maji na mafuta anayotoa. Hii ni hila ya shetani kabisa.

2. Miujiza ya mbinguni imelenga kumpa Mungu utukufu kwa sababu Mungu wa mbinguni hashiriki utukufu wake na kiumbe. Licha ya kauli ya kisanii "nani mtenda miujiza? ", lakini ni ukweli usio shaka wafuasi wa Mwamposa humpa utukufu yeye.

3. Msikilize vema Mwamposa, ni mhubiri mzuri sana wa miujiza na mafanikio. HAHUBIRI INJILI YA UFALME WA MBINGUNI. Wafuasi wake WOTE ni genge la wasaka mafanikio na afya pekee, kwani huhubiri habari za uzima ujao na maisha baada ya kifo. Huyu ni mtu hatari mno kwa ufalme wa mbinguni kwani anawafungia watu mlango wa mbinguni kwakuwaahidi raha ya hapa duniani.

4. Baada ya kushuhudia miujiza wafuasi wake hutoka bila uwezo wala upeo wa kumhubiri Kristo badala yake wana nguvu na mamlaka ya kuhubiri uweza wa Mwamposa kuponya. Hii inasababishwa na kutofundishwa neno la uzima bali majigambo na majivuno ya mhubiri kuponya. Wafuasi wake bila kujua hujifanya mabalozi wakubwa wa Mwamposa kwa watu wengi huku wakimnadi ni jinsi gani anaweza kuponya na kukupatia mali nk. Hii ni hila ya shetani.

Yako mengi ambayo ningeweza kuyaandika hapa lakini naishia hapo nisikie unajibu vipi hoja hizi za kimaandiko.
Yaani I took time to watch him akiwa Geita na Musoma, Mwanzo hadi Mwisho. Sikuwahi kusikia tubuni na kuamini Injili, Mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Zaidi ya Miujiza ya kupaka Mafuta na kumwaga Maji na kukutana na Mazingaombwe. Then watoe Sadaka za Kujimaliza. Na kuwaambia Watu hawafanikiwii Kwa kuwa Wamelogwa. Mtumishi wa aina hii Noooooooo!
 
kisha akenda nigeria kupewa huo unabii baada ya hapo akahamia dar kwenye vinono vingi? usisahau hili
Nigeria ndio yalikuwa makao yao makuu kwa yule nabii wa uongo aliyefariki.
Siku hizi wameadvance sio lazima kuenda Nigeria popote ulipo wapo
 
Ana muhubiri Yesu wake wa mafuta na maji anaetaka kuchanganywa Ili afanye Kazi na sio Yesu wa Nazareth asiyechanganywa.
 
Hayo ni kweli lakini Yale SIO mafuta ya upako ni mafuta yanayotengenezwa kwa formula za kushirikina.
Na zinajukana . MTU yeyote anaweza kuyanunua Kwa maustadhi na yanafanya KAZI Kwa Hiyo SIO upako Wa Kikristo Bali ni mchanganyiko Wa mitishamba kama Dawa nyingine za kisuna. KUWADANGANYA watu Kuwa ni upako Wa Roho Wa MUNGU ni kupotosha na kumwandolea MUNGU sifa za Upekee.

Natamani kuwaambia ukweli Wakristo wenzangu mana wamepotoka sana. Uliona Mashekhena ubwabwa wameenda kumuunga mkono Nabii Mkuu . Ni Muislam Gani anayekubali Kuwa kuna Nabii mwingine baada ya Nabii Mohamad (SAW)? Wale ni wataalam Wa Dawa za Kisuna wanajua Kuwa zipo Dawa za Kisuna na za majini zinazotumiwa kutibu Kwa uwezo Wa Allah MTU akapona mana Kila kitu alikiumba yeye na akaumba Dawa za Kila Ugonjwa Katika miti aliyoiumba ?


Nikuulize Swali ?

Hiví Unaonaje kama Madaktari Wa Muhimbili wangesema Kuwa tunatibu Kwa Jina la Yesu ! Njooni Juma Pili mlete wagonjwa wenu WOTE waliovuniika miguu ,wenye matatizo ya macho tuna macho ya KIROHO,macho ya upako Yaani miwani. Wakati huo binadam wawe hawajapata elimu Juu ya sayansi rasmi ya tiba ? Je, watu wasingefurika Muhimbili nakujua Kuwa ni Imani ya Kikristo kutibu Kumbe ni sayansi ya Kigiriki na Kirumi ?

Kwa Sasa Imani zimegubikwa na Sayansi ya Kale ya MISRI .
Wayahudi wamegubikwa na Sayansi ya Kimisri ikiwemo Mussa Aliyekulia Kwa Faraoh kama Mtoto Wa Mfalme. Mussa alijua sayansi na ushirikina WOTE mana alikulia NDANI ya Ikulu ya Faraónh Lakini aliuacha akamwamini MUNGU Mmoja na Kupinga Imani za kishirikina . Waisraeli wengi walijua mbinu za wamisri za kishirikina lakini walikua wanaamrishwa waepukane nazo na wakawa wanatungiwa Sheria Kali sana kuachana nazo.
Musa alichelewa kurudi Toka mlimani Siku 40 tu Waisraeli wakaanza ibada za Sanamu Kwa kuchonga Sanamu ya Ng'ombe na kuiabudu.

MANABII WENGI WANATAMANI MIUJIZA LAKINI HAWATAIPEWA KAMWE NA MUNGU ANAACHA MAKUSUDI ILI KUWAJUA WATU WAKE HALISI. SASA WENGI WANAPOONA MUNGU ANACHELEWA KUJIBU MAOMBI YAO YA MIUJIZA WANAAMUA KUCHONGA SANAMU ZA NG'OMBE YAANI VITAMBAA ,MAFUTA ,KEKI, CHUMBI N.K. HIZI NI IBADA ZA WAMISRI. NA MPAKA LEO KULE MISRI KUNAVYUO VYA KICHAWI LAKINI KWA SABABU WANAFUNDISHA KWA KIARABU BASI WATU WANAJUA KUWA NI VYA KIDINI HIVYO KUNA WATU WENGI WANASOMEA KULE NA WANAJUA FOMRULA NYINGI ZA DAWA ZA KUONA ,KUFUGA NA KUTOA MAJINI. NDIZO WANAZOWAPA MANABII NA MAKRISTO WA UONGO WALIOCHOKA KUOMBEA KWA JINA LA YESU BILA MAFUTA NA KUONA KUWA WANATUMIA NGUVU KUBWA SANA KUOMBA NA HAKUNA MUUJUZA WALA NINI.
MAFUTA ni Ibada ya Sanamu.

YESU alimpaka MTU matope machoni kama Dawa lakini na kumwambia Kuwa Imani yake imemponya. Ile ilikuwa ni Dawa tu kama Panadol . Hakusema Kuwa ni matope ya upako.
Someni Vitabu .
Umeandika andiko refu lililojaa upuuzi na pumba.

#MaendeleoHayanaChama
 
Yaani I took time to watch him akiwa Geita na Musoma, Mwanzo hadi Mwisho. Sikuwahi kusikia tubuni na kuamini Injili, Mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Zaidi ya Miujiza ya kupaka Mafuta na kumwaga Maji na kukutana na Mazingaombwe. Then watoe Sadaka za Kujimaliza. Na kuwaambia Watu hawafanikiwii Kwa kuwa Wamelogwa. Mtumishi wa aina hii Noooooooo!
In short this guy is fake! Huhitaji hata dakika tano kujua ni wakala wa shetani
 
Kuoa ni lazima maana yule ni rijali, je mihemko yake ya kihisia anapeleka wapi?

Kwa maslahi ya waumini wake ilitakiwa amsamehe mkewe wawe pamoja
Ukioa wewe inatosha sana...sio kila mtu anawaka tamaa za ngono kama wewe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuhusu suala la huyu Mwamposa nina ushahidi kabisa ana muunganiko na nguvu za giza.
Kwa sababu kuna siku wakati yupo pale Sinza Vatican nilienda pale akawa anaombea watu na ilipofika kwangu akaniuliza shida yako nini? Nikamwambia nahitaji kazi na maombi nilishapeleka lakini bado kuitwa alichoniambia *NYOTA * zangu zimeshuka zipo chini akaniombea. Halafu kuna Uncle wangu ni Mganga wa Kienyeji haswaa huwa anatoa huduma kwa Viongozi wakubwa wa Serikalini na sifa zake zimewafikia mpaka Waarabu wa Oman, Doha, Bahrain, Qatar kote huko huwa anaenda kutoa huduma ya tiba na watu huwa wanafanikiwa. Sasa huyo Uncle wangu kuna siku nilikutana nae Sehemu ananua dawa kwenye maduka ya dawa za asili na yeye ndiyo aliyeniona akaniita. Tukazungumza pale akaniuliza vipi Kazi ulishaanza? Nikamwambia bado baada ya dakika kadhaa pale pale akaniambia Nyota zako chini.
Sasa Mwamposa aliniambia Nyota zangu zipo chini na huyu Mganga wa Kienyeji Naye aliniambia nyota zangu zipo chini. Kuna nini hapo?

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Nabii wa KWELI wa MUNGU hutenda miujiza kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU aliyepewa na MUNGU na siyo kwa uwezo wa "mafuta" au "keki" au kitu chochote kile. Tena siyo yeye anayetenda bali ni YULE ROHO wa MUNGU akaaye ndani yake.

Na huduma hiyo hutolewa bure kabisa bila malipo yoyote. YESU KRISTO alisema : "mmepewa bure, toeni bure". Na ndivyo akina Petro na mitume wengine walifanya zamani zile.

Huyo Mwamposa hana ROHO MTAKATIFU. Mwamposa ni mfanyaMAZINGAOMBWE anayetumia jina la YESU KRISTO kama kivuli.
 
Back
Top Bottom